Thursday, September 12, 2024

Watu 800 Wavamia Kituo Cha Polisi Geita, Wawili Wauawa Kisa Kuhusu Watekaji wa Watoto




Jeshi la Polisi Tanzania limethibitisha kuuawa kwa Watu wawili Mkoani Geita baada ya vurugu zilizoibuka na kupelekea Watu 800 kuvamia kituo cha Polisi wakiwatuhuhumu Watu wawili walioonekana wakiwa wamebeba Watoto wawili na Wananchi waliokuwa katika mnada wa Lulembela kuwahisi kuwa ni wezi wa Watoto na kuanza kuwashambulia.

Taarifa iliyotolewa leo September 11,2024 na Msemaji wa Jeshi la Polisi, David Misime imesema "Chanzo cha tukio hilo ni baada ya Watu wawili kuonekana wakiwa wamebeba Watoto wawili na Wananchi waliokuwa katika mnada wa Lulembela kuwahisi kuwa ni Wezi wa Watoto na kuanza kuwashambuilia, akatokea Mtendaji wa Kata akawabeba kwenye pikipiki na kuwakimbiza Kituo cha Polisi Lulembela"

"Wananchi wanaokadiriwa kufikia 800 walifika kituoni hicho na kuwataka Askari wawakabidhi Watuhumiwa ili wawaue"
"Wananchi hao walianza kushambulia Kituo cha Polisi kwa mawe wakilazimisha kuwachukua Watu hao kwa nguvu ili wawaue, mbali na kushambulia kituo hicho kwa mawe na kutaka kuingia kwa nguvu ndani ya kituo hicho, Wananchi hao walichoma moto gari moja lilioegeshwa nje ya kituo hicho.

"Baada ya Askari kuona hali hiyo ya kuhatarisha maisha ya Watu na mali za Serikali walitumia mabomu ya machozi ili kuwatawanya na iliposhindikana walitumia silaha za moto kwa kupiga risasi juu ili Watu hao watawanyike, katika vurugu hizo Watu wawili wamepoteza maisha, mmoja ni Mwanaume anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 18 hadi 20 na wa pili ni Msichana aitwaye Teresia John mwenye umi wa miaka 18, Mwanafunzi wa kidato cha nne Shule ya Sekondari Lulembela ambaye nyumba yao inatazamana na kituo hicho cha Polisi, hata hivyo, ilibainika Watu waliokuwa wamebeba Watoto hao ni Emanuel John (33) Mkazi wa Kigamboni Lulembela ambaye alikuwa amembeba Mtoto wake aitwaye Ikram Emanuel na wa pili anaitwa Ng'amba Leonard (24) ambaye alikuwa amembeba Mtoto aitwaye John Emanuel, Mama wa Watoto hao aitwaye Rachel Masunga Luhende (22) Mkazi wa Kigamboni Lulembela amethibitisha kuwa Watoto hao ni wa kwake"

Wednesday, September 11, 2024

Oscar Oscar Amchana Mzize :Mchezaji wa Kawaida Sana Hajawai Ibabe Timu

Oscar Oscar Amchana Mzize :Mchezaji wa Kawaida Sana Hajawai Ibabe Timu


KUHUSU ubora wa mshambuliaji wa Yanga na timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Clement Mzize umekuwa na dosari kwa upande wa mchambuzi wa michezo Oscar Oscar ambaye alisema kwamba, mchezaji huyo licha ya kufunga mabao lakini hajawahi kufunga mabao ya kuibeba timu.


"Huu ni msimu wa tatu tunamshuhudia Mzize. Ni mchezaji mzuri sana, lakini hajawahi kufunga hata mabao 10 ya ligi. Hajawahi kufunga mabao ya kuibeba timu kwenye mazingira magumu na hana mabao mengi yanayokumbukwa na wengi.


"Natamani tungeacha mchezo wa kuongeza sifuri. Natamani tungeacha mchezo wa Waingereza. Mzize bado ni mchezaji ambaye kwenye nafasi tano anaweza kufunga bao moja. Bado anakua."


