MWANAMKE mkazi Njage wilayani Kilombero Mkoa wa Morogoro, ameuawa kwa kukatwa kwa shoka kichwani na mumewe kwa kilichoelezwa kuwa ni wivu wa mapenzi.
Kamanda wa Polisi mkoani Morogoro, Willibrod Mutafungwa, alisema hayo jana na kufafanua kuwa tukio hilo lilitokea Julai 28 majira ya asubuhi ambapo mwanamke huyo, Rose Mngwe (43), aliuawa na mumewe, Jacob Kambo (45), mkazi wa Kijiji cha Njage.
Kwa mujibu wa Kamanda Mutafungwa, mwanaume huyo baada ya kumuua mkewe kwa kumkata kwa shoka kichwani, alikimbilia porini na kujinyonga kwenye mti kwa kutumia kamba.
Kamanda Mutafungwa alisema inadaiwa kuwa mwanaume huyo aliamua kufanya kitendo hicho baada ya kuona mkewe amempuuza alipomwambia kuwaondoa watoto wake wa kike aliowazaa nje ya ndoa.
Kamanda alifafanua kuwa alitaka waende kwa waliomzalisha watoto hao kwa madai kuwa wanawanyima nafasi wakiwa hapo.
Alisema miili ya marehemu hao imeshakabidhiwa kwa ndugu zao kwa ajili ya kuendelea na shughuli za mazishi.
Katika tukio lingine, Leo Charles Mashaka (61), mkazi wa Kitongoji cha Igagafu wilayani Kilosa, ameuawa kwa kupigwa na kitu chenye butu kichwani na usoni na mtoto wake wa kumzaa, Emmanuel Leo Charles, sababu ikitajwa ni kudai urithi.
Kamanda Mutafungwa alisema tukio hilo lilitokea Julai 30, alfajiri katika Kata ya Lumuma Tarafa ya Idete ambapo Mashaka alimpigwa na kitu chenye butu kichwani na usoni upande wa kulia na kumsababishia jeraha na michubuko mgongoni, Alisema tukio hilo lilisababishwa na mgogoro katika familia kuhusu urithi.
Kamanda huyo alisema mtuhumiwa alikamatwa na atafikishwa mahakamani baada ya uchunguzi kukamilika.
-
Baadhi ya raia walioyatoroka makaazi yao baada ya mlipuko wa volkano uliotokea usiku wa kuamkia huko mjini Goma mashariki mwa Jamhuri ya Kid...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Tanzania November 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na za ny...
-
Zaidi ya ghorofa 100 jijini Dar es Salaam zilibainika kujengwa kinyume cha taratibu za ujenzi, Bunge lilielezwa. Kwa mujibu wa ripoti iliy...
-
Mhamasishaji maarufu wa mitandaoni, Mwijaku, ameandika ujumbe unaotoa ushauri kwa Rais wa klabu ya Yanga, Injinia Said Hersi, kupitia ukuras...
-
Hii hapa ngoma mpya ya Msanii wa Nyimbo za asili Mama Ushauri ameshirikiana na Ng'wana Ng'washi inaitwa Merimela ,imetengenezwa Lw...
-
Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala ndogo ya Dar es Salaam, imetupilia mbali shauri lililokuwa limefunguliwa na Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina...
-
Msanii maarufu Ntemi O Mabala ' Ng'wana Kang'wa kutoka Kahama Mkoani Shinyanga anakualika kusikiliza wimbo wake mpya unaitwa M...
-
WATU saba wamefariki dunia baada ya bajaji waliyokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na lori eneo la Mpemba, Tunduma wilayani Momba, mk...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 9, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na ...