Binti aliyefahamika kwa Jina la Rabia Poul (19) Mwanafunzi wa Kidato cha Nne katika Shule ya Sekondari Nyanza Mkazi wa Mtaa wa Barabara ya Msalala Manispaa ya Geita amefariki Dunia kwa kujinyonga February 11 Mwaka huu.
Akizungumza na Millardayo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita , SACP. Safia Jongo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo huku akisema chanzo cha kifo cha Mwanafunzi huyo ni kufeli Mtihani wa Kidato cha Nne.
" Binti amejinyonga hadi kufa na tukio hili limetokea siku ya tarehe 11 mwezi wa pili 2025 na chanzo cha tukio hili Mwanafunzi huyo kugundua kwamba amefeli kidato cha nne kwa kupata Division 0 , " SACP. Jongo.
Aidha SACP. Jongo ametoa wito kwa Wazazi na Wlezi kuwajua Watoto wao na kuwalea katika maadili ya kumpendeza Mwenyezi mungu huku akisema kuna baadhi ya Watoto wana vipaji wasizuiwe na waachwe kutokana labda wamefeli isiwe kigezo cha kukaripia Watoto.