Kamanda wa Polisi Mkoa Arusha ACP Justine Masejo
Na Malunde 1 blog - Arusha
Hatimaye Jeshi la Polisi limekiri kukamatwa kwa mtuhumiwa anayedaiwa kuingia katika nyumba za watu katika eneo la Murieti na kuwabaka wasichana kisha kuondoka na nguo za ndani.
Kwa mujibu Mwenyekiti wa mtaa Murieti Dominick Kivuyi amesema kijana huyo Mnene mweupe alikamatwa akiwa na mafuta ambayo hutumia kujipaka asikamatwe, kifimbo chenye ushanga na alikamatwa akiwa uchi katika eneo la balozi Nuru pia akiwa na bisibisi ambayo huwachoma wanawake baada ya kuwabaka na kuondoka na nguo zao za ndani.
Mara baada ya taarifa za kukamatwa kwa 'teleza' huyo, leo asubuhi mamia ya Wakazi wa Kata ya Murieti waliofurika kituo cha polisi Murieti wakitaka kumuona mtuhumiwa huyo anayedaiwa kuwafanyia ukatili wanawake.
Kamanda wa Polisi Mkoa Arusha ACP Justine Masejo, amesema mtuhumiwa huyo amekamatwa leo Jumatano, Agosti 10, 2021 saa tisa usiku baada ya msako mkali uliofanyika katika eneo la Murieti na Kwa Mrombo jijini Arusha.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha amesema kuwa mnamo tarehe 07/08/2021 muda wa saa 06:05 Mchana maeneo ya Morombo jiji la Arusha ulifanyika mkutano wa ulinzi shirikishi na usalama katika eneo la Muriet ambalo lilihusisha wananchi na vikundi vya ulinzi shirikishi pamoja na wawakilishi wa Wilaya ya Kipolisi Muriet,
"Katika kikao hicho kulijitokeza taarifa za kuwepo mtu mmoja asiyefahamika na anayeingia katika nyumba zao nyakati za usiku na mara baada ya kuingia hutokea dirishani ambapo hizo taarifa hizo hazikuwahi kuripotiwa Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha mpaka zilipotolewa katika kikao hicho cha ulinzi shirikishi",amesema.
Amesema baada ya kupata taarifa hizo Jeshi la Polisi Mkoani Arusha lilianza uchunguzi wa kina kwa kushirikiana na vikundi vya ulinzi shirikishi na timu ya makachero kuhusiana na taarifa hizo ambapo siku ya leo tarehe 10.08.2021 muda wa saa 09:00 alfajiri Jeshi la Polisi lilifanikiwa kumkamata mtu mmoja jina limehifadhiwa huko maeneo ya kwa Morombo akiwa katika mazingira ya kutatanisha.
Kamanda Masejo amesema kuwa Jeshi la Polisi Mkoani Arusha linaendelea na uchunguzi wa taarifa hiyo ambayo ilitolewa katika kikao hicho kilichofanyika siku ya Jumamosi.
ACP Masejo ametoa wito kwa wananchi kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu ili kukomesha uhalifu, Pia ametoawito kwa waandishi wa habari kuhakikisha wanatoa taarifa ambazo zimedhibitishwa na jeshi la Polisi ili kutokuleta taharuki kwa jamii na Mkoa mzima kwa ujuml