Monday, March 3, 2025

Aliyechezesha Uume Juu ya Nyeti za Mtoto Akamatwa



Jeshi la Polisi Mkoa wa Mtwara linamshikilia Abdalah Hassani Masangule (56) Mlinzi wa Shule ya Sekondari Tandika na Mkazi wa Mtaa wa Mmingano kwa tuhuma za udhalilishaji wa kingono ambapo Mlinzi huyo kwa nyakati tofauti alikuwa akimlaghai Mwanafunzi wa darasa la tatu mwenye umri wa miaka 11 ( jina la shule limehifadhiwa) na kumvua nguo kisha kutoa uume wake na kuuchezesha juu ya sehemu za siri za Mwanafunzi huyo mpaka anapomaliza haja yake.

Taaarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara imesema "Mtuhumiwa amekuwa akimfanyia vitendo vya unyanyasaji Mhanga huyo na uchunguzi wa awali umebaini kuwa Mtuhumiwa alianza kujenga ukaribu na Mtoto huyo kisha kumlaghai na kutekeleza kitendo hicho, upelelezi wa shauri hilo unaendelea utakapo kamilika atafikishwa Mahakamani"

"Jeshi la Polisi Mkoa wa Mtwara linawataka Wananchi kuwa hakutakuwa na muhali kwa Mtu yeyote atakayejaribu au kufanya vitendo vya ukatili, unyanyayasaji na udhalilishaji wa aina yoyote ile na watachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria"
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...