Sasa rasmi wanafunzi wanaopata mimba Tanzania kurejea masomoni kwenye mfumo rasmi
Juni 2017 hayati Rais Magufuli alipiga marufuku wanafunzi wanaopata mimba kuendelea na masomo ya shule ya msingi na sekondari akisema ndani ya utawala wake hakuna mwanafunzi atakayepata mimba na kuruhusiwa kurudi shuleni.