Wednesday, August 11, 2021

RC Tabora ahimiz uwekezaji katika ufugaji nyuki


WAKAZI wa Mkoa wa Tabora wamehimizwa kuwekeza katika ufugaji wa kisasa wa nyuki kwa ajili ya kuongeza uzalishaji wa asali

Kauli hiyo imetolewa leo na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Buriani wakati alikuwa akizindua Mabaraza ya Biashara ya Wilaya ya Kaliua na Urambo.

Asali ni mojawao wa bidhaa ambayo inaweza kuwaondoa wakazi katika umaskini na kuendelea kuutangaza Mkoa wa Tabora ndani na nje ya Nchi .

Balozi Dkt. Batilda alisema hivi sasa ufugaji wa nyuki katika Mkoa wa Tabora bado unatumia mizinga ya asili ambayo uzalishaji wake wa asali ni kidogo ambapo ni wa wastani wa kilo 9 kwa kila mzinga.

Alisema wakazi wa Tabora wakikubali kubadili teknolojia ya kizamamani na kutumia mizinga ya kisasa watapata wastani kilo 20 hadi 25 kwa mzinga mmoja.

Balozi Dkt. Batilda alisema hivi Mkoa huo unawastani wa mizinga laki nne ambapo kati ya hiyo 40,000 ndiyo ya kisasa.

Alisema Mkoa wa Tabora unatakiwa kutumia fursa iliyopo ya miti ya miombo kuongeza idadi ya mizinga ya kisasa kwa ajili ya kuongeza uzalishaji wa asali.

Balozi Dkt. Batilda alisema tayari uongozi wa Mkoa umeshafanya juhudi ya kukutana na TAWA ili kuomba kibali cha kuwaruhusu wafugaji wa nyuki kutumia mapori yao

Katika nyingine Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda amewataka wakulima kuendesha kilimo ambacho ni rafiki wa mazingira na uoto wa asili.

Alisema hatua itawezesha nyuki kuendelea kuwa na malighafi ambazo zinatumiwa katika utengenezaji wa asali.

Balozi Dkt. Batilda aliongeza kuwa sanjari na hilo ni vema Kila Halmashauri Mkoa huo ikaanzia zoezi la kuwa na mistu yake na elimu hiyo waipeleke hadi ngazi za familia.

 

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...