Chama cha Soka cha Misri (EFA) kimetangaza kuwa kimehakikishiwa ulinzi kwa mashabiki wasiozidi 10,000 ambao watahudhuria mchezo wa Al Ahly dhidi ya Simba, kesho Jumamosi katika Ligi ya Mabingwa Afrika.
Al Ahly inaongoza Kundi D katika michuano hiyo ikiwa na pointi nne wakati Simba inÂashika nafasi ya tatu kwa kuwa na pointi tatu.
Timu hizo zinatarajiwa kukuÂtana kwenye Uwanja wa Borg El Arab unaoingiza watu 80,000 waliokaa kwenye siti.
Taarifa hizo zimekuja baada ya kutolewa tetesi juu ya idadi ya mashabiki ambao wanatakiwa kuingia uwanjani, hivyo Al Ahly wametakiwa kutoa idadi hiyo ya tiketi ili kukwepa adhabu kutoka Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kutokana na suala la kiusalama.
Mwamuzi wa mchezo huo anatarajiwa kuwa Maguette Ndiaye raia wa Senegal na atasaidiwa na Djibril Camara pamoja na El Hadji Malick Samba, wakati ofisa wa nne ni Daouda Gueye.
Siku chache zilizopita, Caf ilitangaza kuiondoa Ismaily ya Misri katika michuano hiyo kutokana na mashabiki wao kuonyesha utovu wa nidhamu uliovuka mipaka ikiwemo kurusha mawe uwanjani, chupa za maji, kwa mwamuzi wa akiba na kwa mashabiki wageni katika mchezo wa timu hiyo dhidi ya Club Africain, Januari 18, mwaka huu.
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Tanzania November 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na za ny...
-
Mhamasishaji maarufu wa mitandaoni, Mwijaku, ameandika ujumbe unaotoa ushauri kwa Rais wa klabu ya Yanga, Injinia Said Hersi, kupitia ukuras...
-
Zaidi ya ghorofa 100 jijini Dar es Salaam zilibainika kujengwa kinyume cha taratibu za ujenzi, Bunge lilielezwa. Kwa mujibu wa ripoti iliy...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 9, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na ...
-
Msimamo Ligi Kuu Bara 2024/2025 Msimamo Ligi Kuu Bara 2024/2025, NBC Premier League Tanzania Msimamo Ligi Kuu NBC 2024/2025 Tanzania Premier...
-
Msanii maarufu Ntemi O Mabala ' Ng'wana Kang'wa kutoka Kahama Mkoani Shinyanga anakualika kusikiliza wimbo wake mpya unaitwa M...
-
Na Mbuke Shilagi Kagera. Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko amesema kuwa mradi wa umeme wa maji ya maporomoko wa Rusumo...
-
Hii hapa ngoma mpya ya Msanii wa Nyimbo za asili Mama Ushauri ameshirikiana na Ng'wana Ng'washi inaitwa Merimela ,imetengenezwa Lw...
-
Msanii wa nyimbo za asili Nyanda Madirisha Obhado 'Maliganya' maarufu Shikomba Bhulolo anakualika kusikiliza wimbo wake mpya 2021 un...