"Kuna watu wameanza kumpa jina na la Didier Drogba. Ni vizuri mtu kuwa na ndoto kubwa, lakini ni vizuri zaidi kuwa na ndoto zenye uhalisia. Tuna kijana anaitwa Kelvin John. Ni Mtanzania mwenzetu. Ni kijana wetu na anacheza Ligi Kuu Denmark. Wakati anaanza kuchipukia alipewa jina la Mbappe. Hadi leo hakuna mfanano wowote." Oscar Oscar

Tuesday, September 10, 2024

Mbozi wajipanga kukomesha ukatili kwa watoto


Na Baraka Messa, Mbozi

KUTOKANA na vitendo vya ukatili kukithir katika wilaya ya Mbozi mkoani Songwe Baraza la Madiwani Halmashauri hiyo limejipanga kupambana na janga hilo la ukatili  vikiwemo vitendo vya ulawiti na ubakaji kwa watoto wadogo chini ya miaka nane.

Hayo yamebainishwa na katibu tawala wa Wilaya hiyo Mbwana Kambangwa akiongea na Habari Leo baada  kikao cha baraza kamili la Madiwani kwa robo muhura mwaka 2023/2024 kilichofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri hiyo ambapo amewataka madiwani kuongeza nguvu kwenye mapambano dhidi ya vitendo vyote vya ukatili wa kijinsia katika maeneo yao.

"Matukio mengi ya ukatili kwa watoto wadogo yamekuwa yakiripotiwa na kuibuliwa na vyombo vya Habari mara kwa mara katika wilaya yetu ya Mbozi,  hali hii imekuwa tishio kwa ustawi wa kizazi kijacho"

Amewataka madiwani ambao ni wawakilishi wa wananchi kujikita katika utoaji elimu mara kwa mara kuhusu madhara ya ukatili kwa watoto wadogo, ikiwa ni pamoja na kuwa karibu na watoto ili kubaini changamoto zinazowakabili ili wasaidiwe.

Kambangwa amesema pia wamepokea maelekezo kutoka Kwa Waziri Mkuu  walipofanya kikao kupitia Mtandao ambapo kunamaagizo maalumu 13 walipewa ikiwemo la kupambana na ukatili wa Kijinsia huku akisema kuwa Mbozi ni  miongoni  mwa Wilaya zilizo kithiri kuwa na vitendo vya Ukatili wa kijinsia.

Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo  George Msyani  amesema Halmashauri inaendelea kupambana dhidi ya matendo ya kikatili huku mipango  ikiwa juu ya kuendelea kutoa elimu  Kwa jamii juu ya matendo ya Ukatili na kueleza athari zake.

" Tumepeana maagizo madiwani wote , suala la elimu ya ukatili katika kata zetu liwe ni ajenda ya kudumu, Kila diwani anapofanya mikutano atoe elimu kuhusu madhara ya ukatili kwa watoto wadogo tukishirikiane na watalaam wa ustawi wa jamii, maendeleo ya jamii pamoja na jeshi la polisi" alisema Msyani.

Kwa upande wake Neema Kibona  alisema matendo ya Ukatili hasa Kwa Watoto wadogo yanazidi kushamili kutokana na uwepo wa kufichiana maovu kwa wanajamii hasa kwa kutaka kumaliza mambo kienyeji bila kufuata Sheria  hali ambayo inaendelea kuwa changamoto kubwa.

Afisa elimu shule za msingi na awali wilaya ya Mbozi Dorothy Mwandila anasema ubize wa wazazi katika shughuli za kiuchumi kumekuwa na athari kubwa katika malezi ya watoto, kwani watoto wengi hulazimika kulelewa na watu wengine ambao sio wazazi na kupata madhara.

"Watoto wetu tuwalee wenyewe, tuache kuwategemea  ndugu wengine na majirani kutulelea watoto wetu, kwa sababu matukio yaliyo mengi ya ulawiti na ubakaji kwa watoto chini ya miaka nane hufanywa na ndugu wa karibu,

Kuna madhara makubwa ya kutokuwa karibu na watoto, kuna kisa kimoja watoto wa mama mmoja baba mmoja kaka yao alikuwa anawaingilia kinyume na maumbile wadogo zake wawili chini ya miaka 10 bila wazazi wao kujua kutokana na ubize wa kuondoka asubuhi na kurudi usiku nyumbani" alisema Mwandila.

