Saturday, February 2, 2019

Diwani aomba ufanyike uhakiki wa mashamba ya ufuta


Na. Ahmad Mmow,Lindi.

Baada ya kukamilika zoezi la uhakiki wa taarifa za wakulima wa korosho katika wilaya ya Nachingwea mkoa wa Lindi,Diwani wa kata ya Mkoka,halmashauri ya wilaya hiyo,Hamisi Kalembo (CUF)ameomba ufanyike uhakiki wa taarifa za wakulima wa ufuta.

Kalembo aliomba ombi hilo juzi wakati wa mkutano wa kawaida wa robo ya pili ya mwaka wa fedha wa 2018/2019 wa baraza la madiwani,uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa halmashauri hiyo uliopo mjini Nachingwea.

Diwani huyo alisema kufuatia kuchelewa kulipwa wakulima wa korosho msimu huu kutokana na uhakiki wa taarifa za wakulima ili kuwabaini watu waliopata zao hilo kwa njia zisizo halali.Nivizuri halmashauri hiyo ifanye uhakiki wa mashamba ya ufuta na wamiliki wake mapema.

Alisema zoezi la uhakiki wa taarifa za wakulima wa korosho limechangia kwakiasi kikubwa kuchelewa kwa malipo ya wakulima wa zao hilo msimu wa 2018/2019.Kwahiyo ili kuepuka hali hiyo isijirudie kwa wakulima wa zao la ufuta,nivema uhakiki wa tarifa za wakulima wake uanze sasa.

"Mpaka sasa wakulima wengi wa korosho hawajalipwa.Hali ambayo imesbabisha maisha magumu kwa wakulima na hata halmashauri hii.Uhakiki wa kuwabaini walionunua kwa kangomba(ununuzi nje ya mfumo rasmi) umesababisha hali hiyo.Je haitakuwa vizuri halmashauri ikaanza kufanya uhakiki,"alihoji Kalembo.

Kalembo ambae alitangaza kuwa nimiongoni mwa wakulima wa korosho ambao hadi juzi walikuwa hawajalipwa,alisema kwakuwa hata ufuta unapendwa na walanguzi,bila shaka serikali itatangaza kufanyika zoezi la uhakiki wa taarifa za wakulima wa ufuta.Hata hivyo inaweza kutangaza wakati wa uuzaji na ununuzi.Kitendo ambacho kitasababisha wakulima kuchelewa kulipwa.

Akijibu ombi la diwani huyo,mwenyekiti wa halmashauri hiyo ya wilaya ya Nachingwea,Ahmad Makoroganya,alisema zoezi la uhakiki ambalo alilitaja Kalembo lilifanywa na serikali kuu.Huku akibainisha kwamba halmashauri hiyo haikuhusika kwa mtindo wowote kuandaa,kusimamia na kutekeleza zoezi hilo.

Makoroganya aliweka wazi kwamba taarifa za wakulima wa korosho na ufuta zipo.Kwani ni miongoni mwa kazi na wajibu wa idara ya kilimo kupitia wataalamu wake.Kwahiyo hakuna sababu kwa halmashauri kufanya uhakiki huo.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...