Friday, May 29, 2026

MADIWANI WAASWA KUWA CHACHU YA MAENDELEO KISHAPU NA KUEPUKA MGONGANO WA MASLAHI

 Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Peter Masindi akifungua mafunzo ya madiwani wa Halmashauri hiyo yakuwajengea uwezo katika masuala ya maadili,rushwa na kukumbushwa wajibu wao ambayo yametolewa na Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU Mkoa wa Shinyanga

Na Stella Herman,Shinyanga

Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Peter Masindi, amewataka madiwani kusimamia kwa umakini miradi ya maendeleo katika maeneo yao huku akisisitiza kuwa wao ndiyo wawakilishi wa wananchi na nguzo muhimu ya maendeleo ya Taifa.

Akizungumza  wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo madiwani kuhusu kujiepusha na vitendo vya rushwa, kubaini mianya ya rushwa pamoja na kuwakumbusha maadili na wajibu wao, Masindi amesema viongozi hao wanapaswa kuwa chachu ya mabadiliko kwa kuwajibika ipasavyo katika maeneo wanayoyaongoza.

Amesema wananchi wanawategemea madiwani kuwasimamia na kuwawakilisha vizuri, hivyo wanapaswa kuangalia changamoto zilizopo katika kata zao na kuchukua hatua kwa wakati ili kuhakikisha maendeleo yanapatikana.

“Wananchi watawapima baada ya miaka mitano kwa kazi mtakazozifanya, Maendeleo ya kata yanawategemea ninyi, msipofanya maamuzi sahihi kata zenu haziwezi kupata maendeleo,” amesema Masindi.

Aidha amewataka madiwani kufanya kazi kwa kuzingatia maadili, nidhamu pamoja na kutunza siri za vikao na majukumu yao, akieleza kuwa dhamana waliyopewa ni kubwa ndiyo maana Serikali imeamua kutoa mafunzo hayo ili kuwakumbusha wajibu wao kwa wananchi.

Kwa upande wake, Mwendesha Mashitaka wa TAKUKURU Mkoa wa Simiyu ambaye pia ni wakili  Maximilian Kyabona, amewaasa madiwani kujiepusha kutanguliza maslahi binafsi mbele na kusahau kuwa wao ni wawakilishi wa wananchi.

Kyabona amesema madiwani ndiyo watakaowezesha Halmashauri ya Kishapu kupata maendeleo iwapo watawajibika ipasavyo, kupinga rushwa na kufichua mianya yote inayoweza kusababisha miradi ya maendeleo kushindwa kutekelezwa.

Alitaja baadhi ya mambo ambayo madiwani wanapaswa kuyaepuka kuwa ni pamoja na kubadili vifungu vya matumizi ya fedha, kuchukuliana posho pamoja na kujihusisha na zabuni mbalimbali zinazoweza kuleta mgongano wa maslahi.

Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Peter Masindi akifungua mafunzo ya madiwani wa Halmashauri hiyo yakuwajengea uwezo katika masuala ya maadili,rushwa na kukumbushwa wajibu wao ambayo yametolewa na Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU Mkoa wa Shinyanga
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kishapu Josephat Limbe akizungumza wakati wa mafunzo kwa madiwani yaliyotolewa na TAKUKURU
Mwendesha mashitaka wa TAKUKURU Mkoa wa Simiyu Maximilian Kyabona akitoa elimu ya masuala ya rushwa na maadili kwa madiwani wa Halmashauri ya Kishapu
Mkuu wa TAKUKURU Wilaya ya Kishapu Atuganile Stephen akifuatilia mafunzo ya madiwani
Mwendesha mashitaka wa TAKUKURU Mkoa wa Simiyu Maximilian Kyabona akitoa elimu ya masuala ya rushwa na maadili kwa madiwani wa Halmashauri ya Kishapu
Mwendesha mashitaka wa TAKUKURU Mkoa wa Simiyu Maximilian Kyabona akitoa elimu ya masuala ya rushwa na maadili kwa madiwani wa Halmashauri ya Kishapu
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Peter Masindi akifungua mafunzo ya madiwani wa Halmashauri hiyo yakuwajengea uwezo katika masuala ya maadili,rushwa na kukumbushwa wajibu wao ambayo yametolewa na Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU Mkoa wa Shinyanga

Mwendesha mashitaka wa TAKUKURU Mkoa wa Simiyu Maximilian Kyabona akitoa elimu ya masuala ya rushwa na maadili kwa madiwani wa Halmashauri ya Kishapu
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kishapu Josephat Limbe akizungumza wakati wa mafunzo kwa madiwani yaliyotolewa na TAKUKURU
Mkuu wa TAKUKURU Wilaya ya Kishapu Atuganile Stephen 
amesema mafunzo hayo yamelenga kuwakumbusha madiwani wajibu wao pamoja na suala la maadili katika kusimamia miradi na kujiepusha kutanguliza mbele maslahi yao binafsi badala ya kuwatumikia wananchi waliowachagua.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...