Katika jimbo la Kwara nchini Nigeria, watu 10 wameripotiwa kupoteza maisha baada ya kutumia dawa bandia za mitishamba.
Msemaji wa Idara ya Polisi ya Kwara Ajayi Okasanmi, alitangaza kuwa watu 10 kutoka familia moja walifariki baada ya kutumia dawa bandia ya mitishamba, ambazo zinadaiwa kuwa tiba ya maambukizi ya miguu katika eneo la Gwanara.
Akibainisha kwamba wafanyikazi wa matibabu walipelekwa katika mamlaka ya jimbo, Okasanmi alitangaza kuwa uchunguzi ulianzishwa kuhusu tukio hilo.
Okasanmi pia aliwataka umma kujiepusha na vinywaji na madawa ya aina hiyo.