Thursday, September 12, 2024

Watu 800 Wavamia Kituo Cha Polisi Geita, Wawili Wauawa Kisa Kuhusu Watekaji wa Watoto




Jeshi la Polisi Tanzania limethibitisha kuuawa kwa Watu wawili Mkoani Geita baada ya vurugu zilizoibuka na kupelekea Watu 800 kuvamia kituo cha Polisi wakiwatuhuhumu Watu wawili walioonekana wakiwa wamebeba Watoto wawili na Wananchi waliokuwa katika mnada wa Lulembela kuwahisi kuwa ni wezi wa Watoto na kuanza kuwashambulia.

Taarifa iliyotolewa leo September 11,2024 na Msemaji wa Jeshi la Polisi, David Misime imesema "Chanzo cha tukio hilo ni baada ya Watu wawili kuonekana wakiwa wamebeba Watoto wawili na Wananchi waliokuwa katika mnada wa Lulembela kuwahisi kuwa ni Wezi wa Watoto na kuanza kuwashambuilia, akatokea Mtendaji wa Kata akawabeba kwenye pikipiki na kuwakimbiza Kituo cha Polisi Lulembela"

"Wananchi wanaokadiriwa kufikia 800 walifika kituoni hicho na kuwataka Askari wawakabidhi Watuhumiwa ili wawaue"
"Wananchi hao walianza kushambulia Kituo cha Polisi kwa mawe wakilazimisha kuwachukua Watu hao kwa nguvu ili wawaue, mbali na kushambulia kituo hicho kwa mawe na kutaka kuingia kwa nguvu ndani ya kituo hicho, Wananchi hao walichoma moto gari moja lilioegeshwa nje ya kituo hicho.

"Baada ya Askari kuona hali hiyo ya kuhatarisha maisha ya Watu na mali za Serikali walitumia mabomu ya machozi ili kuwatawanya na iliposhindikana walitumia silaha za moto kwa kupiga risasi juu ili Watu hao watawanyike, katika vurugu hizo Watu wawili wamepoteza maisha, mmoja ni Mwanaume anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 18 hadi 20 na wa pili ni Msichana aitwaye Teresia John mwenye umi wa miaka 18, Mwanafunzi wa kidato cha nne Shule ya Sekondari Lulembela ambaye nyumba yao inatazamana na kituo hicho cha Polisi, hata hivyo, ilibainika Watu waliokuwa wamebeba Watoto hao ni Emanuel John (33) Mkazi wa Kigamboni Lulembela ambaye alikuwa amembeba Mtoto wake aitwaye Ikram Emanuel na wa pili anaitwa Ng'amba Leonard (24) ambaye alikuwa amembeba Mtoto aitwaye John Emanuel, Mama wa Watoto hao aitwaye Rachel Masunga Luhende (22) Mkazi wa Kigamboni Lulembela amethibitisha kuwa Watoto hao ni wa kwake"
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...