Wednesday, June 16, 2021

Wadau na Serikali simamieni haki za watoto

 



Na Maridhia Ngemela, Mwanza.

Mkurugenzi wa shirika la Wote sawa amewaomba wadau mbalimbali kwa kushirikiana na Serikali kuendelea kulinda haki za watoto ili wafikie malengo yao.

shirika lisilo la kiserikali la Wote Sawa linalojishughulusha na kutetea haki za mfanyakazi wa nyumbani na kupinga usafirishaji haramu  wa binadamu Angela Benedicto ameiomba Serikali na wadau kuendelea kutekeleza na kusimamia sheria na miongozo iliyopo nchi ili waweze kumlinda mtoto wa kike.


Hayo yamesemwa leo kwenye madhimisho ya siku ya mtoto wa afrika yaliyofika katika  uwanja wa furahisha uliopo wilayani Ilemela mkoani Mwanza.

Alisema ni  vema Tanzania  kusimamia mikataba na makubaliano ya kimataifa ambayo yamewekwa katika ulinzi wa mtoto na jamii.

"Jamii kwa ujumla inapaswa kuhakikisha inamlinda mtoto kwa kupaza sauti pindi anapoona anafanyiwa vitendo vya ukatili ili  hatua kali zichukuliwe na iwefundisho kwa watu wengine wenye tabia hizo za kunnyanyasa watoto.

"Masuala haya yanapofika  katika ngazi ya mahakama waweze kutoa hukumu kwa wakati ilikupata haki .

kwa sababu tumeona Watoto wengi wanafanyiwa  vitendo hivi lakini mashatika yanaenda taratibu na kupelekea watu kukata tamaa.

"Haki ya elimu iendelee kuzingatiwa kwa sababu ni bure kwani kuna baadhi ya  wazazi na walezi wamekuwa chanzo cha kutowapeleka watoto wao shule waweze kuchukuliwa hatua za kisheria ili wapate  haki ya elimu.

"Leo hii tunaadhimisha siku ya mtoto wa afrika lakini pia ni Siku ambayo tunakumbukia shirika la kazi duniani  pamoja na wanachama wake chini Geniva lilisaini mkataba wa wafanyekazi  za staha kwa wafanyakazi wa nyambani.

"Tunaendelea kuhamasisha wananchi kulinda haki za mfanyakazi wa nyumbani ili asitendewe ukatili wa aina yoyote na kama amekosewa o ni Siku ya mtoto wa afrika na mfanyakazi wa nyumbani.

 "Tunaiomba serikali  iweze kulidhia mkataba wa kimataifa wa haki za wafanya kazi wa ndani kwani tangu mwaka 2011 ni miaka mingi imepita lakini  bado haujalidhiwa tunaomba  ulidhiwe kwa sababu ni daraja kubwa kwa wadau na wafanyakazi ili waweze kupata stahiki zao na haki za msingi ili iwe na staha na kuwa mkombozi kwao",alisema Angela.

Alisema shirika hilo tangu mwaka  2012,limeoko watoto 600 waliofanyiwa  vitendo vya ukatili na kuwarudisha  kwao  kwani pamoja na jitihada nyingi za serika kuhusu kulinda haki za watoto lakini bado kuna changamoto mbalimbali ambazo zinatakiwa zitatuliwe kisheria.

Naye Meneja wa Shirika la Sos children Village Mwanza Dorothy Ndege alisema wanafanya kazi Kwa ukaribu na serikali kwenye miradi yao kwani  kwa nusu mwaka  wametumia zaidi ya  Sh million 100 kwa ajili ya miradi ya elimu na afya  ili kupunguza changamoto zinazowakabili watoto na kupunguza kwa watoa huduma ili kuweza kuhakikisha wanapewa haki zao na kulindwa.

Alisema  pamoja na hujudi zinazofanywa na asasi mbalimbali  lakini watoto  hao wanatakiwa  kupaza sauti zao  ili waweze kujilinda wenyewe na kuacha kusubilia kulindwa  ili kuhakikisha wanafikia ndoto zao.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya  Ilemela Dk Severini Lalika  alipokuwa akizungumza  kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Mwanza,Robert Gabliel ameitaka jamii kufichua  wazazi na walezi wanaotenda vitendo vya ukatili  kwa watoto wao .

Sanjari na kuacha usafirishaji haramu wa watoto kwani kufanya hivyo ni kosa.

Maadhimisho hayo  yaliyoambatana  na kaulimbiu isemayo  tutekeleze agenda 2040 kwa Afrika inayolinda haki za watoto.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...