Wednesday, June 30, 2021

SEKTA YA MIFUGO INA MCHANGO MKUBWA KATIKA KUKUZA UCHUMI WA NCHI-PROF.OLE GABRIE

 

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Mifugo Prof. Elisante Ole Gabriel akizungumza wakati wa hafla ya kuwapatia vyeti wauza wa pembejeo sita waliochaguliwa kushiriki katika kutoa huduma za ugani kwa wafugaji walioko maeneo ya Dar es Salaa, Pwani, Morogoro na Tanga.

Mratibu wa Mradi wa AgResults Tanzania Dairly Productivity Challenge Bi.Neema Mrema akizungumza wakati wa hafla ya kuwapatia vyeti wauza wa pembejeo sita waliochaguliwa kushiriki katika kutoa huduma za ugani kwa wafugaji walioko maeneo ya Dar es Salaa, Pwani, Morogoro na Tanga.

Mshirika wa Price Water house Cooper (PwC), Bw.Nelson Msuya wakati wa hafla ya kuwapatia vyeti wauza wa pembejeo sita waliochaguliwa kushiriki katika kutoa huduma za ugani kwa wafugaji walioko maeneo ya Dar es Salaa, Pwani, Morogoro na Tanga.

Mkurugenzi wa Uzalishaji na Masoko wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Bw.Steve Michael wakati wa hafla ya kuwapatia vyeti wauza wa pembejeo sita waliochaguliwa kushiriki katika kutoa huduma za ugani kwa wafugaji walioko maeneo ya Dar es Salaa, Pwani, Morogoro na Tanga.

Wadau mbalimbali wa sekta ya mifugo nchiniwakifuatilia hafla ya kuwapatia vyeti wauza wa pembejeo sita waliochaguliwa kushiriki katika kutoa huduma za ugani kwa wafugaji walioko maeneo ya Dar es Salaa, Pwani, Morogoro na Tanga.

Wauza pembejeo waliochaguliwa kushiriki katika kutoa huduma za ugani kwa wafugaji walioko maeneo ya Dar es Salaam, Pwani, Morogoro na Tanga wakipatiwa vyeti mara baada ya kufanya vizuri katika sekta hiyo.Zoezi la utoaji vyeti limefanyika leo Jijini Dar es Salaam.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

*********************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

Sekta ya mifugo sasa inachangia uchumi wa nchi zaidi ya asilimia 7.4% na mwaka huu wa fedha unaoisha, sekta hii inakuwa kwa asilimia 5% lengo likiwa kufikia mara mbili kwenye mchango wa uchumi na kuweza kufikia angalau asilimia 15 ifikapo mwaka 2025.

Ameyasema hayo leo Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Mifugo Prof. Elisante Ole Gabriel wakati wa hafla ya kuwapatia vyeti wauzaji wa pembejeo sita waliochaguliwa kushiriki katika kutoa huduma za ugani kwa wafugaji walioko maeneo ya Dar es Salaa, Pwani, Morogoro na Tanga.

Amesema uzalishaji wa maziwa nchini umefikia bilioni 3.4 ikiwa maziwa yanayosindikwa ni lita milioni 75 hii inamaana inaleta wawekezaji wengi kuja kuchakata na kuleta thamani kwasababu wateja wananunua maziwa ambayo yameongezwa thamani .

"Takwimu zinaonesha katika lita bilioni 3.4 maziwa yanayotka kwenye ng'ombe wa kienyeji ni lita bilioni 2.38 kwahiyo lita bilioni 1.2 tu zinaonesha zinatokana na ng'ombe wa maziwa". Amesema Prof. Ole Gabriel.

Aidha amesema Tanzania ni nchi ya pili kwa wingi wa mifugo barani Afrika ambapo inazaidi ya ng'ombe milioni 33.9 na mbuzi wameshafika zaidi ya milioni 22 wakati kondoo wamefika takribani milioni 6, kuku wamefikia milioni 87.7.

Kwa upande wake Mratibu wa Mradi wa AgResults Tanzania Dairly Productivity Challenge Bi.Neema Mrema amesema kuwa kupitia mradi huo wana matokeo mazuri wameyaona ambapo kuna ng'ombe 558 tayari wana mimba na wengine tayari wameshapata watoto pia kuna ng'ombe 336 ambao wameogeshwa kitaalamu na vilevile kuna ng'ombe 62 ambao hao wamepata chanjo kuanzia mbili na kuendelea.

"Wauza pembejeo hawa wameweza kuwafikia wafugaji 2776 na kuuza pembejeo nne ambazo ni vidhibiti vimelea, Chanjo, lishe uhimilishaji pia mpaka sasa tuna ng'ombe 17,000 ambao wamepata huduma mbalimbali za lishe katika kuongeza afya bora na pia kuweza kupata maziwa yaliyobora". Amesema Bi.Mrema.

