Saturday, February 8, 2025

CCM RUVUMA WAFANYA MKUTANO MKUBWA KUUNGA MKONO DKT. SAMIA, DKT. MWINYI KUPEWA MITANO TENA!!


Baadhi ya Wanachama wa CCM wakiwa katika matembezi ya kuunga mkono Azimio hilo la kuchaguliwa kuwa wagombea Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Ruvuma.
Mwenyekiti wa Halmashauri kuu ya Mkoa wa Ruvuma Hemed Challe akiongoza matembezi hayo ya kuunga mkono juhudi za kuwapongeza wagombea wa nafasi za Urais kupitia Chama hicho.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Ruvuma Oddo Mwisho akiongoza matembezi ya hiari katika juhudi za kuunga mkono wagombea wa Urais kupitia Chama cha Mapinduzi
Wanachama wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Ruvuma wakiwa kwenye mkutano
Wananchi waliojitokeza kwenye mkutano huo
Na Regina Ndumbaro Ruvuma. 

 Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Ruvuma kimefanya mkutano maalum wa kujadili na kupitisha azimio la kuwaunga mkono viongozi walioteuliwa na chama hicho kugombea nafasi ya urais kwa uchaguzi ujao. 

Mkutano huo, uliofanyika chini ya uongozi wa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Ruvuma, Oddo Mwisho, umeonyesha mshikamano mkubwa wa wanachama wa CCM mkoani humo katika kuimarisha chama kuelekea uchaguzi.


Katika azimio hilo, viongozi walioteuliwa kugombea nafasi ya urais ni Dkt. Ally Hassan Mwinyi kwa upande wa Zanzibar na Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na Mgombea Mwenza Dkt. Emanuel Nchimbi kwa upande wa Tanzania Bara. 

Mwenyekiti Oddo Mwisho amewahimiza wanachama wa CCM mkoani Ruvuma kuwaunga mkono viongozi hao na kushiriki kikamilifu katika kampeni za chama kwa lengo la kuleta ushindi mnono katika uchaguzi huo.

Mbali na kujadili wagombea wa nafasi ya urais, mkutano huo pia ulijikita katika tathmini ya miradi mbalimbali ya maendeleo inayoendelea mkoani Ruvuma chini ya uongozi wa Dkt. Samia Suluhu Hassan. 


Mradi mkubwa wa umeme na maji wenye thamani ya takribani Shilingi bilioni 400 umetajwa kuwa miongoni mwa mafanikio makubwa yanayotekelezwa kwa manufaa ya wananchi wa Ruvuma.

Mwisho amebainisha kuwa mradi wa ujenzi wa barabara za mitaa unaendelea kwa kasi, jambo linalothibitisha dhamira ya CCM ya kuboresha miundombinu kwa ajili ya maendeleo ya wananchi. 

Amesema kuwa hatua hizo ni matokeo ya jitihada za serikali ya CCM chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan, ambaye ameonesha dhamira ya dhati ya kuwaletea wananchi maendeleo endelevu.

Katika mkutano huo, Mwenyekiti huyo wa CCM Mkoa wa Ruvuma amewashukuru viongozi wa chama na serikali waliowezesha kufanikisha maazimio hayo huku akimpongeza Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Kanali Ahmed Abbas, kwa kushiriki katika mkutano huo na kuunga mkono azimio la kuwaimarisha wagombea wa CCM katika uchaguzi ujao.

Pia amewapongeza madiwani na wabunge waCCM kwa mshikamano wao na juhudi zao za kushirikiana na wananchi katika kuimarisha chama na kutekeleza miradi ya maendeleo inayowanufaisha wananchi wa Ruvuma. 

Amesisitiza kuwa mshikamano huo ni nguzo muhimu katika kuhakikisha CCM inaendelea kuwa chama kinacholeta maendeleo ya kweli kwa Watanzania.

Akihitimisha hotuba yake, Mwenyekiti Oddo Mwisho amewataka wanachama wa CCM Mkoa wa Ruvuma kuendelea kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha ushindi wa chama hicho kwenye uchaguzi ujao. 

