Na Shamimu Nyaki, Dar es Salaam
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa ameziagiza Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Wizara ya Maliasili na Utalii kushirikiana katika kuyatambua maeneo yanayokidhi vigezo vya kuingizwa katika Gazeti la Serikali na kuwa urithi wa Taifa ili yalindwe.
Mhe. Majaliwa ametoa maagizo hayo leo Mei 21, 2021 Jijini Dar es Salaam alipofungua Kongamano la Kutambua na Kuenzi Mchango Anuwai wa Historia ya Tanzania katika Ukombozi wa Bara la Afrika, ambapo amewasisitiza Watanzania kujivunia historia hiyo kwa kufanya kazi kwa bidii na kulinda rasilimali za nchi kwa uzalendo, kuendelea kuwa na Utangamano,Utaifa pamoja na kuenzi mazuri yaliyoachwa na wapigania Uhuru wa nchi na Afrika.
"Kongamano hili linaonyesha umuhimu wa Lugha ya Kiswahili katika Bara la Afrika kwa kuwa ndio lugha iliyotumika katika Harakati za ukombozi,nasisitiza Watanzania kutumia Kiswahili ndani na nje ya nchi na lazima Wakalimani wengi wazalishwe ambao watasaidia kutafsiri lugha hii adhimu" amesisitiza Waziri Mkuu Majaliwa.
Aidha, ameendelea kusisitiza umuhimu wa kufundishwa kwa Somo la Historia katika ngazi zote za shule lengo likiwa ni kufundisha vijana historia ya Tanzania, umuhimu na mambo yote ambayo Tanzania imefanya ndani na nje ya nchi, kutambua umuhimu wa kulinda tunu na amali za nchi pamoja na umuhimu wa kuendelea kuilinda amani ya nchi.
Wakati huo huo Waziri Mkuu ametumia nafasi hiyo kuagiza Wizara ya Habari, TAMISEMI na Ofisi ya Rais kuchambua na kutolea maamuzi changamoto zinazowakabili Maafisa Michezo na Utamaduni ikiwemo ya Muundo wa Utumishi ili kila mmoja awajibike kilingana na Taaluma yake.
Awali akimkaribisha Waziri Mkuu, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa amesema Kongamano hilo ni sehemu ya utekelezaji wa maazimio ya Umoja wa Afrika ya mwaka 2011 ya kuwa Tanzania iwe na Makao Makuu ya Uhifadhi wa Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika ili urithi huo usipotee kwa ajili ya vizazi vilivyopo na vijavyo.
"Kongamano hili litaelimisha umma umuhimu wa kujikomboa kiuchumi na kifikra kupitia uhifadhi na utangazaji wa zao la utalii wa kiukombozi pamoja na kuhamasisha jamii kuwa na utangamano wa kitaifa ambao huzaa uzalendo"amesisitiza Mhe.Bashungwa.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Hassan Abbasi amesema kuwa lengo la Kongamano hilo ni kusherehekea mchango wa Tanzania katika ukombozi wa Bara la Afrika, huku akieleza kuwa baada ya Kongamano hilo litafuatiwa na Kikao kazi kwa Maafisa Utamaduni na Michezo kujadili mambo mbalimbali ya sekta hizo.
Katika Kongamano hilo Mada mbalimbali ikwemo Mchango wa Tanzania katika ukombozi wa Afrika na Chimbuko la Programu ya Urithi wa Ukombozi wa Afrika na Umuhimu wake kwa Tanzania na Afrika, pamoja na shuhuda mbalimbali za wapigania uhuru.
MWISHO..
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Na Mbuke Shilagi Kagera. Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko amesema kuwa mradi wa umeme wa maji ya maporomoko wa Rusumo...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Tanzania November 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na za ny...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 9, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na ...
-
Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga Daktari Daniel Henry Na Isaac Masengwa ******************* Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga...
-
Mhamasishaji maarufu wa mitandaoni, Mwijaku, ameandika ujumbe unaotoa ushauri kwa Rais wa klabu ya Yanga, Injinia Said Hersi, kupitia ukuras...
-
Msimamo Ligi Kuu Bara 2024/2025 Msimamo Ligi Kuu Bara 2024/2025, NBC Premier League Tanzania Msimamo Ligi Kuu NBC 2024/2025 Tanzania Premier...
-
WATU saba wamefariki dunia baada ya bajaji waliyokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na lori eneo la Mpemba, Tunduma wilayani Momba, mk...
-
Zaidi ya ghorofa 100 jijini Dar es Salaam zilibainika kujengwa kinyume cha taratibu za ujenzi, Bunge lilielezwa. Kwa mujibu wa ripoti iliy...
-
Msanii wa nyimbo za asili Nyanda Madirisha Obhado 'Maliganya' maarufu Shikomba Bhulolo anakualika kusikiliza wimbo wake mpya 2021 un...
