Thursday, June 10, 2021
Serikali Kuzindua Makao Ya Taifa Ya Watoto Waishio Mazingira Hatarishi
Na Mwandishi Wetu, Dodoma
Kuelekea Siku ya Mtoto wa Afrika, Serikali inatarajia kuzindua Makao ya Taifa ya Malezi na Makuzi ya Watoto yaliyojengwa katika Kata ya Kikombo, jijini Dodoma.
Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dodoma, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia ,Wazee na Watoto, Dkt Dorothy Gwajima amesema Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Isdor Mpango atazindua makao hayo wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika yatakayofanyika tarehe 16 mwezi huu.
Dkt. Gwajima amesema lengo la kujengwa kwa makao hayo ni kutatua changamoto za makao ya Taifa ya awali yaliyokuwa Kurasini Dar es Salaam za ufinyu wa maeneo ya shughuli mbalimbali ikiwemo michezo, bustani, ujasiriamali na ufugaji kutofanyika sawasawa hivyo kufanya hali ya lishe na uchumi kuwa duni.
" Ujenzi huu ni sehemu ya utekelezaji wa mpango wa Taifa wa Kimkakati wa kuwatambua, kutengamanisha na kuwaunganisha na familia watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi, pia ni utekelezaji wa maagizo ya Mhe. Rais kuwa watoto wanaotunzwa kwenye makao waandaliwe mapema kadri inavyowezekana kuwaunganisha na familia ili kuwawekea msingi wa malezi" alisema Dkt. Gwajima.
Ameongeza pia watoto wanatakiwa kukaa kwenye makao kwa muda tu na wakiisha kuimarika warejeshwe kwenye makazi ya kawaida iwe ya kambo au kuasili ili waishi kawaida katika familia.
Dkt. Gwajima amesema, uzinduzi huo utaambatana na uzinduzi wa vituo vya Jamii vya malezi, Makuzi na Maendeleo ya awali ya watoto pamoja na Baraza la Taifa la Watoto hapo tarehe 14 mwezi huu.
Aidha, Dkt. Gwajima ametoa rai kwa wazazi na jamii kwa ujumla kuhakikisha wanatimiza jukumu la malezi ya watoto wao na kuwa, hatua ya kulelewa katika makao iwe ni ya mwisho baada ya hatua zote kushindikana.
Mradi wa Ujenzi wa Makao ya Watoto Kikombo, umetekelezwa kwa Ushirikiano kati ya Serikali kupitia Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto na Shirika la ABBOT Fund Tanzania na Makao hayo yana uwezo wa kuhudumia watoto 250 kwa wakati mmoja na hadi sasa watoto wanaohudumiwa katika Makao hayo ni 28.
Mwisho.
-
Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga Daktari Daniel Henry Na Isaac Masengwa ******************* Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga...
-
WATU saba wamefariki dunia baada ya bajaji waliyokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na lori eneo la Mpemba, Tunduma wilayani Momba, mk...
-
Rais Uhuru Kenyatta na viongozi wengine nchini Kenya wametuma salamu zao za rambi rambi kwa familia ya marehemu Yusuf Haji. Rais Uhuru Kenya...
-
MWANA-mfalme wa Uingereza,. Prince Charles, ambaye ni mtoto wa kwanza wa Malkia Elizabeth wa Pili wa Uingereza, na mrithi wa kwanza katika ...
-
Mfanyabiashara raia wa Kenya, Raphael Ongangi anayedaiwa kutekwa na watu wasiojulikana maeneo ya Oysterbay, Dar es Salaam nchini Tanzania am...
-
Zikiwa zimesalia siku chache tu Hoteli Mpya ya Kisasa yenye Ubora wa hali ya juu 'SHY PARK HOTEL' ifunguliwe Rasmi mwezi Agosti 202...
-
Vijana wametakiwa kuwa wazalendo katika nchi yao kwa kukemea vitendo viovu katika jamii na kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu. Aidha Sil...
-
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko amefunga rasmi mafunzo ya sheria za usalama barabarani kwa maaskofu na wachungaji wa makanisa ya...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Mbunge wa Kigoma Mjini na Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe asomewa mashtaka matatu ya uchochezi, yenye nia ya kuleta ch...