Amesema kuwa mradi huo una malengo matatu ambapo lengo la kwanza ni kuongeza uzalishaji na tija ya maziwa kwa wafugaji wadogowadogo, kuongeza kipato kwa wafugaji wadogowadogo wa maziwa, kuleta uwiano sahihi na kuboresha mifumo ya uendeshaji wa shughuli katika sekta ya maziwa .

Hata hivyo Bi.Mrema amesema washiriki sita wa mradi huo kutoka sekta binafsi wamepata tuzo na motisha ya dola za kimarekani 27,000 kwa pembejeo 4116 zilizokamilika ili waweze kuendelea kutoa huduma na kuongeza uzalishaji wa maziwa na kukidhi soko la Tanzania.


DC Godwin Gondwe afanya ziara ya kushtukiza katika soko jipya la Magomeni

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Godwin Gondwe leo amefanya ziara ya kushtukiza katika soko jipya la Magomeni ambapo amezunguka kwenye soko hilo na kusikiliza kero za Wafanyabiashara walioingia ndani ya soko na kisha kuahidi kuzifanyia kazi.

Kero kubwa aliyokutana nayo DC Gondwe ni kutoka kwa Wafanyabiashara wanaouza bidhaa zao nje ya soko ambapo ameahidi kutolea tamko suala hilo.

 

Majaliwa: Wizara Kilimo Simamieni Kilimo Cha Ngano Na Zabibu


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameiagiza Wizara ya Kilimo isimamie upatikanaji wa mbegu bora katika kilimo cha ngano na zabibu pamoja na kuweka mpango mzuri utakaosimamia na kuendeleza kilimo cha mazao hayo .

 "…Utoaji wa vibali kwa wanunuzi wa ngano na mchuzi wa zabibu ufanywe kwa kuzingatia wale ambao watathibitisha kununua malighafi hizo ndani kwanza. Hakikisheni mnasimamia vizuri makubaliano kati ya wakulima na wanunuzi wakubwa ili tusinunue bidhaa hizo kutoka nje."

Ameyasema hayo leo (Jumatano, Juni 30, 2021) wakati akiahirisha mkutano wa tatu wa Bunge la 12, Bungeni jijini Dodoma. Bunge limeahirishwa hadi Agosti 31 mwaka huu.

Akizungumzia kuhusu fursa mpya ya kilimo cha soya, Waziri Mkuu ameiagiza Wizara ya Kilimo ihakikishe inakuwa na mpango mzuri wa kuendeleza kilimo hicho kwa kuwapatia wakulima mbegu kwa kuanza na mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma.

Kadhalika, Waziri Mkuu amezungumzia kuhusu masoko ya mazao ambapo kwa upande wa tumbaku, ameiagiza Wizara ya Kilimo ishirikiane na Wizara ya Fedha na Mipango kukamilisha mazungumzo na wanunuzi wa zao hilo hususan kipindi hiki ambacho bei yake inaonekana kuimarika kwenye soko la dunia.

"Pia nafahamu kuwa tayari tupo kwenye msimu wa pamba. Ninasisitiza kuwa wakulima wa pamba wasikatwe gharama za pembejeo kwa kuwa tayari zipo kwenye mjengeko wa bei. Kwa hiyo, nitoe wito kwa wakulima kupeleka sasa pamba yao kwenye minada ili waweze kunufaika na bei ya sasa."

Kuhusu kilimo cha mkataba, Waziri Mkuu amesema wameamua kutumia utaratibu huo kwa baadhi ya mazao yakiwemo ya alizeti, ngano, shayiri na soya ili kumpatia tija mkulima, ambapo kwa upande wa soya soko la uhakika lipo nchini China.

"Kwa msingi huo, nasisitiza kwamba Wizara ya Kilimo hakikisheni mikataba inayoingiwa na wakulima inakuwa wazi ikionesha bei na kiwango cha kuuza. Vilevile, simamieni mikataba baina ya wakulima na wanunuzi wakubwa."

Kadhalika, Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuipongeza Wizara ya Kilimo kwa wazo lao la kuwa na maghala kwenye nchi zenye fursa ya masoko. "Wafuateni wateja msisubiri waje kwenu kwani biashara ni ushindani."

(Mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU


Mtwara kukutana na Dar kesho Mpira wa wavu fainali ya UMISSETA


Na Mathew Kwembe, Mtwara

Mabingwa watetezi wa kombe la UMISSETA katika mchezo wa mpira wa wavu (Volleyball) timu ya wasichana ya Mtwara watakutana na timu ngumu ya Dar es salaam kesho katika mchezo wa kusisimua utakaochezwa katika uwanja wa chuo cha ualimu Mtwara.

Mtwara imeingia hatua hiyo baada ya kuichapa Mbeya seti 3-0 na Dar es salaam imefanikiwa kufika fainali baada ya kuitoa Mara kwa seti 3-0.