Program Jumuishi ya Taifa ya Malezi Makuzi na Maendeleo ya awali ya Mtoto iliyozinduliwa mwaka 2021, inayotekelezwa kwa miaka mitano yaani  (2021/2022-2025/2026 inasisitiza wazazi ,walezi na jamii kuhakikisha wanawekeza kwa watoto kuanzia miaka 0-mpaka miaka 8 katika afua muhimu za lishe, afya , elimu, ulinzi na usalama pamoja na uchangamshi wa awali ili kufikia kikamilifu hatua za ukuaji.

MATOKEO ya Tanzania Vs Guinea Leo Tarehe 10 September 2024

 

MATOKEO ya Tanzania Vs  Guinea Leo Tarehe 10 September 2024

MATOKEO ya Tanzania Vs  Guinea Leo Tarehe 10 September 2024

Guinea inacheza na Tanzania katika Raundi ya Awali ya Kombe la Mataifa ya Afrika mnamo Septemba 10. Mechi hiyo itaanza saa 19:00 kwa saa za kwenu.

Timu ya taifa ya kandanda ya Guinea na timu ya taifa ya kandanda ya Tanzania zinakutana tena miaka 4 baada ya mchezo wa Hatua ya Makundi uliomalizika kwa sare ya 2-2. Timu ya taifa ya kandanda ya Guinea iko katika hali mbaya inapokaribia mpambano huu baada ya kushindwa kutoka kwa DR Congo na Msumbiji. Kocha na wachezaji huenda wakaweka juhudi za ziada kwenye safu ya ulinzi kwani wamekuwa wakiruhusu mabao kwa mechi 4 mfululizo sasa.

Timu ya taifa ya soka ya Tanzania inashuka dimbani baada ya kucheza sare ya bila kufungana dhidi ya Etheopia Jumatano iliyopita na kuendeleza mfululizo wa kutopoteza hadi mechi 5. Inaonekana hawapaswi kuwa na matatizo mengi katika kujilinda kuwa na laha 5 mfululizo safi.

Udaku Special inaangazia Guinea dhidi ya Tanzania kwa wakati halisi, ikitoa mtiririko wa moja kwa moja na matokeo ya moja kwa moja ya mechi, orodha ya timu, takwimu kamili za mechi, maoni ya mechi ya moja kwa moja na muhtasari wa video rasmi. Tunashughulikia mechi zote za awamu ya Awali ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wakati halisi na kutoa utiririshaji wa moja kwa moja inapowezekana.

MATOKEO TAIFA STARS Vs GUINEA

19:00 : TANZANIA 0: 0 GUINEA



Source

WANANCHI TUMULI NA IGUGUNO WAHAMASISHWA KUSHIRIKI UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA

 Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama Bi. Asia Messos amewataka wakazi wa kata za Tumuli na Iguguno wilayani hapa kujitokeza kwa wingi kushiriki Uchaguzi wa Serikali Za Mitaa utakaoufanyika Novemba 27,2024

Wito huo ameutoa Septemba 9,2024 wakati wa ziara ya kikazi ya kata kwa kata yenye lengo la kusikiliza na kutatua kero mbalimbali zinazowakabili wakazi wa kata hizo.

"Tujitokeze kwa wingi kuwania nafasi za Uongozi lakini pia tujitokeze kwa wingi kwenye mikutano ya siasa ili tuweze kusikiliza sera za viongozi wetu tunaotaka kuwachagua, na itakapofika Novemba 27, 2024 ukapige kura kumchagua kiongozi unayemtaka." DED Asia Messos

Vile vile amesisitiza juu ya kuchagua viongozi makini wazalendo wenye kiu ya kuleta maendeleo kwa wananchi na si wabinafsi, "Lakini tunapoenda kuchagua viongozi wetu, tusichague ili mradi tumechagua, chagueni viongzi wenye shahuku ya kuleta maendeleo" DED Asia Messos

Akizungumzia kuhusu zoezi la kuandikisha wapiga kura, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Bi. Asia Messos amesema mchakato wa kuandika wapiga Kura kwenye Daftari la Orodha ya Wapiga Kura utaanza Oktoba 11-21,2024 na kuwataka wananchi wajitokeze kujiandikisha katika daftari hilo.

