Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amemteua Bi. Ummy Ally Mwalimu kuwa Mshauri wa Rais anayeshughulikia Masuala ya Afya ya Uzazi, Mama na Mtoto.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt. Moses Kusiluka, uteuzi huo umetangazwa leo Juni 2, 2026 kupitia Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu.
Bi. Ummy Mwalimu ni mmoja wa viongozi wenye uzoefu mkubwa katika utumishi wa umma nchini, akiwa amewahi kushika nyadhifa mbalimbali za uwaziri katika Serikali ya Tanzania. Katika kipindi cha uongozi wake, amewahi kuhudumu katika sekta za afya, mazingira, Wizara ya Katiba na Sheria pamoja na Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).