Mara baada ya mchezo huo kocha wa Mtwara Gabriel Joshua aliwapongeza wapinzani wake Mbeya kwa ushindani waliouonyesha katika mchezo huo ambapo katika seti ya tatu wenyeji Mtwara walilazimika kushinda seti hiyo kwa point 25-21.

Joshua alisema tangu kuanza kwa mashindano ya mwaka huu hakuna timu iliyoweza kupata pointi 15 hivyo amesifu kiwango cha Mbeya na mashindano ya mwaka huu kwa ujumla kwani timu pinzani zilionyesha kiwango cha uchezaji tofauti na miaka ya nyuma.

Akizungumzia mchezo wa fainali dhidi ya Dar es salaam, nahodha msaidizi wa Mtwara Proscovia Conrad alitamba kuwa timu yake itaigalagaza Dar es salaam na wala hatarajii kupata upinzani kutoka Dar es salaam kama alioupata kutoka kwa timu ya Mbeya.

Michezo ya nusu fainali ya wavulana ya mpira wa wavu itachezwa mchana huu katika uwanja wa chuo cha ualimu Mtwara.

Matokeo ya michezo mingine ya nusu fainali ya mpira wa mikono wasichana kati ya Unguja dhidi ya Morogoro,  ambapo Unguja ilifungwa magoli 16-20, huku Geita dhidi ya Songwe 19-28.

Matokeo hayo yanaipa nafasi Morogoro kucheza na Dar es saaam hapo kesho katika fainali huku Geita na Unguja watacheza kutafuta mshindi wa tatu.

Kwa upande wa mpira wa kikapu timu zilizofuzu hatua ya nusu fainali ni Dar es salaam, Mwanza, Unguja na Morogoro kwa wasichana na wavulana ni Dar es salaam, Mwanza, Unguja na Morogoro.

Michezo yote ya nusu fainali itakamilika leo jioni na mechi za fainali zitachezwa kesho katika viwanja vya chuo cha ualimu Mtwara isipokuwa mchezo wa fainali wa soka utachezwa keshokutwa katika uwanja wa Nangwanda Sijaona Mtwara.


Source

Basi La Abiria Laacha Njia Na Kugonga Nyumba

Basi kampuni la Ulamaa T 330 DGB lililokuwa likisafiri kwenda Arusha kutokea Mwanza limepata ajali alfajiri ya leo kwa kuacha njia na kugonga nyumba eneo la Mkolani darajani jijini Mwanza.

Imeelezwa kwamba ndani ya nyumba hiyo kulikuwa na Watu 6 ambapo hakuna taarifa za kifo bali Majeruhi tu ambao wamepelekwa Hospitali ya Butimba.

Chanzo cha ajali kinaelezwa kuwa ni baada ya Dereva wa Basi kulikwepa gari dogo kulikosababisha gari kuacha njia baada ya kushindwa kulimudu



Bashe Aagiza Ras Tabora Kuwaondoa Watumishi Wa Manispaa Ya Tabora Waliochukua Mashamba Katika Mashamba Katika Skimu Inala


 NA TIGANYA VINCENT
NAIBU Waziri wa Kilimo Hussein Bashe amemwagiza Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Msalika Makungu kuwaondoa watumishi wote wa Manispaa ya Tabora ambao wamejimilikisha mashamba katika mradi wa Umwagiliaji wa Inala.

Alisema wamechukua maeneo hayo na kusababisha wananchi wanaozunguka mradi huo kukosa mashamba kwa ajili ya kulima kilimo cha mpunga.

Bashe alitoa kauli hiyo jana  wakati wa kufungua maadhimisho ya sherehe za siku ya Ushirika Duniani (SUD) ambapo Kitaifa inafanyika Mkoani Tabora na kilele kitakuwa tarehe 3 Julai mwaka huu.

Alisema licha ya Serikali kutumia fedha nyingi kujenga Bwawa hilo bado mradi huo haufanyikazi vizuri kama ulivyokusudiwa kwa sababu ya watumishi wa Manispaa ya Tabora kujimilikisha mashamba ambayo hawayalimi.

Katika hatua nyingine Naibu Waziri huyo alimwagiza Mrajis wa Vyama Vya ushirika Nchini Dkt. Benson Ndiege kufanya miaka mitatu mfululizo  maadhimisho ya sherehe za siku ya Ushirika Duniani (SUD) katika Mkoa mmoja badala ya kila mwaka kuanga katika eneo jipya.

Alisema hali hiyo itasaidia kuleta matokeo chanya kutokana na Washirika kujifunza katika eneo mmoja kwa kipindi cha miaka mitatu.

Wakati huo Naibu Waziri amewataka vijana kujiunga na ushirika ili kuondoa dhana potofu kuwa Ushirika na wazee na watu waliochoka.

Alisema ushirika ndio silaha pekee itakayowasaidia wakulima kupanga katika masoko na kupata bei nzuri itakayowasaidia kuondoa katika umaskini.

