Saturday, June 12, 2021

Rais Samia kuzindua miradi mikubwa mitatu


Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhandisi Robert Gabriel, amesema Rais Samia Suluhu Hassan, anatarajiwa kuwasili mkoani humo Juni 13, mwaka huu kwa ziara ya siku tatu.

Amesema katika ziara hiyo, Rais atazindua miradi mitatu ya kimkakati ambayo ni Kiwanda cha kusafisha dhahabu, Jengo la Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Kanda ya Ziwa na Mradi mkubwa wa Maji Wilayani Misungwi.

Kadhalika, amesema Rais ataweka jiwe la msingi katika ujenzi wa Reli ya kisasa ya kiwango cha Kimataifa (SGR), kipande cha Fela Isaka na kukagua ujenzi wa mradi wa daraja la John Magufuli.

"Rais atahitimisha ziara hiyo kwa kuzungumza na vijana wa Mkoa wa Mwanza kwa niaba ya vijana wote Nchini katika Uwanja wa Mpira wa Nyamagana," Mkuu huyo wa Mkoa.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...