Amewasihi kushiriki kikamilifu katika kampeni na kuwahamasisha wananchi kuendelea kuiamini CCM kama chama chenye dira na maono ya maendeleo ya taifa.

Aidha wanachama wa CCM wameahidi kuendelea kuiunga mkono serikali ya CCM na viongozi walioteuliwa kupeperusha bendera ya chama hicho katika uchaguzi ujao.

Source

Shule ya Sekondari Manyara Boys inajengwa kwa kasi.


Na John Walter -Babati

Timu ya Menejimenti ya Halmashauri ya Wilaya ya Babati imetembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari ya Manyara Boys, inayojengwa katika Kijiji cha Ngoley, Kata ya Mwada.

Shule hiyo inajengwa na Serikali kupitia mradi wa EP4R (Education Program for Results) na inatarajiwa kugharimu kiasi cha Shilingi bilioni 4.1 hadi kukamilika kwake.

Wakati wa ziara hiyo, timu hiyo ilitoa msisitizo kwa mafundi kuhakikisha wanakamilisha ujenzi kwa wakati na kuzingatia viwango vya ubora vinavyotakiwa.

Aidha, walihimiza kuongeza nguvu ili kuhakikisha mradi huo unakamilika kwa ufanisi na kwa mujibu wa mpango wa serikali wa kuboresha elimu nchini.

Shule ya Sekondari ya Manyara Boys inatarajiwa kuwa miongoni mwa shule muhimu za kanda ya kaskazini, ambapo baada ya kukamilika, itapokea wanafunzi wa kidato cha kwanza hadi kidato cha sita kutoka maeneo mbalimbali ya Tanzania.

Ujenzi wa shule hiyo ni sehemu ya juhudi za serikali za kuongeza fursa za elimu na kuboresha mazingira ya kujifunzia kwa vijana.

Wakazi wa eneo hilo na wadau wa elimu wanatarajia shule hiyo itakuwa na mchango mkubwa katika kuinua kiwango cha elimu katika mkoa wa Manyara na kanda ya kaskazini kwa ujumla.
 

Friday, February 7, 2025

USAWA WA KIJINSIA TANZANIA: KUTOKA MKUTANO WA BEIJING HADI MATOKEO YA LEO


MWANGA katikati ya giza nene uliangazia ulimwengu Mwaka 1995,wakati ambao Mwanamke alionekana kutoweza kufanya jambo lolote bila Mwanaume, Mkutano wa Beijing-China uliibua mwongozo wa kurasa 129 uliobeba ajenda 12 ambazo zilizolenga kumuwezesha mwanamke.

Ajenda hizo zilijikita hasa katika kukabiliana na umaskini, kupata elimu na mafunzo, afya Bora, kukabiliana na mizozo ya kivita, uchumi, Mfumo wa Uongozi na upitishaji maamuzi, mifumo ya kitaasisi, haki za binadamu, vyombo vya habari,na mazingira wezeshi kwa mtoto wa kike.

Ambapo kulingana na maazimio ya Beijing Tanzania imepiga hatua kubwa katika kumuwezesha mwanamke kumiliki mali na rasimali ambapo kwenye ardhi Sheria ya ardhi imeotoa haki sawa kwa raia wote kumiliki ardhi na kwenye umiliki wa mali imekuwa ikitoa mikopo ya asilimia kumi katika halmashauri.

Aidha Mtandao wa jinsia Tanzania (TGNP) umekuwa kituo kikuu nchini ambacho kinasaidia kutoa hamasa na kuwajengea uwezo wanawake Vijana kupata uongozi kwa lengo la kuingiza idari kubwa ya wanawake katika mfumo ya maamuzi.

Aidha ushiriki wa Kisiasa wa kundi la wanawake bado ni hafifu ambapo kupitia takwimu zilizotewa na Mtandao wa jinsia nchini imeonesha kuwa bado hali sio nzuri kwani ni wanawake asilimia 2.1 pekee ndio walishiriki katika kuwania nafasi za kugombea uongozi wa serikali za mitaa na vijiji ambapo juhudi kubwa zinatakiwa kuwekwa ili kuundwe sera ambayo itajumuisha mwanamke katika kila nafasi za Maamuzi.