Bashe alisema Serikali itaendelea kuunga mkono Ushirika ili hatimaye uweze kuwa msaada mkubwa kwa wakulima kuchangia katika pato la Taifa kutoka la sasa la asilimia 26 na kuongezeka Zaidi.

Alisema kilimo ndio Sekta inayotoa ajira kwa wananchi wengi ni vema ikachangia kwa kiasi kikubwa katika pato la Taifa.

Kauli mbiu ya maadhimisho ya siku ya ushirika Duniani mwaka huu ni Ushirika  pamoja tujijenge uya kwa ubora na tija.


Penzi Kikohozi alijifichi nakupenda Lulu bora niwe mtumwa kwako- Lavalava


Penzi halfichiki kama chafya unaweza kusema hivyo hii imetokea kwa msanii Lavalava na Lulu Diva baada ya leo Lavalava kuamua kuanika ukweli wa penzi lao kwa kusema kuwa anampenda sana na amekubali kuwa mtumwa kwake.

Mara nyingi penzi la wasanii hawa limekuwa ni la siri sana hata pale vinapovuja video au picha wakiwa kwenye mapenzi mazito huwa wakihojiwa wanakataa lakini Kupitia kwenye ukurasa wake wa instaramu Lavalava ameandika hivi;

Dah Usiku Wajana Ndosijalala Kabisa Lulu Kiukweli Achatu Ifike Mahali Mtu Aweke Wazi Penzi Kikohozi Alijifichi Nakupenda Lulu Bora Niwe Mtumwa Kwako Hakuna Jinsi inaenda Wiki Sasa Hatuelewani Naumia Binadamu Tumeumbiwa Kukosea Hakuna mkamilifu Samahani Sana Narudia Tena Samahani nisamehe Mwenzako Plz πŸ’”πŸ’”πŸ₯ΊπŸ’¦πŸ’¦πŸ’¦πŸ’¦

UHURU WA VYOMBO VYA HABARI NA MATARAJIO YA UONGOZI WA AWAMU YA SITA YA SERIKALI YA TANZANIA


Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Uhuru wa vyombo vya habari ni miongoni mwa haki za msingi za kila raia wa Tanzania. Haki hii huwawezesha raia kupata na kutoa taarifa, kujieleza ili kutoa maoni yao katika masuala mbalimbali yenye maslahi yao. 

Pia, uhuru wa vyombo vya habari huchochea kukua kwa misingi ya haki za binadamu, demokrasia, na utawala bora.

 Kuwepo kwa misingi hii husaidia wananchi kushiriki katika uendeshaji wa nchi, kuchagua viongozi wanaowataka, kuhoji uendeshaji wa serikali pamoja na kufahamu masuala yanayoathiri maisha yao.

Katika miaka ya hivi karibuni, kumekuwepo na changamoto zinazoathiri au kuminya uhuru vya vyombo vya habari. Taasisi na asasi za kiraia zikiwemo Baraza la Habari Tanzania (MCT), Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA TAN), LHRC, na zinginezo zimeripoti matukio kadhaa kuashiria kuwepo kwa mazingira magumu kwa vyombo vya habari na wanahabari kutekeleza uhuru huu.

 Matukio hayo ni pamoja na kufutwa au kufungia vyombo vya habari, kutoza faini na karipio dhidi ya vyombo vya habari, ukamataji na uwekaji kizuizini kwa waandishi wa habari na vikwazo vya kisheria na kikanuni zinazodhibiti vyombo vya habari na wanahabari kutekeleza wajibu wao kwa uhuru.

Hata hivyo, kuapishwa kwa Mhe. Samia Suluhu Hassan kuwa Rais wa Awamu ya Sita ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kunaleta matumaini ya kuwepo kwa mazingira wezeshi yanayohimiza uhuru wa vyombo vya habari nchini.

 Matumaini haya yanajikita katika nia thabiti ya Mhe. Rais Samia ya kuhakikisha vyombo vya habari vinatimiza wajibu wake wa kuhabarisha umma kwa uhuru.

Akizungumza wakati wa kikao chake na wahariri wa vyombo vya habari kilichoafanyika tarehe 28 June 2021, Mhe. Rais Samia alinukuliwa akihimiza vyombo vya habari vilivyofungiwa kufunguliwa huku akivitaka kuzingatia sheria na miongozo ya serikali. 

Aidha, Mhe. Rais Samia mbali ya kuelekeza kulindwa na kuheshimiwa kwa uhuru wa vyombo vya habari, alitoa hakikisho la serikali yake kuzingatia kuwepo kwa sheria zisizokwaza upatikanaji na usambazaji wa habari nchini.

Ni matumaini ya wanahabari nchini kwamba Mhe. Rais Samia ameonesha dhamira ya wazi ya kuweka mazingira mazuri yanayochagiza uhuru wa vyombo vya habari. 

