Tuesday, December 17, 2024

Airtel Tanzania yazindua promosheni ya Airtel Santa Mizawadi Kuwazawadia wateja na mawakala


Airtel Tanzania inaanza msimu huu wa sikukuu na Airtel Santa Mizawadi promosheni maalum yakutoa shukrani na kuwazadia  wateja na mawakala wote wanaoendelea kutumia huduma za Airtel katika msimu wa sikukuu. Airtel Santa Mizawadi ni promosheni kabambe ambayo itawapa washindi fursa ya kuondoka na zawadi kemkem ikiwemo pocket WiFi, simu janja, pikipiki, runinga na pesa Taslim hadi shilingi milioni moja.

Jinsi ya kushirikina kujishindia Mizawadi ya Airtel Santa Mizawadi, ikiw awewe ni Wakala wa Airtel unatakiwa tu kufanya miamala ya kuweka na kutoa fedha, ambapo pia ili Mteja aweze kuingia kwenye droo anatakiwa tu kufanya miamala kama vile kununua bando, Kutuma pesa,  kutoa pesa, kulipa bili, kufanya miamala ya kibenki, kutuma au kupokea pesa nje ya nchi, kununua muda wa maongezi au vifurushi kupitia *149*99#, *150*60#, au kwa kutumia 'My Airtel App'.

Akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa promosheni hiyo iliyofanyika makao makuu ya Airtel Tanzania jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano, Jackson Mmbando alieleza kuwa Promosheni ya Airtel Santa Mizawadi ni inalenga kuwashukuru wateja na mawakala waaminifu na wanaoendelea kutumia Airtel katika msimu wote huu wa sikukuu.

"Kupitia Promosheni ya Airtel Santa Mizawadi tunasambaza upendo na kunogesha sikukuu kwa wateja na  mawakala wetu wetu ambao wamekuwa na mchango mkubwa katika mafanikio yetu," alisema Mmbando.
Mmbando alisisitiza kuwa Airtel inaendelea kujidhatiti kutoa huduma za kipekee katika msimu wa sikukuu huku akidokeza kuwa kila muamala unaofanyika unatoa nafasi kwa wateja au mawakala kujishindia zawadi zitakazoboresha Maisha yao.

Kwa upande wake Meneja Huduma kwa Wateja Bi Celine Njuju "Airtel tunawadhamini sana wateja wetu, Tusingefika hapa tulipoleo bila ya wateja na mawakala wetu, Airtel Santa Mizawadi  ni promosheni kabambe kwa kuwa itanogesha balozi wetu, mtamuona Mr SANTA wetu akitembele  baadhi ya mitaa yetu kuhakikisha wateja na mawakala wanapata pia zawadi za papo kwa hapo, ikiwa utabahatika kukutana nae basi nakuahidi atanogesha msimu wako  wa sikukuu vizuri ufurahie wewe na  wapendwa wako."

"Kwa kumalizia, washindi wa Airtel Santa Mizawadi watapatikana kupitia Droo za zitakazochezwa kila wiki mara moja ambapo washindi  wote watapigiwa simu kupitia namba maalum ya Airtel 100" alisisitiza Bi Njuju

Kwa taarifa zaidi kuhusiana na promosheni hii, tunawahimiza wateja na mawakala wetu kutembelea tovuti ya Airtel au kuwasiliana na watoa huduma wetu wa Airtel kwa kupiga 100.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...