Monday, July 26, 2021
NIDA Textile Industries yakumbana na rungu la Waziri Jafo, Wapewa Siku 45
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano na Mazingira Mh. Selemani Jafo ametoa siku 45 kwa Kiwanda cha kutengeneza nguo cha NIDA Textile Industries kuhakikisha kimepata kibali cha kutiririsha maji ambayo yanaingia katika Mto ulioko katika eneo hilo, kutoka katika Mamlaka ya Bonde Mto Wami- Ruvu kinachothibitisha ubora wa maji wanayotiririsha ni salama kwa Mazingira na hayana athari yoyote kwa mazingira.
Ametoa agizo hilo Mkoani Dar es Salaam alipotembelea kiwanda hiko kilichopo katika eneo la Tabata katika Manispaa ya Ubungo alipokua katika ziara yake ya siku moja na kubaini hakuna kibali cha kutiririsha maji ambacho ni muhimu kwa sababu Kiwanda hiko kina mfumo wa kutiririsha maji taka kwahiyo kinatakiwa kuwa na kibali hiko .
"Ninatoa siku 45 ikiwa na maana ya mwezi mmoja na nusu muwe mmeshapata kibali kutoka Mamlaka ya Bonde kuhusiana na maji taka mnayotiririsha kama ni salama au la mana maji haya hayaonyeshi kwa macho maji haya ni salama kwa mazingira na viumbe hai" Waziri Jafo
Aidha Waziri Jafo alitembelea kiwanda cha kutengeneza sabuni cha Royal Soap and Detergents kilichopo Kata ya Mabibo katika Manispaa ya Ubungo kujionea changamoto za uchafuzi wa mazingira katika eneo hilo ambazo zimekua zikilalamikiwa kwa muda mrefu na Wananchi wa eneo hilo la Kata ya Mabibo ikiwemo hewa chafu inayotoka kiwandani hapo .
Akiwa Kiwandani hapo alisikiliza pande zote yani Upande wa Kiwanda na Wananchi ambapo waliwakilishwa na Diwani wa Kata hiyo Mh. Joseph Kleruu na hatimaye alitoa maagizo kuwa ameona kuna changamoto ya Kimahusiano kati ya Wananchi wa eneo hilo na mwenye Kiwanda hivyo ameagiza kifanyike kikao kati ya mwenye Kiwanda, Afisa Mazingira wa Manispaa pamoja Diwani na Mwenyekiti wa Mtaa huo ambao ni Wawakilishi wa Wananchi kwa pamoja wafikie makubaliano halafu taarifa ya Makubaliano hayo iende kwa Mkuu wa Wilaya ya Manispaa ya Ubungo .
'Nimeona kuna changamoto ya kimahusiano katika eneo hili tafadhali wekeni mahusiano mazuri na Wananchi wanaowazunguka hiyo ni muhimu sana naagiza mfanye kikao ndani ya wiki mbili kupata ufumbuzi wa suala hili na ndani ya miezi sita tutakuja tena kujionea katika suala la mazingira utekelezaji wa makubaliano hayo umefanyika au la " Waziri Jafo
Akiongea baada ya kupokea maagizo hayo Mkuu wa Wilaya Manispaa ya Ubungo Mh. Kheri James alimuhahikishia Waziri Jafo kupokea maagizo hayo na atayafanyia kazi na taarifa ya makubaliano itapelekwa Ofisini kwa Waziri kama alivyoagiza.
Naye Meneja wa Uendeshaji wa Kiwanda hiko Ntula Shalanda amemuahidi Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano na Mazingira Mh. Selemani Jafo kupokea maagizo hayo na kuyafanyia kazi na watakutana na Wawakilishi hao wa Wananchi kama alivyoagiza.
Katika ziara hiyo Waziri Jafo aliambatana na Mkuu wa Wilaya wa Manispaa ya Ubungo Kheri James pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Manispaa ya Ubungo na Wataalamu wa Mazingira kutoka NEMC na Manispaa ya Ubungo.
-
Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga Daktari Daniel Henry Na Isaac Masengwa ******************* Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga...
-
WATU saba wamefariki dunia baada ya bajaji waliyokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na lori eneo la Mpemba, Tunduma wilayani Momba, mk...
-
Rais Uhuru Kenyatta na viongozi wengine nchini Kenya wametuma salamu zao za rambi rambi kwa familia ya marehemu Yusuf Haji. Rais Uhuru Kenya...
-
MWANA-mfalme wa Uingereza,. Prince Charles, ambaye ni mtoto wa kwanza wa Malkia Elizabeth wa Pili wa Uingereza, na mrithi wa kwanza katika ...
-
Mfanyabiashara raia wa Kenya, Raphael Ongangi anayedaiwa kutekwa na watu wasiojulikana maeneo ya Oysterbay, Dar es Salaam nchini Tanzania am...
-
Mbunge wa Kigoma Mjini na Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe asomewa mashtaka matatu ya uchochezi, yenye nia ya kuleta ch...
-
Zikiwa zimesalia siku chache tu Hoteli Mpya ya Kisasa yenye Ubora wa hali ya juu 'SHY PARK HOTEL' ifunguliwe Rasmi mwezi Agosti 202...
-
Vijana wametakiwa kuwa wazalendo katika nchi yao kwa kukemea vitendo viovu katika jamii na kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu. Aidha Sil...
-
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko amefunga rasmi mafunzo ya sheria za usalama barabarani kwa maaskofu na wachungaji wa makanisa ya...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