Hata hivyo, ni wajibu wa kila chombo cha Habari na waandishi wa Habari kuutumia vizuri uhuru huu kwa kutimiza Wajibu kwa kuzingatia weledi na maadili katika kutafuat, kuchakata na kusambaza taarifa na habari mbalimbali zenye maslahi kwa umma.

 Daima watambue kwamba hakuna uhuru bila wajibu.

Amteka mpenzi wake akitaka arudishiwe hela alizo honga, amuua


Jeshi la Polisi Mkoani Geita linamshikilia mwanaume mmoja mwenye umri wa miaka 30 kwa tuhuma za kumuua mpenzi wake aitwaye Esta John (28) mkazi wa Ibamba Wilaya Bukombe Mkoani humo ambaye kabla ya kifo chake alitekwa nyara na mpenzi wake.

Katika taarifa ya Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita Henry Mwaibambe aliyoitoa kwa waandishi wa habari inasema kwamba mwanamke huyo aliondoka nyumbani kwake juni 13 mwaka huu akiwa na mtu aliyesemekana ni mpenzi wake.

Baada ya kutoweka kwa muda mwanaume huyo ambaye jeshi la polisi halijamtaja kwa majina yake, alianza kuwapigia simu wazazi wa mwanamke akihitaji kulipwa pesa alizokuwa akimuhudumia kwa ahadi ya kumuoa na kwamba mtuhumiwa alibaini kuwa sio mwaminifu .

Kamanda Mwaibambe amesema baada ya taarifa kufika katika vyombo vya usalama upelelezi ulianza mara moja na kufankiwa kumkamata mtuhumiwa huyo akiwa na mali za marehemu ambaye alimteka nyara.

"Katika mahojiano alikiri kumteka nyara mwanamke huyo akishinikiza kulipwa gharama alizotumia kumtunza kwa ahadi ya kuoana lakini alibaini kwamba sio mwaminifu, aliposhindwa kurudisha pesa yake ndipo alichukua uamuzi wa kumuua na kumzika huko katika kijiji Masota Wilaya ya Bukombe'' Kamanda Mwaibambe.

Aidha amesema mtuhumiwa aliwaongoza Askari Polisi mpaka eneo alikomzika ambapo hatua za kisheria zilifuatwa ikiwmo kufukua kaburi na kufanya uchunguzi wa utambuzi wa mwili wa marehemu na kwamba uchunguzi zaidi wa tukio hilo unaendelea na upelelezi ukikamilia mtuhumiwa aafikishwa katika vyombo vya sheria.

Tuesday, June 29, 2021

Video : GUDE GUDE - DUNIA

Hatuna presha dhidi ya Simba, Tunawapiga - Yanga




KUELEKEA mchezo wao wa dabi ya Kariakoo dhidi ya Simba utakaopigwa siku ya Jumamosi, Uongozi wa kikosi cha klabu ya Yanga umefunguka kuwa hauna presha na mchezo huo, na wanaamini kwa maandalizi wanayoyafanya wataibuka na ushindi.

Yanga Jumamosi hii watakuwa wageni wa Simba katika mchezo wa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara utakaopigwa kwenye uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam. Mchezo huu hapo awali ulipangwa kupigwa Mei 8, kabla ya kuahilishwa mpaka Julai 3, mwaka huu.

Timu hizo zinaingia katika mchezo huu zikiwa na kumbukumbu ya sare ya bao 1-1, iliyopatikana katika Mchezo wa mzunguko wa kwanza uliopigwa Novemba 7, mwaka jana.

Akizungumzia maandalizi yao, Ofisa habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema: "Baada ya kufanikiwa kufika hatua ya fainali ya kombe la Shirikisho, kikosi chetu kimeendelea kuwa kambini kwa ajili ya kujiandaa na michezo yetu iliyosalia ya Ligi Kuu Bara ikiwemo mchezo dhidi ya Simba.

"Kwetu hatuna presha yoyote kuelekea mchezo huu, kwa kuwa tunautazama kama mchezo wa kawaida ambao tunakwenda kushinda na kuongeza pointi tatu muhimu, "

 

Video : BAHATI BUGALAMA - MIZIMU YA MABABU

Wimbo Mpya : LUNG'WECHA ITULI MUGUNITAKI BHAGALU

Tanzia :MHANDISI MFUGALE AFARIKI DUNIA



Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), Mhandisi Patrick Mfugale, amefariki dunia leo Juni 29, 2021 katika Hospitali ya Benjamin Mkapa jijini Dodoma.

Taarifa zinaeleza kuwa Mhandisi Mfugale aliondoka jana jijini Dar es Salaam na kuelekea Dodoma akiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi kwa safari ya kikazi ambapo majira ya saa tano asubuhi ya leo, alianza kujisikia vibaya na kukimbizwa hospitali ambapo muda mfupi baadaye, alifariki dunia.

