Waandaaji wa mashindnao ya Olimpiki ya Tokyo wataruhusu wanamichezo ambao wananyonyesha watoto kwenda na watoto wao wachanga kwenye Michezo hiyo mwezi ujao.
Msemaji wa IOC alisema Jumatano, akibadilisha msimamo ambao ulikuwa umezua maombi mengi ya wanamichezo kutakiwa kuruhusiwa kwenda na watoto wao na maafisa wa afya ya umma kulalamika vikali Kamati ya Tokyo 2020, ambayo inaratibu sera ya Michezo hiyo.
Serikali ya Japan, ilithibitisha mabadiliko hayo katika taarifa Jumatano usiku, ikisema, "Baada ya kuzingatia kwa uangalifu hali ya kipekee inayowakabili wanamichezo walio na watoto tunayo furaha kuthibitisha kwamba, inapobidi, watoto wachanga wataweza kuandamana na wanariadha kwenda Japan.
"Wakati huo huo Bondia aliyekosa kufuzu kwa mashindano ya Olimpiki kwa sababu alikuwa mjamzito ameshinda moja ya mapigano yake makubwa – kushiriki kwenye Michezo ya Tokyo msimu huu.
Mandy Bujold, bingwa wa Canada mara 11, atakuwa Japan baada ya mahakama ya Usuluhishi wa mizozo ya Michezo (Cas) kutoa uamuzi uliokuwa na faida kwake.
Bujold alipata dhahabu kwenye mchujo wa Canada mnamo Desemba 2019 na alionekana kuelekea kushiriki kwenye Olimpiki yake ya pili, lakini hafla ya mwisho ya kufuzu kwa nchi za Amerika mapema mwaka huu zilifutiliwa mbali kwa sababu ya janga la Corona