Friday, July 2, 2021

Jeshi laitwa kusitisha uporaji Eswatini


Serikali ya Eswatini imeamuru jeshi la nchi hiyo kurejesha utulivu baada ya siku kadhaa za maandamnao ya vurugu yanayoshinikiza mageuzi ya kidemokrasia kwenye taifa hilo la kifalme kusini mwa Afrika.

Kaimu waziri mkuu, Themba Masuku, amesema ingawa wanaheshimu haki ya watu kuandamana lakini hawataruhusu kile alichokitaja kuwa mashambulizi dhidi ya watu na uporaji mali unaofanywa na waandamanaji.

Masuku amesema serikali imeamuru jeshi kurejesha utulivu, kulinda miundombinu muhimu pamoja na kusimamia utekelezaji wa kanuni za kukabiliana na kusambaa kwa virusi vya corona ambazo zinakiukwa na waandamanaji.

Wakati huo huo, taifa jirani la Afrika Kusini limesema linafuatilia kwa karibu hali inayoendelea nchini Eswatini na kuitolea mwito serikali kujizuia kutumia nguvu dhidi ya waandamanaji.

Wafuasi wa upinzani nchini humo wanamlaumu Mfalme Mswati wa III kwa kuendesha nchi hiyo kwa mabavu pamoja na matumizi mabaya ya fedha za umma.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...