Enzi za uhai wake, Mfugale atakumbukwa kwa kufanya utafiti na kutengeneza mfumo wa madaraja nchini ambapo miongoni mwa madaraja aliyosimamia ujenzi wake ni Daraja la Kikwete lililopo kwenye Mto Malagarasi, Daraja la Mkapa lililopo Rufiji, Daraja la Umoja linalounganisha Tanzania na Msumbiji lililopo Ruvuma na Daraja la Nyerere lililopo Kigamboni jijini Dar es Salaam.

Pia Mfugale atakumbukwa kwa kubuni na kusimamia ujenzi wa barabara za kitaifa zenye urefu wa takribani kilometa 36,258 na ndiye aliyekuwa mwenyekiti wa kikosi cha ujenzi wa reli ya kisasa SGR inayoendelea kujengwa.

Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. Amina!

TUME YA UTUMISHI WA UMMA YAENDELEA NA MKUTANO WA NNE KWA MWAKA WA FEDHA 2020/2021 JIJINI DAR ES SALAAM

Makamishna wa Tume ya Utumishi wa Umma wakiwa katika Mkutano leo 29 Juni 2021: Mheshimiwa Khadija A.M. Mbarak (kushoto) na Mheshimiwa Immaculata P. Ngwale (kulia) wakishiriki katika Mkutano wa Nne kwa mwaka wa fedha 2020/2021 unaofanyika Jijini Dar es Salaam. (Picha na PSC)
Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma, Bw. Nyakimura Muhoji (kushoto) akiwa na Makamishna wa Tume ya Utumishi wa Umma, Mhe. Balozi (Mstaafu) Daniel Ole Njoolay (katikati) na Mhe. Balozi (Mstaafu) John Haule wakishiriki katika Mkutano wa Tume leo 29 Juni 2021 unaofanyika Jijini Dar es Salaam.
Maafisa wa Tume ya Utumishi wa Umma: Bw. Peleleja Masesa, Katibu Msaidizi, Idara ya Rufaa na Malalamiko (kushoto), Bw. Evarist Mashiba, Afisa Sheria Mkuu (katikati) na Bw. Charles Mulamula, Mkurugenzi wa Kitengo cha Huduma za Sheria (kulia) wakishiriki Mkutano wa Tume unaoendelea kufanyika Jijini Dar es Salaam. (Picha na PSC)

TUNAUZA MAGARI NA KUKOPESHA

 


BIN KHALIFA MOTORS ni kampuni inayoagiza Magari kutoka Japan na Uingereza.


Tunakopesha Magari kwa bei nafuu, Unalipa asilimia 60% alafu asilimia 40% unalipa kwa miezi minne dhamana ni compprehensive insurance bima kubwa na mteja atalipia cartrack king'amuzi pindi atakapomaliza deni kitatolewa.


Ofisi zetu zipo magomeni mapipa na morroco.


Pia tunatoa ushauri wa kitaalam na kibiashara kuhusu magari bila malipo yoyote


Kwa mawasiliano 

+255718228825

+255784228825

+255758228825


Instagram page @bin khalifa motors co ltd













PATA KIWANJA KWA 1,800,000. DAR



Habari njema. kutoka SUYUTI LINK TANZANIA, tumeandaa mradi mkubwa wa tano kwa watanzania wenye kipato cha kawaida. 


Mradi wetu umekidhi vigezo vyote. 


Mradi wetu upo vikindu mjini maarufu kidubwa Village. 


BEI ya viwanja vyetu 1,800,000 /=

Utalipa kwa awamu mbili. 


Mradi upo 2km kutoka kilwa road 


HUDUMA ZA KIJAMII.

Huduma zote za kijamii zinapatikana kama vile.


1.Maji 

2.Shule za serikalini

3.Hospitali 

4.Umeme upo tayari ndani ya mradi 

5.Barabara zinapitika masaa 24 bila shida yoyo te

6.nyumba za ibada zipo karibu 

7.Eneo lipo tambarare hakuna mabonde. 

8.Viwanja vipo kwenye mpangilio mzuri,kwa mipango miji 


UKUBWA WA VIWANJA Futi 40 x 50 Utapatiwa na nyaraka zote za kiserikali. 


MAWASILIANO.

Tupigie Simu 0654 77 39 67  au 0687 83 04 05


Utatupata kupitia mitandao ya kijamii kama (Facebook, Instagram, YouTube) kwa jina moja @suyutwilinktanzania


ANGALIA VIDEO HII


USAFIRI NI BURE KILA SIKU PAKA SITE. 


SUYUTWI LINK Tanzania. 

TIMIZA NDOTO ZAKO. 









Shock as a woman in Mombasa accuses Rais UHURU Kenyatta of child neglect as she reveals the President is the father of her two kids – LOOK!


 A Mombasa-based woman has accused President Uhuru Muigai Kenyatta of child neglect and threatened to sue him in court to get child support.

In a Facebook post on Sunday, Evelyn Ikandi Evermwende said her efforts to meet the president have not been successful, and is only left with the choice of seeking court intervention.

