Saturday, December 14, 2024

WIZARA YA ELIMU YARIDHISHWA NA MIRADI YA TEA CHALINZE



 Mwalimu mkuu wa shule ya Msingi Kibiki Bi. Magreth Kileo (aliyesimama), akitoa taarifa ya ujenzi wa miradi ya madarasa chini ya ufadhiri wa mamlaka ya Elimu Tanzania(TEA) kwa Mkurugenzi Msaidizi wa uthibiti ubora wa elimu toka wizara ya Elimu, sayansi na teknolojia Bi. Monica Mpululu (katikati) na Afisa miradi toka TEA ,Bi. Mwafatma Mohamed(kulia)
AFISA elimu awali na msingi halmashauri ya Chalinze Bi. Miriam Kihiyo (kulia) na Mthibiti  mkuu ubora wa shule wa halmashauri hiyo(kushoto)


NA. ELISANTE KINDULU, CHALINZE

MKURUGENZI msaidizi wa uthibiti ubora wa elimu Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia, Bi. Monica Mpululu, ameridhishwa na miradi ya ujenzi wa madarasa katika halmashauri ya Chalinze mkoa wa Pwani.

Bi. Monica, aliyasema hayo hivi karibuni alipotembelea shule ya Msingi Kibiki akiambatana na viongozi mbalimbali kutoka mamlaka ya elimu Tanzania(TEA).

Mkurugenzi huyo alisema, ujenzi wa madarasa matatu, ofisi ya mwalimu mkuu pamoja matengezo ya madawati yaliyofadhiliwa na TEA, umefanyika kwa ustadi mkubwa japo kuna sehemu ndogo ya kufanya marekebisho kutokana na changamoto ya ardhi.

Naye mwalimu mkuu wa shule hiyo Bi. Magreth Kileo aliishukuru TEA kwa miradi hiyo ingawa shule bado inakabiliwa na uhaba wa  nyumba za walimu, upungufu wa madawati na ofisi ya walimu.

Mkurugenzi huyo aliambatana na Bi. Mwafatma Mohamed(afisa miradi wa TEA),  Bi. Eliafile Solla(afisa uhusiano wa TEA ),Bi. Miriam Kihiyo(afisa elimu ya awali na msingi halmashauri ya Chalinze) na Mthibiti mkuu wa shule halmashauri ya Chalinze.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...