Saturday, July 20, 2024

DC Mpogolo aongoza kikao cha wadau kujadili na kupokea maoni ya dira ya taifa 2025/50


Mkuu wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo leo tarehe 19 Julai 2024, ameongoza kikao cha kamati ya Ushauri Jiji la Dar es salaam na wadau wa Maendeleo kutoka Makundi mbalimbali, kutoa maoni yao kuhusu uundwaji wa Dira ya maendeleo ya Taifa ya mwaka 2050.

Akizungumza katika Kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa arnatouglo Jijini humo mhe mpogolo amewasihi wadau hao kuwa maoni yao ni muhimu kwa mustakabali wa maendeleo ya wananchi wa wilaya ya Ilala pamoja na Taifa kwa ujumla na kwamba mapendekezo hayo yatachukuliwa kwa uzito wake na kufikishwa ngazi za juu.

"Nawashukuru kwa ushiriki wenu hasa viongozi wa vyama vya Siasa pamoja na wadau wote ,hii inadhihirisha nia njema ya dhati tulionayo wote kwa Pamoja juu ya Maendeleo ya Taifa letu, mkumbuke miaka 25 iliyopita Wilaya ya Ilala haikua na miundombinu kama ilivyo sasa hata kwenye miundombinu ya Elimu tunalazimika kujenga majengo ya ghorofa, hivyo miaka 25 ijayo hali itakua tofauti" alisema Mpogolo

Mratibu wa kikao hicho cha kukusanya maoni ya dira ya maendeleo ya taifa 2050 Mposi Gwasisa amesema Dira ya miaka 25 iliyopita ililenga zaidi katika maisha bora , amani na utulivu na Jamii iliyoelemika na kujifunza.

Aidha amesema Dira ya maendeleo ya taifa ya mwaka 2050 inatambua kuwa maendeleo ya Tanzania yanaletwa na watanzania wenyewe ndomaana wanakusanya maoni na ushauri kutoka kwa wanajamii ili kupata nguzo zitakazoongoza kwa kipindi cha miaka





 

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...