Saturday, June 12, 2021

Amber Lulu achezea kichapo kutoka kwa mzazi mwenzake


Msanii wa muziki wa bongo Amber Lulu amefunguka ukweli kuhusu kupigwa na mzazi mwenziye na kusema kuwa ataki kumuacha mwanaye akiwa mdogo sababu ya kipigo.

Ambe amesema kuwa mzazi mwenzake uwa anapenda kupiga na alianza kumpiga toka akiwa mjamzito na akatoa sababu iliyofanya ampige siku mbili hizi ni baada ya kumwambia kwa sasa watulie ili wamlee mtoto wao vizuri.

 "Nimepigwa na Baba Wa Mtoto wangu ,Kosa langu ni kumwambia tumuangalie Mtoto tutulie lakini ananiona si lolote haoni hata huruma ninavyohangaika" alisema Amberlulu

Aliendelea kusema "Wakati ni Mjamzito alikuwa ananipiga sana ila nilivumilia kumlinda Mwanangu'' 
'Mama amesema niachane nae kwasababu ameshindwa kutambua umuhimu wangu ,Hajivunii familia yake na ndio umekuwa ni mchezo wake wa kila siku kunipiga'' Amber lulu.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...