Mkutano wa Beijing umechagiza ushawishi mkubwa katika nchi mbalimbali ulimwenguni ambapo kupitia ajenda zake zilizo jikita katika usawa wa kijinsia zimeibua makongamano ambayo yalileta mipango ya Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs).


Aidha matunda yatokanayo na mkutano wa Beijing yameimarisha huduma Bora ya afya kwa mama na mtoto pamoja na Elimu kwa watoto wa kike ambapo serikali ya awamu ya sita imejitolea kutoa Elimu bure kuanzia shule ya msingi hadi kidato Cha sita.


Azimio la Beijing limeibua mapambano mengi ambapo vitendo vya ukatili hasa ubakaji vilivyokuwa vikishamiri vimepungia kwa asilimia kubwa kutokana na juhudi zilizofanyika kwa ajili ya kumlinda mtoto wa kike kuthaminika katika jamii.


Vilevile,kufikia usawa wa kijinsia ni muhimu kwa maendeleo endelevu katika jamii zote,kwani majukumu ya wanawake na wanaume yanajengwa kijamii, lakini mara nyingi tofauti za kijinsia zilizopo huwakosesha wanawake faida hii inazuia maendeleo yao kama binadamu wengine.


Licha ya miongo kadhaa ya juhudi za maendeleo ya jumla katika kuboresha maisha ya wanawake kumekuwa na hali isiyoridhisha kwa baadhi ya maeneo hasa katika uwakilishi wa wanawake Viongozi katika ngazi za Maamuzi.


Katika ukanda wa Afrika Mashariki, Tanzania ni mojawapo ya nchi zinazofanya vizuri katika ushiriki wa wanawake katika uongozi kulingana na takwimu za Interparliamentary Union (IPU) hadi Januari 2019, Tanzania inashika nafasi ya pili kwa nchi za Afrika Mashariki na nafasi ya 25 duniani kwa kuwa na asilimia 36.9 ya wanawake Wabunge.


Bado nchi haijaweza kufikia lengo la 50/50 na hivyo, hatuna budi kuongeza juhudi katika kuongeza nafasi za wanawake katika ngazi mbalimbali za maamuzi ili kufikia lengo hilo

10 bora ya Vyuo Vikuu Afrika Mashariki kwa mwaka 2025



Elimu ya juu barani Afrika inazidi kuimarika, na vyuo vikuu vya Afrika Mashariki vinachangia pakubwa katika hili. Kulingana na orodha iliyotolewa na UniRank, hapa ni vyuo vikuu 10 bora Afrika Mashariki kwa mwaka 2025, kulingana na sifa zao za kimataifa.

1. Chuo Kikuu cha Nairobi (Kenya)



Chuo hiki kinashika nafasi ya 7 barani Afrika. Kimejijengea umaarufu kutokana na ubora wake katika sayansi, uhandisi, na biashara. UON ni chuo kikuu kinachotoa elimu bora na kina miundombinu ya kisasa.

2. Chuo Kikuu cha Makerere (Uganda)



Kikiwa na nafasi ya 16 Afrika, Makerere ni moja ya vyuo vikuu vya zamani na vinavyoheshimika zaidi katika Afrika Mashariki. Chuo hiki kinajivunia programu bora katika sayansi za jamii na biashara.

3. Chuo Kikuu cha Kenyatta (Kenya)



Kimeshika nafasi ya 28 Afrika. Chuo hiki kinatoa elimu ya kiwango cha juu, haswa katika fani za elimu, sanaa, na biashara, kikiwapa wanafunzi wake uwezo wa kuongoza katika sekta mbalimbali.

4. Chuo Kikuu cha Strathmore (Kenya)



Kikiwa na nafasi ya 31 Afrika, Strathmore ni chuo cha kibinafsi kinachojulikana kwa ubora wa elimu katika nyanja za biashara, sheria, na teknolojia.

5. Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Tanzania)



Nafasi ya 37 Afrika inajivunia chuo hiki ambacho ni kiongozi katika elimu ya juu nchini Tanzania, hasa katika sayansi za kijamii na sheria.

6. Chuo Kikuu cha Mount Kenya (Kenya)



Kilicho na nafasi ya 54 Afrika, Chuo Kikuu cha Mount Kenya kinatoa programu mbalimbali zinazozingatia mahitaji ya soko la ajira.

7. Chuo Kikuu cha Jomo Kenyatta cha Kilimo na Teknolojia (Kenya)


Chuo hiki kimeshika nafasi ya 57 Afrika na kinajivunia kuwa na programu bora katika uhandisi, kilimo, na teknolojia.

8. Chuo Kikuu cha Rwanda (Rwanda)


Nafasi ya 62 Afrika, Chuo Kikuu cha Rwanda ni miongoni mwa vyuo vikuu bora katika ukanda wa Afrika Mashariki, kikiwa na umakini katika elimu ya sayansi na biashara.

9. Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Marekani Afrika (Kenya)


Chuo hiki, kinachoshika nafasi ya 66 Afrika, kinatoa elimu inayozingatia ubora wa kimataifa, hasa katika programu za biashara na sheria.

10. Chuo Kikuu cha Egerton (Kenya)


Kilichoshika nafasi ya 71 Afrika, Egerton ni maarufu kwa kutoa elimu bora katika kilimo na sayansi za mazingira.

WATAALAMU WA TAKWIMU WATAKIWA KUTEKELEZA MAJUKUMU YAO KWA UFASAHA KATIKA KUPAMBANA NA UMASKINI


Wataalamu wa takwimu wametakiwa kuendelea kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi na ufasaha kwa kuwa uwepo wa takwimu sahihi ni muhimu katika kutatua matatizo yanayolikabili taifa.

Wito huo umetolewa na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Mhe. Stanslaus Nyongo (Mb), leo tarehe 7 Julai, 2025, wakati akifungua kikao kazi cha wataalamu wa Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi Tanzania kwa mwaka 2024-2025 jijini Dodoma.

Mhe. Nyongo alieleza kuwa maamuzi makubwa ya kisera yanahitaji taarifa sahihi, na takwimu zitakazopatikana kupitia utafiti huo zitasaidia katika kutafuta njia bora ya kupunguza umaskini katika nchi.

Aidha, Mhe. Nyongo alieleza kuwa, kwa mujibu wa takwimu zilizopo sasa, watanzania wengi wanaishi kwa chini ya dola moja ya Kimarekani (1.9). Katika malengo ya Dira ya Taifa ya 2050, Serikali inalenga kuongeza kipato cha mwananchi hadi kufikia Tsh. 4,000 hadi 8,000.

Alisema kuwa hayo ndio matamanio ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, na kwamba jukumu la kuandaa mipango itakayowezesha kipato cha Mtanzania kufikia matarajio hayo wamepewa Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji.

Aliongeza kuwa utafiti huu ni muhimu kwani utatoa picha halisi ya hali ya kipato cha kila Mtanzania na kusaidia Serikali kupanga mikakati bora itakayoboresha ustawi wa wananchi. Aidha, aliipongeza Ofisi ya Taifa ya Takwimu kwa mchango wake katika uchambuzi wa takwimu muhimu zinazosaidia maendeleo ya taifa.

Kwa upande wake, Kamisaa wa Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022, Mhe. Anne Makinda, alieleza kuwa jumla ya wadadisi 1,000 wamepatiwa mafunzo kwa ajili ya kufanya utafiti huo.

Mtakwimu Mkuu wa Serikali, Bi. Albina Chuwa, alifafanua kuwa sensa hiyo itasaidia kupima kiwango cha umaskini wa kipato na kutoa mwanga juu ya maeneo yanayohitaji kuboreshwa katika sekta mbalimbali.

