Saturday, February 2, 2019

Diwani aomba ufanyike uhakiki wa mashamba ya ufuta


Na. Ahmad Mmow,Lindi.

Baada ya kukamilika zoezi la uhakiki wa taarifa za wakulima wa korosho katika wilaya ya Nachingwea mkoa wa Lindi,Diwani wa kata ya Mkoka,halmashauri ya wilaya hiyo,Hamisi Kalembo (CUF)ameomba ufanyike uhakiki wa taarifa za wakulima wa ufuta.

Kalembo aliomba ombi hilo juzi wakati wa mkutano wa kawaida wa robo ya pili ya mwaka wa fedha wa 2018/2019 wa baraza la madiwani,uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa halmashauri hiyo uliopo mjini Nachingwea.

Diwani huyo alisema kufuatia kuchelewa kulipwa wakulima wa korosho msimu huu kutokana na uhakiki wa taarifa za wakulima ili kuwabaini watu waliopata zao hilo kwa njia zisizo halali.Nivizuri halmashauri hiyo ifanye uhakiki wa mashamba ya ufuta na wamiliki wake mapema.

Alisema zoezi la uhakiki wa taarifa za wakulima wa korosho limechangia kwakiasi kikubwa kuchelewa kwa malipo ya wakulima wa zao hilo msimu wa 2018/2019.Kwahiyo ili kuepuka hali hiyo isijirudie kwa wakulima wa zao la ufuta,nivema uhakiki wa tarifa za wakulima wake uanze sasa.

"Mpaka sasa wakulima wengi wa korosho hawajalipwa.Hali ambayo imesbabisha maisha magumu kwa wakulima na hata halmashauri hii.Uhakiki wa kuwabaini walionunua kwa kangomba(ununuzi nje ya mfumo rasmi) umesababisha hali hiyo.Je haitakuwa vizuri halmashauri ikaanza kufanya uhakiki,"alihoji Kalembo.

Kalembo ambae alitangaza kuwa nimiongoni mwa wakulima wa korosho ambao hadi juzi walikuwa hawajalipwa,alisema kwakuwa hata ufuta unapendwa na walanguzi,bila shaka serikali itatangaza kufanyika zoezi la uhakiki wa taarifa za wakulima wa ufuta.Hata hivyo inaweza kutangaza wakati wa uuzaji na ununuzi.Kitendo ambacho kitasababisha wakulima kuchelewa kulipwa.

Akijibu ombi la diwani huyo,mwenyekiti wa halmashauri hiyo ya wilaya ya Nachingwea,Ahmad Makoroganya,alisema zoezi la uhakiki ambalo alilitaja Kalembo lilifanywa na serikali kuu.Huku akibainisha kwamba halmashauri hiyo haikuhusika kwa mtindo wowote kuandaa,kusimamia na kutekeleza zoezi hilo.

Makoroganya aliweka wazi kwamba taarifa za wakulima wa korosho na ufuta zipo.Kwani ni miongoni mwa kazi na wajibu wa idara ya kilimo kupitia wataalamu wake.Kwahiyo hakuna sababu kwa halmashauri kufanya uhakiki huo.

JK Comedian aanza kutumia kingereza kuigiza sauti za viongozi wa Afrika (Video)

JK Comedian amefunguka kuzungumzia namna alivyoweza kuifanya kazi yake ya kuigiza sauti za viongozi mbalimbali. Pia amesema kwa sasa anajipanga kuachia filamu ya Mr JK ambayo ndani yake itakuwa na mambo mbalimbali.

The post JK Comedian aanza kutumia kingereza kuigiza sauti za viongozi wa Afrika (Video) appeared first on Bongo5.com.


Source

Huu ndio mkwara wa mashabiki wa Simba “Al ahly atakufa nyingi leo” (+ Video)

Ikiwa leo ndio siku ambayo mitanange mkubwa wa ligi ya mabingwa barani Afrika itafanyika katika mataifa tofauti barani Afrika, macho na masikio ya wengi yakonchini Misri ambako matanage kati ya Simba ya Tanzania watakipiga na Al ahly kutoka Misri. Ikumbukwe Simba wanaenda Misri tayari wakiwa nafasi ya tatu kweny kundi lao D na huu ndio …

The post Huu ndio mkwara wa mashabiki wa Simba “Al ahly atakufa nyingi leo” (+ Video) appeared first on Bongo5.com.


Source

BABA MZAZI AWAPACHIKA MIMBA MABINTI ZAKE WAWILI

 Baba wa mabinti wawili mjini Eldoret nchini Kenya anasakwa na maafisa wa polisi baada ya kuwabaka na kuwapachika mimba watoto hao kwa wakati tofauti.

