Thursday, August 23, 2018

Mange Kimambi Amchamba Ray C Kisa Hamissa Mobetto "Ebu Kuwa Basi Kizee Mwenzangu "

Mange Kimambi Amchamba Ray C Kisa Hamissa Mobetto "Ebu  Kuwa Basi Kizee Mwenzangu "
Mwanadada mwanaharakati Mange kimambi ameamua kuununua ugomvi wa Ray C na Mwanamitindo Hamissa Mobetto na kuamua kumpa makavu Ray C na Kumtaka aache kumuandama mwenzake.

Kupitia akaunti yake ya Instagram mange ameandika waraka mrefu kwa kumtia moyo Hamissa kutokana na watu wanaotaka kumshusha katika mapambano yake ya maendeleo.

"Usikose kusikiliza nyimbo ya Madam Hero by @hamisamobetto, link ipo kwenye bio yake.Endelea kupambana mama, naamini ukifika umri kama wetu sisi vizee utakuwa na mafanikio makubwa sana....Sijui watu huwa wanawaza nini kufananisha mafanikio ya mtoto wa miaka 23 na mtu mzima wa miaka zaidi ya 40. Watanzania bwana. Sio sawa inabidi mumfananishe na watu wa umri wake sio mumfananishe na sisi vizee.
.
.
@hamisamobetto usivunjike moyo you are doing great, ni watu wangapi wameweza kufanya unayoyafanya kwa umri wako? Hao wanaokudharau na kukuita maskini walipokuwa na umri kama wako hawakuwa hata na robo ya ulichonacho wewe. Take your time, you will get there......


Hata nyumbu aliekuwa ana throw shade kwako juzi eti unajisikitisha kwa watu pia umempita maendeleo Yani umemwacha mbaliiiiiiiiiii angalau wewe una biashara inayoeleweka yeye biashara yake ni kutafuta drama 😏. Wasikuumize kichwa hao we piga kazi. Eti unajisikitisha kwa watu kasahau yeye alivyokuwa anajliza kutwa sijui anaona bora afe, sijui kachoka kuishi kutwa alikuwa anajiliza humu watu tunampa moyo asigive up alafu leo anajifanya kusema mtu asijisikitishe kwa watu.
.
.
@hamisamobetto Usione sikutetei siku hizi ukadhani vipi hapana ni vile Magu anani keep busy. Kuna mambo ya maana zaidi, itabidi upambane tu 🤣🤣🤣. Natamanigi niwachambe ila ndo hivyo nikipata muda huwa naona ni bora nimchambe Magu. @rayctanzania embu kuwa basi na wewe kizee mwenzangu kha! Alafu nakupenda ujue ila unaudhi unavyomnyanyasa huyu mtoto 😏. Mtoto wa watu anatafuta rizki tu why umzibie? Anapambana na chochote ili mradi afanikiwe kama huwezi kumsapoti si ukae kimya ila why umwaribie rizki yake mtu ambae hana ugomvi na wewe?? Embu acha bwana. Haipendezi''.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...