Tuesday, May 25, 2021
Wizara Yatangaza Operesheni Komesha Uhalifu Nchi Nzima, IGP Sirro Kuongoza Ma RPC Katika Operesheni Hiyo
Na Abubakari Akida ,Dodoma
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi imetangaza Operesheni Maalumu lengo ni kukomesha uhalifu ambao umeanza kurejea taratibu baada ya muda mrefu nchi kuwa katika hali ya amani na usalama.
Akizungumza mbele ya Mkutano wa Waandishi wa Habari jijini Dodoma, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,George Simbachawene amesema kwa tathmini uhalifu umepungua sana nchini ila baadhi ya matukio machache yanayotokea yamekua yanapata muhamko mkubwa kutokana na njia za upashanaji habari kubadilika hivi sasa.
"Sisi kama Wizara kupitia Jeshi la Polisi tumejipanga,leo nimekaa kikao na IGP Sirro pamoja na Makamishna wake wote tumejadiliana kuimarisha hali ya ulinzi na usalama kwa wananchi wetu na sasa tunakuja na Operesheni ya Nguvu katika mikoa yote lakini la pili tunasisitiza ulinzi shirikishi maana Watanzania ni wengi ukizingatia idadi ya askari wetu,tunawaomba wenzetu wa TAMISEMI kupitia Kamati za Ulinzi zinazoongozwa na Wakuu wa Mikoa na Wilaya hadi kushuka ngazi ya chini tushirikiane ili kuweza kurudisha dhana ile ya ulinzi shirikishi ambayo ilisaidia sana kukomesha uhalifu" alisema Simbachawene
Akizungumzia tukio la mauaji ya mtoto anaekadiriwa kuwa na umri wa miaka 5 hadi 6 ambae mwili wake uliokotwa karibu na dimbwi la maji katika Kitongoji cha Usadala,Kijiji cha Utemini,kata ya Ndono,wilaya ya Uyui,mkoa wa Tabora, Waziri Simbachawene amesema upelelezi wa awali unaonyesha kama alitupwa huku mwili ukiwa umearibika sana huku akiweka wazi uchunguzi wa jeshi la polisi unaendelea wakishirikiana na Mkemia Mkuu wa Serikali kubaini vinasaba vya mwili wa mtoto huyo kama alikuwa albino au la.
"Nimesikia baadhi ya taasisi za haki za binadamu wakinitaka niseme, nitoe kauli lakini nasema hapana maana upelelezi wa polisi una taratibu zake na tunaendelea kupeleleza kitaalamu juu ya tukio hilo, tunaomba watuamini ili tuache tufanye kazi kitaalamu" alisema Simbachawene
Akizungumza katika Mkutano huo Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini,Simon Sirro amewataka wahalifu kuacha matendo ya hovyo mara moja huku akiweka nguvu ya jeshi katika kupambana na wahalifu.
"Ukitaka kuishi maisha mazuri na marefu acha uhalifu lakini kitendo cha kuendelea kufanya uhalifu ni kuichokoza serikali na niwaambie serikali ni ile ile,IGP ni yuleyule na Rais ni yule yule na ana madaraka ni yaleyale,watu watii sheria bila shuruti kuna watu wametoka gerezani wamerudia matendo yale yale waache hayo matukio kama wanapenda Watoto wao na familia zao" alisema IGP Sirro
-
WATU saba wamefariki dunia baada ya bajaji waliyokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na lori eneo la Mpemba, Tunduma wilayani Momba, mk...
-
Rais Uhuru Kenyatta na viongozi wengine nchini Kenya wametuma salamu zao za rambi rambi kwa familia ya marehemu Yusuf Haji. Rais Uhuru Kenya...
-
Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga Daktari Daniel Henry Na Isaac Masengwa ******************* Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga...
-
Mbunge wa Kigoma Mjini na Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe asomewa mashtaka matatu ya uchochezi, yenye nia ya kuleta ch...
-
Mfanyabiashara raia wa Kenya, Raphael Ongangi anayedaiwa kutekwa na watu wasiojulikana maeneo ya Oysterbay, Dar es Salaam nchini Tanzania am...
-
MWANA-mfalme wa Uingereza,. Prince Charles, ambaye ni mtoto wa kwanza wa Malkia Elizabeth wa Pili wa Uingereza, na mrithi wa kwanza katika ...
-
Vijana wametakiwa kuwa wazalendo katika nchi yao kwa kukemea vitendo viovu katika jamii na kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu. Aidha Sil...
-
Zikiwa zimesalia siku chache tu Hoteli Mpya ya Kisasa yenye Ubora wa hali ya juu 'SHY PARK HOTEL' ifunguliwe Rasmi mwezi Agosti 202...
-
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko amefunga rasmi mafunzo ya sheria za usalama barabarani kwa maaskofu na wachungaji wa makanisa ya...
-
Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mjini Richard Kasesela Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mjini Richard Kasesela amelishauri Kanisa la Kiinjili la Kilutheri ...