Baba huyo anasemekana kuanza kuwabaka wanawe mwaka wa 2014 mama yao alipoaga dunia.

 Mshukiwa alikuwa amerejea nyumbani kutoka gerezani baada ya kukamatwa kwa kumbaka binti wake kitinda mimba.

 Kulingana na taarifa za Citizen TV, jamaa huyo alipofika nyumbani kwake, alimbaka tena bintiye mkubwa ambaye kwa sasa amempachika pia mimba. 

 Msichana huyo aliwambia wanahabari kuwa dadake mdogo alijitoa uhai mwaka wa 2018 akiwa na ujauzito wa miezi saba. 
Msichana huyo ambaye pia ni mjamzito, alisema aliwasilisha malalamishi yake kwa wazee wa kijiji ila hakuna hatua ambayo imechukuliwa dhidi ya baba yao

 Aliamua kuranda katika mitaa ya mji wa Eldoret ila wasamaria wema wajitokeza na kumpa makazi.

Wasichana hao wamekuwa wakiteseka mikononi mwa baba yao ambaye anapaswa kuwalinda tangu mama yao alipofariki mwaka wa 2014.

Friday, February 1, 2019

Mchungaji atuhumiwa kufanya mapenzi na mtoto

Mchungaji atuhumiwa kufanya mapenzi na mtoto
Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mjini Richard Kasesela amelishauri Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania KKKT Dayosisi ya Iringa kumuondoa kutomfumbia macho aliyekuwa Msaidizi wa Askofu wa Dayosisi hiyo mchungaji Yusto Kinyori kwa tuhuma za ya kufanya mapenzi
na mtoto wa mchungaji mwenzake kwenye gari.

Kasesela amesema hayo kwenye Mkutano Mkuu wa kumchagua Msaidizi wa Askofu wa kanisa hilo uliofanyika katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania KKKT usharika wa Ipogolo ambapo amesema kuwa anayo video clip ikionesha mchungaji huyo akifanya mapenzi kwenye gari na mtoto wa mchungaji mwenzake.

Kasesela amesema kuwa kinachomuuma zaidi viongozi wa dini ndiyo wanaotumwa kwenda serikali kuwawakilisha baadhi ya viongozi au kutoa matamko mbalimbali kwa niaba ya kanisa lakini kiongozi huyo amekengeuka kwa sababu ya kitendo alichokifanya na kushauri kanisa limuondoe haraka kwa sababu analiaibisha kanisa.

Kwa upande wake Askofu wa Kanisa hilo Dayosisi ya Iringa Mchungaji Blastone Gavile amesema mkutano huo maalumu umefanyika kutokana na vikao vilivyofanyika mwishoni mwa mwakajana kujadili ofisi ya msaidizi wa askofu kutokana na tuhuma zilizokuwa zikimkabili.

Mara baada ya kufanya uchaguzi huo walimpata msaidizi wa askofu Askari Mgeyekwa ambaye alikuwa mkuu wa KKKT usharika wa Kihesa na ameibuka kidedea kwa kupata kura 480, kura za hapana 17 na zilizoharibika 10 na jumla ya wapiga kura walikuwa 457.
Source

EFA yahakikishiwa ulinzi kwenye mchezo wa Al Ahly dhidi ya Simba

Chama cha Soka cha Misri (EFA) kimetangaza kuwa kimehakikishiwa ulinzi kwa mashabiki wasiozidi 10,000 ambao watahudhuria mchezo wa Al Ahly dhidi ya Simba, kesho Jumamosi katika Ligi ya Mabingwa Afrika.

Al Ahly inaongoza Kundi D katika michuano hiyo ikiwa na pointi nne wakati Simba in­ashika nafasi ya tatu kwa kuwa na pointi tatu.

Timu hizo zinatarajiwa kuku­tana kwenye Uwanja wa Borg El Arab unaoingiza watu 80,000 waliokaa kwenye siti.

Taarifa hizo zimekuja baada ya kutolewa tetesi juu ya idadi ya mashabiki ambao wanatakiwa kuingia uwanjani, hivyo Al Ahly wametakiwa kutoa idadi hiyo ya tiketi ili kukwepa adhabu kutoka Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kutokana na suala la kiusalama.

Mwamuzi wa mchezo huo anatarajiwa kuwa Maguette Ndiaye raia wa Senegal na atasaidiwa na Djibril Camara pamoja na El Hadji Malick Samba, wakati ofisa wa nne ni Daouda Gueye.