"Ili uweze kupiga kura unapaswa uwe umejiandikisha kwenye Daftari la Orodha ya Wapiga Kura, mchakato huu utaanza Tarehe 11-20, Oktoba 2024, itakapofika hii tarehe twendeni kwa pamoja tukajiandikishe tupate nafasi ya kuchagua viongozi wetu tunaowataka" Bi. Asia Messos

Aidha Bi. Asia Messos amewakumbusha wakazi wa kata hizo juu ya umuhimu wa kulinda miundombinu ya serikali, kupambana na vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa kutoa taarifa kwenye mamlaka husika, kuhakikisha wanashiriki katika shughuli za maendeleo pamoja na kuchangia chakula shuleni.

Edo Kumwembe 'Huu Ndio Unafiki wa Watanzania Kwa Bwana Samatta'




Haijamchukua Samatta hadi astaafu ndipo aheshimike. Juzi juzi tu tumecheza na Ethiopia na tayari umma wa Watanzania umemkumbuka. Mechi mbovu ya kawaida huku wachezaji wengi wa eneo la mbele wakishindwa kuonyesha makali yao, tayari Watanzania wamemkumbuka Samatta.
.
Huu ndio unafiki wa Watanzania katika ubora wake. Ukweli ni kwamba Samatta bado hayupo katika ubora wake lakini bado ana nafasi ya kuonyesha uzoefu wake uwanjani. Kama sio kwa mechi nzima basi ni kwa dakika kadhaa.

Kuwepo kwake uwanjani tu kunawafanya baadhi ya wachezaji wa timu pinzani kuwa na hofu naye. Hapo ndipo kina Simon Msuva wanafunga mabao na bado tunatoa kejeli kwa Samatta hajitumi uwanjani isipokuwa Msuva ndiye anayejituma zaidi.
.
Hata mwamuzi akimwona Samatta anaweka heshima zaidi kwake kwa sababu anajua wasifu wake. Ni kitu cha kawaida ndiyo maana imeletwa staili ya kumpa unahodha mchezaji ambaye ni staa zaidi katika taifa. Messi kwa Argentina, Ronaldo kwa Ureno, Neymar kwa Brazil, Mbappe kwa Ufaransa. Mifano ni mingi.

— Edo Kumwembe, Legend.

Source

Sunday, September 8, 2024

Polisi Wafunguka Kuhusu Aliyetekwa Tegeta na Kukutwa Ameuawa Ununio....




Jeshi la Polisi limesema linaendelea na uchunguzi wa tukio la kusikitisha la mauaji ya Kiongozi wa CHADEMA, Ali Kibao na timu ya uchunguzi wa matukio makubwa toka Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai toka Makao Makuu imetumwa kuongeza nguvu kwenye timu ya awali ili kuhakikisha waliofanya mauaji haya wanakamatwa na kufikishwa Mahakamani.

Taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Jeshi la Polisi, David Misime leo September 08,2024 imesema "Jeshi la Polisi linatoa wito kwa yeyote mwenye taarifa za kweli na za uhakika aziwasilishe kwa mujibu wa taratibu ili kusaidia kufanikisha kukamilika mapema kwa uchunguzi wa tukio hili la kusikitisha"

"Jana Septemba 7,2024 Jeshi la Polisi lilitoa taarifa juu ya Ally Mohamed Kibao kushushwa kutoka kwenye basi la Tashrif na kuchukuliwa na Watu ambao hawakuweza kutambulia na kwamba uchunguzi ulianza baada ya kupokelewa taarifa hiyo"

"Baada ya kutolewa taarifa za kuonekana mwili wa Mtu mwanaume ambaye hakuweza kutambulia kwa wakati huo ni mwili wa nani huko Ununio Jijini Dar es Salaam, utambulizi umefanyika kwa mujibu wa taratibu na kubainika ni mwili wa Ally Mohamed Kibao, aidha uchunguzi wa mwili wa marehemu (postmortem) umefanywa leo tarehe 08/09/2024 na Madaktari bingwa kwa kushirikisha Familia"

SIMANZI: Kibao Akutwa Amefariki Ununio Baada ya Kutekwa Maeneo ya Tegeta

 

SIMANZI: Kibao Akutwa Amefariki Ununio Baada ya Kutekwa Maeneo ya Tegeta

Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe, Viongozi na Wafuasi wengine wa Chama hicho pamoja na Wananchi wengine wamefika Hospitali ya Mkoa wa Kinondoni, Mwananyamala leo September 08,2024 kufuatia mwili wa aliyekuwa Mjumbe wa Sekretarieti ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)Taifa na Msaidizi wa Katibu Mkuu, Ali Mohamed Kibao ambaye aliliripotiwa kutekwa juzi , kukutwa Hospitalini katika chumba cha kuhifadhia maiti ukiwa umeharibika.


