Sunday, February 9, 2025

SIMBACHAWENE AUNGANA NA FAMILIA YA LOWASA KWENYE IBADA YA SHUKRANI



Na Barnabas Kisengi Arusha

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene leo February 09,2025 ameungana na wanafamilia, viongozi wa chama, serikali na wananchi katika Ibada ya shukrani ya Waziri Mkuu Mstaafu, Hayati Edward Lowassa.

Ibada hiyo imefanyika katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Monduli mkoani Arusha, ikiwa ni mwaka mmoja tangu Taifa lilipompoteza kiongozi huyo.

Akizungumza kwa niaba ya Familia ya Hayati Edward Lowassa, Mwanae ambaye pia ni Mbunge wa Monduli, Fredrick Lowassa ametumia fursa hiyo kuwashukuru wananchi wote waliokuwa pamoja tangu Baba yao alipofariki hadi hivi sasa huku akimshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa mchango wake mkubwa wa kuwa pamoja na familia hiyo tangu Baba yao alipoanza kuugua hadi umauti ulipomkuta

"Kwa unyenyekevu mkubwa ninawaomba Watanzania wote tuendelee kumuenzi Hayati Edward Lowassa kwa yale yote mazuri aliyoyafanya enzi za uhai wake" amesisitiza Fredrick Lowassa

Naye, Baba Askofu Mstaafu wa KKKT Dayosisi ya Kaskazini Kati, Dkt. Solomon Masangwa ameitaka familia hiyo kuzidi kumuangukia Mwenyezi Mungu katika kila jambo wanalolifanya.










Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...