Msanii Nuh mziwanda amefunguka leo alipokuwa akiongea na leo tena ya Couds Fm na kusema kuwa muziki wake kwa sasa umekufa na anakbali kuwa muziki huo kwa sasa umekufa kwa sababu ya uzembe katika mapenzi. Nuh mziwanda amefunguka na kusema kuwa pamoja na kwambaaliwahi kufanya vizuri sana lakini kitu kikubwa anachokiri kuwa kinampoteza katika ulimwengu wa muziki ni baada ya kuoa na kuna misukosuko mingi ilitokea na kufanya kuachana na mke wake ambae alikuwa pia ni mzazi mwenzake. Nuh anasema kuwa baada ya hayo yote aliona kabisa jinsi anavyoyumba na kumfanyya kuyumba na ndio maana hata alitoa wimbo wa natapatapa ambao ulikuwa ni storo ya kweli ya maisha yake halisi kwa muda huo. Nuh aliwahi kuwa katika mahusiano na shiloleh na baadae kuachana na ndipo alipofunga ndoa na mwanamke mwingine ambae walizaa mtoto mmoja na kisha kushi ndwa kukaa pamoja na kuachana.
The post Mziwanda Akiri Kuwa Muziki wake Umeuliwa na Mapenzi. appeared first on Ghafla! Tanzania.
Source