Monday, September 2, 2024

Mrembo Aliyebaguliwa Miss South Afrika Ashinda Taji Hilo Miss Nigeria


Mrembo Aliyebaguliwa Miss South Afrika Ashinda Taji Hilo Miss Nigeria

Mrembo Aliyebaguliwa Miss South Afrika Ashinda Taji Hilo Miss Nigeria

Chidimma Vanessa Adetshina(@chichi_vanessa), mwanafunzi wa sheria mwenye umri wa miaka 23, ameshinda taji la Miss Universe Nigeria 2024.

Chidimma alizaliwa Afrika Kusini kwa baba wa Kinaijeria na mama mwenye asili ya Msumbiji,, ushindi huu ni muhimu sana kwake--baada ya kujitoa kwenye shindano la Miss South Africa 2024,kutokana na ukosoaji kuhusu uraia wake.

"Ninapokubali heshima hii, nataka kusema maono yanayochoma ndani yangu, maono ya umoja wa Afrika na kuishi kwa amani. Tuvunje vizuizi vinavyotutenganisha.

Tujenge bara ambapo kila Mwafrika anaweza kusafiri bila ubaguzi, kufuata ndoto zao, na kuchangia katika ukuaji na ustawi wa bara letu kubwa," ni sehemu ya ujumbe ambao Chidimma Vanessa Onwe Adetshina ameutoa baada ya kushinda taji la Miss Universe Nigeria.

Vanessa amechukua taji hilo ikiwa ni wiki chache tu baada ya kujiondoa kwenye shindano la Miss South Africa baada ya kubaguliwa kutokana na kuwa na Mzazi raia Nigeria na mama yake kudaiwa kuwa anatokea Msumbiji.

Licha ya kushinda Miss Universe Nigeria, bado, Vanessa ana uraia wa Afrika Kusini


Source
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...