Na Ahmad Mmow.
Katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma stahiki kutoka katika ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Mwanasheria Mkuu wa Serikali nchini, Hamza Johari ameahidi kutembelea ofisi za kanda za mwanasheria mkuu ili kuimarisha utoaji huduma kwa wananchi.
Mwanasheria Mkuu huyo ametoa ahadi hiyo leo katika manispaa ya Mtwara Mikindani alipokutana na kuzungumza na wadau mbalimbali wa sheria mkoani Mtwara.
Alisema ofisi yake itaendelea kuimarisha utoaji huduma kwa wananchi katika maeneo mbali mbali nchini. Kwahiyo katika ziara hiyo alikutana na watumishi wa ofisi ya Mwanasheria mkuu wa serikali ili kuwasisitiza na kuwakumbusha umuhimu wa kuwahudumia wananchi.
" Kama nikivyosema, tutaendelea kuimarisha utoaji huduma kwa wananchi katika maeneo mbalimbali nchini. Hivyo katika ziara hii tunakutana na watumishi wa ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kusisitizana juu ya kuwahudumia wananchi, " alisema Johari.
Johari amesema mkoa wa Mtwara ni mkubwa na una shughuli nyingi za kiuchumi. Kwahiyo ni vema kuwa na mawasiliano ya karibu kati ya ofisi ya Mwanasheria mkuu na ofisi ya mkuu wa mkoa na wananchi wengine.
Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Mtwara, Patrick Sawala alisema serikali inaendelea kushirikiana na wadau wengine kuhakikisha kwamba wananchi wanaendelea kuwa salama.
Katika ziara hiyo mwanasheria mkuu huyo wa serikali ametembelea eneo linalotarajiwa lujengwa jengo la ofisi ya kanda, pamoja na na ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali mkoa wa Mtwara.