Na John Walter -Babati
Marafiki wa Elimu katika mji wa Babati mkoani Manyara chini ya Shirika la Haki Elimu wameiomba serikali waendelee kuweka Mazingira wezeshi kwa Wanafunzi wenye mahitaji maalum katika shule za Sekondari na msingi ili wapate haki ya huduma kama wengine.
Wakizungumza wakati wakitoa taarifa ya ufuatiliajii Maendeleo ya elimu katika mji wa Babati, Mratibu wa Marafiki wa Elimu Gaudensia John Igoshashalismo amesema shule 20 walizozitembelea wamegundua elimu jumuishi bado haizingatiwi licha ya Serikali kujitahidi kuweka Miundombinu rafiki kwa wenye mahitaji maalum.
Matokeo ya ufuatiliajii yanaonesha shule 20 zilizotembelewa zina jumla ya walimu 484, Wanawake 297 na wanaume 187 ambapo kati yao ni walimu 12 tu sawa na asilimia 2.5, walimu 12 ndio wenye taaluma ya Elimu maalum huku walimu 185 ambao ni sawa na asilimia 39 ndio wenye uwezo wa kufundisha madaraja jumuishi.
Nao Wadau wa Elimu wamesema wapo tayari sasa kuhakikisha Elimu jumuishi inazingatiwa katika maeneo yao.
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya mji wa Babati Shabani Mpendu na Mwenyekiti wa Halmashauri ya mji wa Babati Abdulrahman Kololi, wameahidi kuzitafutia ufumbuzi changamoto zilizobainishwa katika ripoti ya Marafiki wa Elimu na kupongeza jitihada wanazofanya.
Afisa program idara ya ushiriki na uwajibikaji jamii Haki Elimu Naomi mwakilembe amesema wataendelea kuwasapoti Marafiki wa Elimu katika kuhakikisha Elimu jumuishi inazingatiwa.