Dkt. Chuwa alibainisha kuwa utafiti huu utaenda kufanyika katika mikoa yote ya mijini na vijijini, na aliwahimiza kaya zitakazochaguliwa kutoa ushirikiano wa kutosha kwa wadadisi ili Serikali iweze kupata takwimu zitakazotumika katika juhudi za kupunguza umaskini. 

Akesha makaburini akimngojea mume!


Ukisikia watu wanasema dunia ina mambo, basi jua mambo yenyewe ndio haya. Kutana na mrembo aitwaje Naomi mwenye umri wa miaka 43 ambaye amekuwa akitamani kupata mwanaume wa kumuoa kwa muda mrefu bila mafanikio.  

Anasema hali hiyo ilimfanya kukata tamaa licha ya kuwa tayari kufanya lolote ili tu kuolewa. Jambo la ajabu alilowahi kufanya ni kulala usiku mzima kwenye makaburi akiamini lingeondoa kizuizi kinachomzuia kuolewa.

"Sikuwa na chaguo jingine ila kujaribu zaidi ya kufanya hivyo kwa ajili ya maisha bora. Siku hiyo, nilikutana na shangazi yangu mkubwa ambaye aliniambia kwamba nikilala kwenye makaburi, mambo yangeniendea vizuri na kupata mume ndani ya muda mfupi," alisema.  

Hata hivyo, anasema hakuna kilichotokea hata baada ya kufuata matakwa hayo ya ajabu. Alibaki bila matumaini kwani juhudi zake zote hazikufanikiwa. Lakini hakupoteza tumaini kwamba siku moja angeolewa na kuwa na familia yake. 

Kupitia kwa rafiki yake wa muda mrefu, aliambiwa amjaribu mtaalamu wa mitishamba kwa jina la Dr Bokko na kupewa namba zake ambazo ni +255618536050, aliwasiliana na mtu huyo ambaye kwa muda mrefu alikuwa amesaidia maelfu ya wanawake wenye changamoto kama yake. 

Punde tu alipofika kwa Dr Bokko ili kupata huduma yake, uchawi wa mafanikio ya ndoa ulifanywa kwa maana ya kuvunja laana inayomzuia kuolewa licha ya umri wake kwenda sana. 

Alimhakikishia usiri katika kazi yao na kwamba rekodi zake, faili, wala utambulisho wake hautatolewa kwa  mtu mwingine au kuwekwa hadharani isipokuwa atakapoamua kutoa ushahidi yeye mwenyewe. 

Wiki chache baadaye, alifurahi sana baada ya kumpata mwanaume wa maisha yake. Alisema mwanzoni alikuwa haamini, lakini baada ya kumchunguza mwanaume huyo, aligundua kuwa alikuwa tayari kweli kumuoa na sasa wanaishi kama mume na mke na wana familia.  

Mwisho.


Wananchi wa Ngapapa Gizani kwa miezi miwili


Na John Walter -Kiteto
Wananchi wa Kijiji cha Ngapapa, wilayani Kiteto, bado wanakabiliwa na changamoto ya kukosekana kwa huduma ya umeme kwa zaidi ya miezi miwili, hali inayowaathiri katika shughuli zao za kila siku, zikiwemo biashara, elimu, na huduma za kijamii.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) wilayani Kiteto, tatizo hilo limesababishwa na hitilafu kwenye moja ya transfoma inayohudumia kijiji hicho. TANESCO imesema tayari wameshawasilisha taarifa kwa uongozi wa mkoa kwa hatua zaidi, lakini hadi sasa tatizo bado halijapatiwa suluhisho.

Kutokana na hali hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Kiteto, Remidius Mwema, ametoa maagizo kwa TANESCO kuhakikisha kuwa tatizo hilo linatatuliwa haraka ili kurejesha huduma ya umeme kwa wananchi. Amesisitiza kuwa umeme siyo hisani bali ni haki ya wananchi, kwani serikali tayari imefikisha huduma hiyo katika vijiji vyote nchini.