"Mr. President, Uhuru Muigai Kenyatta, at the coast this weekend. Please address this issue before you go back to your station in Nairobi. 

"Do you recognise that these two children, Fadhili Jomo and Ahadi Maria came into this world via you? 

"Sir, I am really tired of being followed around by people affiliated to you. 

"My life has been hanging," Ikandi wrote.


Ikandi added that she has done all she can in her capacity to provide for the kids but whatever she has is never enough since she also shares the same with other suffering Kenyans.

"I do nothing peacefully because nafuatwa usiku na mchana. 

"After realising that you weren't taking responsibility, I worked hard as the woman I am. I do anything within my ability to earn an income for my children.

"Unfortunately, I can't do it peacefully. They imagine it's your money yet I hussle on my own," she said.

 Uhuru is said to have sired one child in 2016 and the other one in 2018.

TAASISI YA WAJIBU YAZINDUA RIPOTI ZA UWAJIBIKAJI MWAKA 2019/2020, WADAU WAPONGEZA

WADAU mbalimbali kutoka taasisi za Serikali, viongozi, wabunge ,Asasi za Kiraia na wanafunzi vyuo vikuu wameshuhudia uzinduzi wa Ripoti tano za Uwajibikaji ambazo zimetokana na Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali( CAG).

Ripoti hizo zimeandaliwa na Taasisi ya WAJIBU ambayo imeziandaa ripoti hizo za uwajibikaji baada ya kuichambua kwa kina ripoti ya CAG ambayo iliwasilishwa kwa Rais Samia Suluhu Hassan Machi 28 mwaka huu na baadae ripoti hiyo ya CAG ikakabidhiwa kwa Bunge Aprili 4 mwaka huu.

Akizungumza jana Juni 28,2021 jijini Dodoma, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya WAJIBU,Bwa. Ludovic Utouh ambaye amewahi kuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG), amesema ripoti hizo ni za tano tangu waanze kuandaa na kuzitayarisha kutokana na ripoti za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.

"Kama tunavyojua ripoti za mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali ambazo zimewasilishwa kwa Rais Machi 28 na kuwasilishwa bungeni Aprili 4, ni ripoti zinazotayarishwa kitaalamu, ni ripoti kubwa na ripoti ambazo kusema kweli kwa Watanzania wangi huwa hawana shauku ya kuisoma kwa sababu ya ukubwa wake.

"Sasa sisi WAJIBU tunachukua ripoti zile na kuchambua kwa undani na tunachukua yale tunayoamini yanauzito na umuhimu mkubwa kwa watanzania, kwa hiyo utakuta ripoti ya WAJIBU iliyozinduliwa leo ya Serikali kuu na mashirika ya umma inatokana na ripoti mbili kubwa za CAG za Serikali Kuu na mashirika ya umma na tumeweza kuja na kitabu cha kurasa 31.

"Na utakuta katika ripoti ile kubwa tumechambua mambo 10 ambayo tumeona yana umuhimu zaidi kwa maendeleo ya nchi yetu na ukienda kwenye ripoti ya serikali ya mtaa na miradi ya maendeleo ambayo nayo imetokana na ripoti mbili za CAG ambayo ina mambo 21 ina mambo nane ambayo tumeona yana umuhimu kwa umma.

"Ukija kwenye ripoti ya tatu ambayo ni ripoti ya Ufanisi ile kwa kuwa imetokana na ripoti ya CAG mwaka jana aliwasilisha bungeni ripoti 15 za ufanisi, sisi katika kupitia ripoti zile tumeona zina mambo muhimu zaidi kwa maendeleo ya nchi na tumeweza kuja na ripoti yenye page 31 ambayo inajikita kwenye maeneo hayo, "amesema Utouh.

Amesema ombi lake baada ya kuzinduliwa kwa ripoti hizo za uwajibikaji, ni vema wananchi wakazisoma kwani watazisambaza katika maeneo mbalimbali na zitakuwepo kwenye Website ya WAJIBU ,pia zitapatikana kwenye taasisi.

"Tutazigawa kupitia taasisi mbalimbali ili watanzania wapate ripoti hizi na wazisome, wakati tunasherehekea siku 100 za uongozi wa Rais Samia kweli sisi kama wananchi wa Tanzania tuwe na ari ya kuungana naye na kumsaidia kwa nia yake njema aliyonayo ya kuleta maendeleo ya nchi katika kudai uwajibikaji pale.

"Ambapo tunaona taasisi ya serikali au chombo cha Serikali hakitimizi wajibu wake , ndio lengo la WAJIBU tunasema kwamba rasimali za Serikali za taifa zikisimamiwa vizuri zinakuwa za kila Mtanzania.

