Friday, February 7, 2025

USAWA WA KIJINSIA TANZANIA: KUTOKA MKUTANO WA BEIJING HADI MATOKEO YA LEO


MWANGA katikati ya giza nene uliangazia ulimwengu Mwaka 1995,wakati ambao Mwanamke alionekana kutoweza kufanya jambo lolote bila Mwanaume, Mkutano wa Beijing-China uliibua mwongozo wa kurasa 129 uliobeba ajenda 12 ambazo zilizolenga kumuwezesha mwanamke.

Ajenda hizo zilijikita hasa katika kukabiliana na umaskini, kupata elimu na mafunzo, afya Bora, kukabiliana na mizozo ya kivita, uchumi, Mfumo wa Uongozi na upitishaji maamuzi, mifumo ya kitaasisi, haki za binadamu, vyombo vya habari,na mazingira wezeshi kwa mtoto wa kike.

Ambapo kulingana na maazimio ya Beijing Tanzania imepiga hatua kubwa katika kumuwezesha mwanamke kumiliki mali na rasimali ambapo kwenye ardhi Sheria ya ardhi imeotoa haki sawa kwa raia wote kumiliki ardhi na kwenye umiliki wa mali imekuwa ikitoa mikopo ya asilimia kumi katika halmashauri.

Aidha Mtandao wa jinsia Tanzania (TGNP) umekuwa kituo kikuu nchini ambacho kinasaidia kutoa hamasa na kuwajengea uwezo wanawake Vijana kupata uongozi kwa lengo la kuingiza idari kubwa ya wanawake katika mfumo ya maamuzi.

Aidha ushiriki wa Kisiasa wa kundi la wanawake bado ni hafifu ambapo kupitia takwimu zilizotewa na Mtandao wa jinsia nchini imeonesha kuwa bado hali sio nzuri kwani ni wanawake asilimia 2.1 pekee ndio walishiriki katika kuwania nafasi za kugombea uongozi wa serikali za mitaa na vijiji ambapo juhudi kubwa zinatakiwa kuwekwa ili kuundwe sera ambayo itajumuisha mwanamke katika kila nafasi za Maamuzi.

Mkutano wa Beijing umechagiza ushawishi mkubwa katika nchi mbalimbali ulimwenguni ambapo kupitia ajenda zake zilizo jikita katika usawa wa kijinsia zimeibua makongamano ambayo yalileta mipango ya Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs).


Aidha matunda yatokanayo na mkutano wa Beijing yameimarisha huduma Bora ya afya kwa mama na mtoto pamoja na Elimu kwa watoto wa kike ambapo serikali ya awamu ya sita imejitolea kutoa Elimu bure kuanzia shule ya msingi hadi kidato Cha sita.


Azimio la Beijing limeibua mapambano mengi ambapo vitendo vya ukatili hasa ubakaji vilivyokuwa vikishamiri vimepungia kwa asilimia kubwa kutokana na juhudi zilizofanyika kwa ajili ya kumlinda mtoto wa kike kuthaminika katika jamii.


Vilevile,kufikia usawa wa kijinsia ni muhimu kwa maendeleo endelevu katika jamii zote,kwani majukumu ya wanawake na wanaume yanajengwa kijamii, lakini mara nyingi tofauti za kijinsia zilizopo huwakosesha wanawake faida hii inazuia maendeleo yao kama binadamu wengine.


Licha ya miongo kadhaa ya juhudi za maendeleo ya jumla katika kuboresha maisha ya wanawake kumekuwa na hali isiyoridhisha kwa baadhi ya maeneo hasa katika uwakilishi wa wanawake Viongozi katika ngazi za Maamuzi.


Katika ukanda wa Afrika Mashariki, Tanzania ni mojawapo ya nchi zinazofanya vizuri katika ushiriki wa wanawake katika uongozi kulingana na takwimu za Interparliamentary Union (IPU) hadi Januari 2019, Tanzania inashika nafasi ya pili kwa nchi za Afrika Mashariki na nafasi ya 25 duniani kwa kuwa na asilimia 36.9 ya wanawake Wabunge.


Bado nchi haijaweza kufikia lengo la 50/50 na hivyo, hatuna budi kuongeza juhudi katika kuongeza nafasi za wanawake katika ngazi mbalimbali za maamuzi ili kufikia lengo hilo
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...