Wananchi wa Ngapapa wameeleza kusikitishwa na hali hiyo, wakisema kuwa kukosekana kwa umeme kumeathiri biashara zao, hasa wale wanaotegemea vifaa vya umeme kama vile mashine za kusaga nafaka, friji za kuhifadhi bidhaa, na vyanzo vya mwangaza wakati wa usiku. Vilevile, wanafunzi wamelazimika kusoma katika mazingira magumu, huku vituo vya afya vikikumbwa na changamoto ya kuhifadhi dawa zinazohitaji ubaridi.

Wananchi hao wameiomba serikali na TANESCO kuchukua hatua za dharura ili kurejesha huduma hiyo muhimu haraka iwezekanavyo.

Simba Amebanwa Mbavu na Fountain Gate FC


Mnyama amebanwa katika dimba la Tanzanite Kwaraa, Babati kufuatia sare ya 1-1 dhidi ya wenyeji Fountain Gate Fc waliomaliza wakiwa pungufu ya mchezaji mmoja baada ya golikipa John Noble kuoneshwa kadi nyekundu kwa kupoteza muda.

FT: Fountain Gate Fc 1-1 Simba Sc
⚽ 75' Chasambi (og)
⚽ 57' Ateba

Monday, February 3, 2025

Mwenyekiti CCM Manyara atoa onyo kwa wanasiasa.


Na John Walter -Manyara
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Manyara, Mheshimiwa Peter Toima Kiroya, amewaonya wanasiasa wanaotumia majukwaa ya kijamii kusambaza chuki na kutoa taarifa za uongo zinazoweza kuvuruga umoja wa wananchi.

Akizungumza katika hafla ya shukrani kwa Mwenyekiti wa Kijiji cha Loiborsoit A, Lengay Lemonji, Mheshimiwa Toima ambaye alikuwa mgeni rasmi, alisema kuwa muda wa kufanya siasa bado, hivyo kila mmoja anapaswa kutimiza wajibu wake ipasavyo.

Toima alishangazwa na kitendo cha baadhi ya wanasiasa kuhudhuria shughuli hiyo bila hata kualikwa na kuanza kuzungumza mambo ambayo yalikuwa nje ya lengo la sherehe.

"Wenyeviti wa mitaa, vijiji, vitongoji na mitaa wanapaswa kufanya kazi kwa weledi kwa mujibu wa sheria za nchi na Ilani ya CCM, Wanatakiwa kuwatumikia wananchi kwa upendo, kutatua changamoto zao au kuzifikisha sehemu husika badala ya kuendekeza migogoro," alisema Mheshimiwa Toima.

Aliwasihi viongozi na wananchi kumtanguliza Mungu katika kila jambo na kushirikiana kwa ajili ya maendeleo ya jamii.

 Pia alisisitiza kuwa wakati wa uchaguzi utakapowadia, wananchi wamchague kwa kura nyingi Dkt. Samia Suluhu Hassan ili aendelee kuwaletea maendeleo.

Mheshimiwa Toima alionya vikali tabia ya baadhi ya wanasiasa wanaogeuza hafla za kijamii kuwa majukwaa ya kisiasa na kutumia fursa hizo kujipatia umaarufu au kujigamba.

 Alisema hali hiyo huleta taharuki na migongano isiyo ya lazima ndani ya jamii, kinyume na dhamira njema ya wenye sherehe.

Aidha, alieleza kuwa wanasiasa wanapaswa kutumia majukwaa kama haya kuhamasisha mshikamano wa wananchi na kushiriki katika shughuli za maendeleo badala ya kupandikiza chuki.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kijiji cha Loiborsoit A, Lengay Lemonji, aliwashukuru wananchi kwa kumuamini na kumchagua kwa kura nyingi. 

Pia alimshukuru mgeni rasmi kwa kuhudhuria hafla hiyo.

Wanakijiji wa Loiborsoit A walimpongeza mwenyekiti wao kwa kumpatia zawadi mbalimbali kama ishara ya kuthamini mchango wake katika maendeleo ya kijiji hicho.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...