Sunday, August 1, 2021

Msigwa: ''Tanzania itapata chanjo asilimia 60''

Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Ndg. Gerson Msigwa amesema Serikali imejiwekea mkakati wa angalau kupata chanjo asilimia 60 ili kuhakikisha inapambana na ugonjwa wa Uviko-19.

Msigwa ameyasema hayo leo Agosti 1, 2021 kwenye mkutano wake na wanahabari ambapo amesisitiza kuwa chanjo bado ni hiari na kesho Agosti 2, 2021 zitaanza kutolewa nchi nzima kwenye zaidi ya vituo 550.

''Rais Samia Suluhu anafanya kazi kubwa sana kuhakikisha Tanzania inapata chanjo nyingi iwezekanavyo, kwasababu nchi yetu imejiwekea tupate chanjo asilimia kama 60 hivi ambapo tutakuwa tumejihakikishia kukata maambukizi ya ugonjwa huu wa Uviko-19'', amesema Gerson Msigwa, Msemaji Mkuu wa Serikali.

Ameongeza kuwa, ''Zoezi la chanjo litaanza kutolewa kesho kuna vituo kama 550 vilivyoandaliwa, chanjo hizi hazijaleta madhara kwa waliotumia kama tulivyokuwa tunasikia na chanjo hizi zitaendelea kuletwa baada ya zile dozi milioni 1 kuna nyingine zitaendelea kuletwa.''

Aidha amefafanua kuwa, ''Nchi zote zitasaidiwa chanjo kwa idadi ya asilimia 20 ya watu wake, kwahiyo Tanzania kupitia mpango huu tutapata takribani chanjo milioni 11, kwahiyo zilizokuja hizi zaidi ya milioni 1 ni sehemu ya mpango wa COVAX Facility chini ya WHO.'' 

 

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...