Taarifa iliyotolewa leo Sept 8, 2024 kupitia ukurasa wa mtandao wa X(zamani Twitter) na Meya wa zamani wa Ubungo, Boniface Jacob imesema "Mwili wa Kibano ulikutwa umetupwa jana alfajiri maeneo ya UNUNIO (jirani na viwanja vya NSSF) ukiwa na majereha makubwa sehemu za usoni kiasi Ndugu zake walipata tabu kuutambua kirahisi, kwa mujibu wa Wenyeji wa Ununio ambao ni walima mchicha, wanasema jana asubuhi walitoa taarifa kwa Jeshi la Polisi baada ya kuona mwili wa Mtu mzima, mweupe mwenye asili ya kiarabu ambaye baadaye Jana jioni ndugu waliutambua kuwa ni mwili Ali Mohammed Kibao ukiwa na majeraha"


Itakumbukwa jana September 7, 2024 Katibu Mkuu wa CHADEMA John Mnyika aliongea na Waandishi wa Habari na kusema Kibano alikamatwa na Watu wanaodhaniwa kuwa ni Askari Polisi eneo la Tegeta baada ya gari mbili za Jeshi la Polisi kuzuia basi la Tashrif lenye namba T 343 EES alilokuwa amepanda kutoka Dar kwenda Tanga kisha Watu wenye silaha ikiwemo bunduki wakaondoka nae ambapo baadaye Polisi kupitia kwa Msemaji wake David Misime walisema wameiona taarifa hiyo na wameanza uchunguzi.


Kabla ya umauti wake Ali Kibao aliwahi kuwa Afisa wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) akastaafu na kujiunga na CCM, baadaye akachaguliwa kuwa Katibu Mwenezi wa CCM Mkoa wa Tanga wakati wa Rais Mstaafu Kikwete na baadaye alijiunga CHADEMA.

Babati mji waahidi kuifanyia kazi ripoti ya Marafiki wa Elimu kuhusu Elimu jumuishi.



Na John Walter -Babati
Marafiki wa Elimu katika mji wa Babati mkoani Manyara chini ya Shirika la Haki Elimu wameiomba serikali waendelee kuweka Mazingira wezeshi kwa Wanafunzi wenye mahitaji maalum katika shule za Sekondari na msingi ili wapate haki ya huduma kama wengine.

Wakizungumza wakati wakitoa taarifa ya ufuatiliajii Maendeleo ya elimu katika mji wa Babati, Mratibu wa Marafiki wa Elimu Gaudensia John Igoshashalismo amesema shule 20 walizozitembelea wamegundua elimu jumuishi bado haizingatiwi licha ya Serikali kujitahidi kuweka Miundombinu rafiki kwa wenye mahitaji maalum.

Matokeo ya ufuatiliajii yanaonesha shule 20 zilizotembelewa zina jumla ya walimu 484, Wanawake 297 na wanaume 187 ambapo kati yao ni walimu 12 tu sawa na asilimia 2.5, walimu 12 ndio wenye taaluma ya Elimu maalum huku walimu 185 ambao ni sawa na asilimia 39 ndio wenye uwezo wa kufundisha madaraja jumuishi.

Nao Wadau wa Elimu wamesema wapo tayari sasa kuhakikisha Elimu jumuishi inazingatiwa katika maeneo yao.


Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya mji wa Babati Shabani Mpendu na Mwenyekiti wa Halmashauri ya mji wa Babati Abdulrahman Kololi, wameahidi kuzitafutia ufumbuzi changamoto zilizobainishwa katika ripoti ya Marafiki wa Elimu na kupongeza jitihada wanazofanya.

Afisa program idara ya ushiriki na uwajibikaji jamii Haki Elimu Naomi mwakilembe amesema wataendelea kuwasapoti Marafiki wa Elimu katika kuhakikisha Elimu jumuishi inazingatiwa.



Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...