Siku chache zilizopita, Caf ilitangaza kuiondoa Ismaily ya Misri katika michuano hiyo kutokana na mashabiki wao kuonyesha utovu wa nidhamu uliovuka mipaka ikiwemo kurusha mawe uwanjani, chupa za maji, kwa mwamuzi wa akiba na kwa mashabiki wageni katika mchezo wa timu hiyo dhidi ya Club Africain, Januari 18, mwaka huu.

MSAIDIZI WA ASKOFU KKKT AREKODIWA AKIFANYA MAPENZI NA MTOTO WA MCHUNGAJI MWENZAKE



Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mjini Richard Kasesela

Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mjini Richard Kasesela amelishauri Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania KKKT Dayosisi ya Iringa kumuondoa /kutomfumbia macho aliyekuwa Msaidizi wa Askofu wa Dayosisi hiyo mchungaji Yusto Kinyori kwa tuhuma ya kufanya mapenzi na mtoto wa mchungaji mwenzake kwenye gari.

Kasesela amesema hayo kwenye Mkutano Mkuu wa kumchagua Msaidizi wa Askofu wa kanisa hilo uliofanyika katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania KKKT usharika wa Ipogolo ambapo amesema kuwa anayo video clip ikionesha mchungaji huyo akifanya mapenzi kwenye gari na mtoto wa mchungaji mwenzake.

Kasesela amesema kuwa kinachomuuma zaidi viongozi wa dini ndiyo wanaotumwa kwenda serikali kuwawakilisha baadhi ya viongozi au kutoa matamko mbalimbali kwa niaba ya kanisa lakini kiongozi huyo amekengeuka kwa sababu ya kitendo alichokifanya na kushauri kanisa limuondoe haraka kwa sababu analiaibisha kanisa.

Kwa upande wake Askofu wa Kanisa hilo Dayosisi ya Iringa Mchungaji Blastone Gavile amesema mkutano huo maalumu umefanyika kutokana na vikao vilivyofanyika mwishoni mwa mwakajana kujadili ofisi ya msaidizi wa askofu kutokana na tuhuma zilizokuwa zikimkabili.

Mara baada ya kufanya uchaguzi huo walimpata msaidizi wa askofu Askari Mgeyekwa ambaye alikuwa mkuu wa KKKT usharika wa Kihesa na ameibuka kidedea kwa kupata kura 480, kura za hapana 17 na zilizoharibika 10 na jumla ya wapiga kura walikuwa 457.
Chanzo - EATV

Mziwanda Akiri Kuwa Muziki wake Umeuliwa na Mapenzi.

Msanii Nuh mziwanda amefunguka leo alipokuwa akiongea na leo tena ya Couds Fm na kusema kuwa muziki wake kwa sasa umekufa na anakbali kuwa muziki huo kwa sasa umekufa kwa sababu ya  uzembe katika mapenzi. Nuh mziwanda amefunguka na kusema kuwa pamoja na kwambaaliwahi kufanya vizuri sana lakini kitu kikubwa anachokiri kuwa kinampoteza katika ulimwengu wa muziki ni baada ya kuoa na kuna misukosuko mingi ilitokea na kufanya kuachana na mke wake ambae alikuwa pia ni mzazi mwenzake. Nuh anasema kuwa baada ya hayo  yote aliona kabisa jinsi anavyoyumba na kumfanyya kuyumba na ndio maana hata alitoa wimbo wa natapatapa ambao ulikuwa ni storo ya kweli ya maisha yake halisi kwa muda huo. Nuh aliwahi kuwa katika mahusiano na shiloleh na baadae kuachana na ndipo alipofunga ndoa na mwanamke mwingine ambae walizaa mtoto mmoja na kisha kushi ndwa kukaa pamoja na kuachana.

The post Mziwanda Akiri Kuwa Muziki wake Umeuliwa na Mapenzi. appeared first on Ghafla! Tanzania.


Source

Wanaume kabla ya kuoa huangalia mwanamke mwenye sifa hizi

Wanaume wengi wanapofikia hatua ya kuoa si kwamba wanakurupuka tu na kuoa mwanamke yeyote mwenye sura nzuri, bali huchukua muda wao mwingi kuchunguza mambo mengi juu ya wake ambao wanadhani kwamba wanaweza kuwa pamoja kwa kipindi chote cha maisha.

Wanawake wengi wanajisahau na kudhani kwamba kitu kinachoweza kuwafanya wakapata wachumba ni uzuri hivyo kupoteza muda wao kujichubua na kujiremba ili wawavutie wanaume bila kujua kwamba kuolewa ni zaidi ya uzuri.