Kwa upande wake Mwakilishi Ofisi ya Msajili wa NGO's Charles Mpaka amewapongeza WAJIBU kwa kuja na ubunifu waliokuja nao wa kupitia ripoti ya CAG na kuziandikia taarifa fupi ."Tumeona ripoti ya CAG ni kubwa na WAJIBU wameona umuhimu wa kuichambua na kuja na taarifa fupi.Ripoti ya CAG ilikuwa na zaidi ya kurasa 250 lakini wao wamekuja na taarifa yenye 21 mpaka 31.

"Maana yake tunaongea asilimia nane mpaka 11 wamekwenda kuipunguza, hivyo itakwenda kusaidia wananchi kupata tafsiri ya haraka na uelewa mwepesi wa ripoti ya CAG,"amesema

Wakati huo huo Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) Mhe.​Naghenjwa Kaboyoka amesema wamekuwa wakifanya kazi na WAJIBU kwa karibu sana na kwamba WAJIBU wamekuwa kama Bunge nje ya Bunge, wamekuwa wakiwakilisha wananchi , maana hizo ripoti zao wanazichambua kiasi kwamba wananchi wanaweza kuzisoma na kuzielewa.

"Kwa hiyo imekuwa mkono wetu wa kulia wa kusaidia kamati zetu mbili za PAC na LAAC , unakuta wenzetu wanakwenda mbali zaidi kueleza yale ambayo hatupati muda wa kuyazungumzia bungeni lakini wenzetu WAJIBU wanayachambua na kuyaeleza kwa wadau, na hivyo wadau wanapata nafasi ya kujua kilichopo.

"Kwa mfano tukiangalia bajeti ya mwaka huu siku zote tunasema kilimo ndio uti wa mgongo lakini akangalia bajeti iliyopita nafikiri ilitolewa tu asilimia mbili na hii ndio sekta ya uzalishaji, sasa kama sekta ya uzalishaji hazitatengewa hela nyingi zikazalisha tunategemea maendeleo gani, yatakuwa maendeleo ya vitu sio watu.

"Serikali za mitaa tuna tatizo moja, tatizo linawezekana hawa wanzetu tangu wamemaliza shule hajawahi kupelekwa kozi , hajui tena taratibu za kimataifa za kutoa ripoti zimekuaje , matokeo yake inawezekana kweli hajaiba lakini akawa hajui jinsi ya kuandaa ripoti, kwa hiyo anapata ripoti chafu.

"Lakini kusema kweli ni vizuri hawa wenzetu ambao wapo katika taaluma ya kusimamia masuala ya fedha mara kwa mara wapelekwe kwenye kozi, mara kwa mara waelezwe taratibu mpya na kufundishwa ,maana unakuta wanasema hawa wamezoea kuandika vocha tu,"amesema.

Ameongeza inawekana ni wasomi wazuri lakini viwango vya kimataifa vya kuandaa ripoti ambavyo vimewekwa havijui , hivyo halmashauri inapata hati chafu, mwingine anapata hati safi na anayepata hati safi haina maana mambo yao ni mazuri kuliko aliyepata hati chafu."Lakini ina maana gani , hesabu zao hawajazifunga kwa utaratibu unaokubalika kimataifa".

Aidha amesema anashukuru kusikia kuna halmashauri ambazo zimeanza kuchukua hatua za kuwapeleka watu wao wa kuandaa ripoti kupata kozi za kuwaongezea ujuzi huku akieleza CAG anaweza kusaidia hao watu wakaelekezwa namna ya kufunga hesabu.
Mwakilishi Ofisi ya Msajili wa NGO's Charles Mpaka (kushoto) akikata utepe kwa pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya WAJIBU,Bwa. Ludovic Utouh (kulia) kuashiria uzinduzi wa ripoti za Uwajibikaji mwaka 2019-2020 jijini Dodoma,huku tukio hilo likishuhudiwa na Wadau wengine mbalimbali zikiwemo taasisi za Serikali, viongozi, Wabunge,Asasi za Kiraia na wanafunzi vyuo vikuu.
Mwakilishi Ofisi ya Msajili wa NGO's Charles Mpaka (kushoto) kwa pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya WAJIBU,Bwa. Ludovic Utouh (kulia) wakiangalia vitabu vya ripoti hizo namna ya kuwagawia Wadau mbalimbali walioshiriki kwenye uzinduzi wa ripoti za Uwajibikaji mwaka 2019-2020 jijini Dodoma.

WADAU mbalimbali kutoka taasisi za Serikali, Wabunge ,Asasi za Kiraia na wanafunzi vyuo vikuu ambao wameshuhudia uzinduzi wa Ripoti hizo,wakipitia kwamakini Ripoti hiyo mara baada ya kuzinduliwa rasmi jijini Dodoma.
Picha ya pamoja mara baada ya uzinduzi wa ripoti hiyo
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya WAJIBU,Bwa. Ludovic Utouh akizungumza jambo mbele ya Wadau mara baada ya ripoti hiyo kuzinduliwa
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...