Thursday, June 17, 2021

Kim Jong-un akiri kuna 'uhaba' wa chakula Korea Kaskazini

 

Rais wa Korea Kaskazini Kim Jong-un mekiri rasmi kuwa nchi hiyo inakabiliwa na uhaba wa chakula.

Akiwahutubia maafisa wa ngazi ya juu nchini humo, Bw. Kim alisema "hali ya chakula majumbani mwa watu kwa sasa ni ya kutia wasiwasi".

Alisema sekta ya kilimo imeshindwa kufikia malengo yake kutokana na tufani ya mwaka jana iliyosababisha mafuriko.

Kuna ripoti kwamba bei ya chakula imepanda, huku shirika la habari la Korea Kaskazini likiripoti kilo moja ya ndizi inagharimu dola 45 za Kimarekani.

Korea Kaskazini imefunga mipaka yake ili kudhibiti kuenea kwa virusi vya Covid-19.

Bishara kati yake na China imeporomoka sana kutokana na hatua hiyot. Korea Kaskazini inategemea China kwa chakula, mbolea na mafuta.

Korea Kaskazini pia inajitahidi chini ya vikwazo vya kimataifa, vilivyowekwa kwa sababu ya mipango yake ya nyuklia.

Kiongozi huyo wa kimabavu wa serikali ya chama kimoja alizungumzia hali ya chakula katika mkutano wa kamati kuu ya Chama cha Wafanyikazi ambayo ilianza wiki hii katika mji mkuu Pyongyang.

Hadi kufikia sasa, Korea kaskazini inadai kuwa kufunga mipaka yake kumefanya waepuke ugonjwa wa virusi vya corona, ingawa wachambuzi wanatilia mashaka dai hili.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...