Hali sasa hivi imebadilika ni tofauti na kipindi cha nyuma ambapo ukiwa na sura nzuri na umbo la kuvutia basi una asilimia 100 za kuolewa.

Utafiti ambao nimeufanya unaonesha kwamba zaidi ya uzuri wa tabia na umbo, kuna kuna sifa nyingine za msingi ambazo mwanamke anatakiwa kuwa nazo ili aweze kuwa katika mazingira mazuri ya kupata mchumba wa kumuoa kiasi kwamba asipokuwa nazo ataishia kuchezewa tu lakini haitatokea mtu kumtakiwa kwamba anataka kumuoa.

1. Mwenye mapenzi ya kweli.
Lengo kubwa la mwanaume kuoa ni kutaka kupata mapenzi ya kweli kutoka kwa mwanamke na ikiwezekana waweze kupata watotoa ambapo watoto hao ndio furaha ya ndoa. Wapo wanawake wengine ambao wanonesha wazi kutokuwa na mapenzi ya kweli bali wanakuwa na mapenzi ya kuzuga. Wanachotaka wao aidha kupata umaarufu tu kwamba yuko na mtu fulani ama kuweza kupata pesa alizonazo mwanaume lakini sio kwamba ana mapenzi ya dhati kutoka moyoni mwake.

Mwanamke asiye na mapenzi ya dhati utamgundua tu, muda mwingiutamuona macho yake yako kwenye mfuko wa mwanaume. Akiona kwamba mfuko umetuna utaona anaonesha mapenzi ya hali ya juu lakini pindi hali inapokuwa kubwa mbaya kifedha mapenzi yanaanza kufifia.

Kwanini wanaume wanapenda wana wake wenye mapenzi ya dhati kutoka mioyoni mwao na si kutokana na fedha walizonazo? Hii inatokana na ukweli kwamba maisha siku zote yanabadilika, kama waswahili wanavyosema, kuna kupanda na kushuka.

Sio kwamba kila siku utakuwa na maisha mazuri na kama itatokea hivyo basi ushukuru mungu.Hivyo basi mwanamke wa kuoa lazima afahamu hivyo na awe tayari kuonesha mapenzi yake ya dhati wakati wote wa maisha yao na si kwa kipindi fulani tu cha neema.

Si hivyo tu pia asilimia kubwa ya maisha ya ndoa yanatawaliwa na mapenzi, kwa hiyo nyanja hiyo inakuwa ya msingi sana kwa wanaume wengi kuiangalia ili wasije wakajikuta wanaoa mwanamke ambaye baada ya muda mapenzi yanakwenda likizo hali ambayo inaweza kuwafanya wasiishi maisha ya raha mustarehe.

2. Wenye tabia nzuri
Tabia njema ndio silaha ya maisha, ukiwa na tabia nzuri kila mtu atakupenda, hiyo ni katika maisha ya kawaida. Lakini linapokuja sualana kuoa tabia inakuwa kitu cha awali sana kungaliwa na hiyo inaweza kuwa na ukweli kwa sababu wapo wasichana wazuri wenye mvuto wa aina yake na maumbile mazuri, lakini wanakosa wanaume wa kuwaoa, ukiuliza kwani utaambiwa anatabia mbaya.

Naweza kusema hilo ndilo limekuwa tatizo kubwa kwa baadhi ya wanawake kukosa wanaume wa kuwaona. Hakuna mwanaume hata mmoja kati ya wale ambao nimejaribu kuongea naye ambaye ameonesha kulidharau suala hilo la tabia.

Si hivyo tu wapo wanaume ambao wameingia kichwa kichwa na kuoa kwa kuangalia sura tu bila kujali tabia, matokeo yake baada ya siku chache yanatokea machafuko ya aina yake hali ambayo imepelekea kuvunjika kwa ndoa kutokana na tabia mbaya alizonazo mwanamke.

3. Mwenye uchu wa maendeleo
Hivi karibuni kumekuwepo na mabadiliko ya aina yake kwa wanaume, wengi sasa hivi hawapendi kabisa kuoa mwanamke ambaye hana kazi yaani 'golikipa'. Kama atakuwa hana kazi basi awe na uchu wa maendeleo kwa kujituma kufanya kazi mbalimbali za kimaendeleo kama vile kilimo kwa wale walio vijijini na biashara ndogondogo kwa wale ambao wako mijijini na hata vijijini.

