Monday, February 10, 2025
Naibu Waziri Mkuu aipongeza Al- Hikma kwa kukuza Mashindano ya kuhifadhi Qur’aan
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amewaasa waislamu nchini kuendelea kumcha Mungu na kutenga muda wa kujifunza na kuisoma Qur'aan Tukufu ambayo itawafunza mambo mema yaliyoelekezwa na Mwenyezi Mungu.
Dkt. Biteko amesema hayo leo Februari 9, 2025 jijini Dar es salaam wakati akizindua Mashindano Makubwa zaidi ya Qur'aan Tukufu Ulimwenguni 2025.
" Nawaomba msivunjike moyo akitokea mwenye tafsiri tofauti nyie msivunjike moyo wala kukatishwa tamaa bali mfanye mashindano haya yawe kinara na kuutangaza uislamu katika ulimwengu," amesema Dkt. Biteko.
Pia amewahimiza kumuomba Mungu ili Qur'aan iwanyanyue na isiwabwage katika shughuli mbalimbali wanazofanya kama kaulimbiu ya mwaka huu inavyosema " Qur'aan Ikunyanyue, Isikubwage".
Amesema Qur'aan inatoa funzo kwa watu na kuwa waasisi wake waliyaanzisha kwa ngazi ya madrasa lakini baadaye kutokana na umuhimu wake yakavutia wengi zaidi na kuwa mashindano ngazi ya mtaa, kata, wilaya, mkoa hadi kuwa ya Afrika Mashariki, Bara la Afrika na kisha kufikia ngazi ya kuwa mashindano ya Ulimwengu
" Mashindano haya mbali na kuwa yanachochea usomaji wa Qur'aan Tukufu na hivyo kujenga uelewa wa hofu ya Mwenyezi Mungu lakini pia yanaitangaza Tanzania katika taswira chanya," amebainisha Dkt. Biteko.
Ameendelea kusema kuwa Nabii Musa aliwalingania watu wake kwa kutumia muongozo kutoka katika Taurati, Nabii Daudi yeye akatumia Zaburi, Nabii Issa (Yesu) akatumia Injili na Mtume Muhamad swalla llahu alayhi wasallam akatumia Qur'aan tukufu kuwalingania watu wa umma wake.
"Kimsingi vitabu hivi vya muongozo vinamfundisha binadamu tabia njema na kumsihi kuzishikilia na kumuonesha tabia zisizofaa na kumuasa kukaa mbali nazo."
Dkt. Biteko amerejea aya katika Qur'aan tukufu sura ya 35, Surat Faatir, aya ya 28 "… kwa hakika wanaomcha Mwenyezi Mungu miongoni mwa waja wake ni wanazuoni".
Amefafanua " Aya hii ina maanisha kuwa wale waliopata ujuzi na mafundisho ya Mwenyezi Mungu ambayo yanapatikana katika Qur'aan tukufu na kuyazingatia yale waliyojifunza ndio wanaofika daraja la uchamungu."
Vilevile, Dkt. Biteko ameipongeza Taasisi ya Al- Hikma kwa jitihada zake za kukuza Mashindano ya kuhifadhi Qur'aan Tukufu ulimwenguni.
Mkurugenzi Mkuu wa Al- Hikma na Mwenyekiti wa Mashindano ya Qur'aan Tukufu Ulimwenguni, Sheikh Nurdin Kishk amesema kuwa mashindano hayo yameendelea kukua kila mwaka kutokana na mapenzi ya kuhifadhi Qur'aan.
Aidha, ameishukuru Serikali kwa ushirikiano wake na kwa kuridhia mashindano hayo kufanyika katika Uwanja wa Taifa mnamo Machi 16, 2025 ambapo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi anatarajiwa kuwa mgeni rasmi.
" Mashindano haya yanayofanywa na Al- Hikma Foundation yameweka alama ambayo haitafutika na mataifa mbalimbali yameanza kuyaiga. Pia, Mashindano Makubwa Zaidi ya Qur'aan Tukufu Afrika sasa yatajulikana kama Mashindano Makubwa Zaidi ya Qur'aan Tukufu kwa Mabara yote ya Ulimwengu ," amesema Sheikh Kishk
Akizungumza kwa niaba ya Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheikh Ali Ngerukwa amesema kuwa Mufti Mkuu yupo tayari kushirikiana na taasisi mbalimbali ikiwemo ya Ali- Hikma katika kutekeleza shughuli zao.
-
Baadhi ya raia walioyatoroka makaazi yao baada ya mlipuko wa volkano uliotokea usiku wa kuamkia huko mjini Goma mashariki mwa Jamhuri ya Kid...
-
Mhamasishaji maarufu wa mitandaoni, Mwijaku, ameandika ujumbe unaotoa ushauri kwa Rais wa klabu ya Yanga, Injinia Said Hersi, kupitia ukuras...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Zaidi ya ghorofa 100 jijini Dar es Salaam zilibainika kujengwa kinyume cha taratibu za ujenzi, Bunge lilielezwa. Kwa mujibu wa ripoti iliy...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Tanzania November 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na za ny...
-
Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala ndogo ya Dar es Salaam, imetupilia mbali shauri lililokuwa limefunguliwa na Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina...
-
Msanii maarufu Ntemi O Mabala ' Ng'wana Kang'wa kutoka Kahama Mkoani Shinyanga anakualika kusikiliza wimbo wake mpya unaitwa M...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 9, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na ...
-
Msimamo Ligi Kuu Bara 2024/2025 Msimamo Ligi Kuu Bara 2024/2025, NBC Premier League Tanzania Msimamo Ligi Kuu NBC 2024/2025 Tanzania Premier...
-
Hii hapa ngoma mpya ya Msanii wa Nyimbo za asili Mama Ushauri ameshirikiana na Ng'wana Ng'washi inaitwa Merimela ,imetengenezwa Lw...