Mwanaume mmoja kutoka Jimbo la Victoria, Australia ambaye alimdanganya Mkewe ili wasafiri pamoja hadi Sudan lakini alipofika huko alichukua Watoto wao na pasipoti ya Mkewe na kumtoroka kurudi Australia akimwacha Mkewe nyuma kwa muda wa miezi 16 amehukumiwa kwenda jela miaka minne.
Mwanaume huyo mwenye umri wa miaka 52 alikamatwa na kufikishwa Mahakamani mapema wiki hii akituhumiwa kwa makosa ya kumshawishi Mkewe kuondoka Australia kinyume na mapenzi yake na kumtelekeza, Hata hivyo, amekana mashitaka hayo na kujitetea akisema kuwa hakumdanganya Mkewe.
Jaji Frank Gucciardo ameeleza kwamba makosa yake yalihusisha mipango ya makusudi, akiongeza kuwa Mtuhumiwa alimtendea Mkewe kitu ambacho sio cha uungwana na kusema kuwa Mwanamke huyo alikuwa na huzuni kubwa na aliathirika kutokana na kuondoka kwa Watoto wake.
Baada ya kukutwa na hatia, Jaji amemhukumu Mwanaume huyo kifungo cha miaka minne na nusu gerezani, katika kesi hiyo, ilibainika kwamba mwanaume huyo alimdanganya Mkewe kuhusu hali yake ya visa, akimfanya afikiri walikuwa na ruhusa ya kurudi Australia, Jaji alisema kwamba kama Mwanamke huyo angejua ukweli kuhusu hali yake ya visa, asingekubali kuondoka Australia.