Ile dhana ya kusema mwanamke ni mama wa nyumbani wa kukaa na kujipodoa akimsubiria mwnaume arudi amstarehesha, sasa hivi imepitwa na wakati. Wanaume wengi wanapenda wanawake ambao ni wahangaikaji, wenye ndoto za maendeleo katika maisha yao. Hata kama watakuwa si wafanyakazi lakini wawe wenye kutoa ushauri kwa waume zao juu ya jinsi gani wafanye ili wafanikiwe.

4. Wasiopenda makuu.
Kuna wanawake wengine wanakuwa na tabia za ajabu sana kiasi kwamba yaweza kuwa kero kwa wanaume. Wapo wanawake ambao wanapenda makuu bila kujali hali halisi ilivyo. Kuna wanawake naweza kusema wana tamaa, kila wikiendi utamsikia "leo tunakwenda wapi dear?"

Akimuona rafiki yake kanunua simuya laki tatu na yeye utamsikia akisema, 'na mimi naomba uninunulie simu kama ya Grace'. Ukienda naye Pub anakuambia,"mimi sinywi pombe za chupa natumia za kopo tena Heineken'. Yeye hajali kiasi cha pesa mwanaume alicho nacho na usipotekelezea anachukia na anaweza hata kupunguza mapenzi.

Wanawake kama hawa wako katika mazingira magumu sana ya kuweza kupata wanaume wa kuwaoa. Mara nyingi katika maisha fedha huzungumza, kama mwanaume atakuwa na pesa ya kutosha itakuwa rahisi sana kwa mwanamke kupata kila atakachopenda lakini si kwa kumwambia mimi nataka kitu fulani.Mwanaune mwenyewe utamsikia akisema, 'unataka nikununulie simu ya aina gani, au leo unataka twende wapi?' hapo ndipo utakuwa na nafasi ya kusema, 'mimi nataka uninunulie simu kama ya fulani ama leo nataka twende sehemu fulani.'

Wanaume ni warahisi sana wa kuwapatia wale ambao wanatarajia kuwaoa chochote ambacho watahitaji kama tu pesa haitakuwa tatizo. Kitu ambacho kinawaudhi wanaume wengi ni ile tabia ya mwanamke kupenda mambo makubwa bila kuangalia uwezo uliopo kwa mwanume.

Kuna wanawake wengine wao si wasemaji kabisa, yeye anasubiri leoamemletea hiki, anapokea na kushukuru, kesho akiambiwa twende beach anakubali. Au wengine wanasubiri mpaka waulizwe wanataka nini, ndio wanasema.

Sisemi kwamba uwe mkimya tu hata kama una shida ya kitu fulani na unafahamu kwamba ukimweleza mwenza wako anaweza kukusaidia, hapana! kama unaona kwamba uwezekano wa kupata kile ambacho unakihitajiupo mweleze kwa utaratibu naamini atakuelewa na kukutimizia.Tabia ambayo hawaipendi wanaume wengi ni ile ya kulazimisha ufanyiwe kitu fulaniwakati inawezekana uwezekano haupo.

5. Wavumilivu.
Wapo wanawake ambao sio wavumilivu kabisa katika maisha.Tunajua kwamba maisha siku zote hayatabiriki, yanaweza kutokea matatizo ya kiafya ama kifedha.Huu ndio wakati wa kuona uvumilivu wa mtu.Kama mwanamke anatarajia kwamba siku zote ni za raha tu na pindi matatizo yanapotokea anachukua uamuzi wa kumtoroka mwanume, huyo siyo mwanamke wa kuoa.

Wangapi leo hii huwatoroka waume zao pindi inapotokea kuumwa, kufilisika ama kupatwa na tatizo lolote ambalo kwa namna moja ama nyingine yanaweza kuwafanya maisha yao kutingishika?

Uvumilivu kwa mwanamke utakuwepo kama tu atakuwa na mapenzi ya dhati kama nilivyozungumza hapo awali. Mwanamke mweye mapenzi ya dhati ni lazima atakuwa mvumilivu na atakuwa tayari kuishi katika maisha ya aina yoyote, yawe ya raha ama ya starehe.Hawa ndio wale ambao wanaume wengi wengependa kuwa nao maishani mwao.

Kwa maana hiyo basi hiyo iwe changamoto kwa wanawake. Wajue kwamba wanaume wanafurahi kuwa na wanawake wa aina gani. Hata kama utakuwa umeshaolewa, kama kuna wakati kunakuwa na kutokuelewana baina yenu, chunguza yawezekana kwamba unakosa mojawapo ya tabia ambazo nimezitaja hapo juu. Waweza kubadilika kwani inawezekana.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...