Wednesday, May 26, 2021

Whatsapp yapinga mabadiliko kanuni za mtandao India



Kampuni ya Facebook ambayo pia inamiliki mtandao wa kijamii wa WhatsApp imefungua kesi dhidi ya serikali ya India ikiomba kuzuiwa kwa kanuni zinazotarajiwa kuanza kutumika leo ambazo wataalamu wa sheria wanasema zitailazimisha kampuni hiyo ya Marekani kuvunja utaratibu wa kulinda usiri wa taarifa watumiaji.


Kwa mujibu wa mtoa taarifa kwa shirika la habari la Reuters mashtaka hayo yanaiomba mahakama ya mji wa Delhi kusema kuwa moja ya vipengele vya kanuni hizo kinavunja haki ya faragha iliyotajwa kwenye katiba ya India kwakuwa kinataka kampuni za "mitandao ya kijamii kumbainisha mtu wa kwanza kutengeneza au kusambaza ujumbe" pindi mamlaka zitakapotaka taarifa hizo.


Wakati sheria za India zikiwataka WhatsApp kumbainisha mtu ambaye amethibitisha pasipo mashaka kuwa ni mhalifu, kampuni hiyo imesema kwa namna mitandao inavyofanya kazi haitaweza kutoa taarifa za ina hiyo ikiwa peke yake bila kushirikiana na wadau wengine.


Imeendelea kufafanua kuwa kwakuwa ujumbe wa mawasiliano unaotumwa baina ya watumiaji wa WhatsApp hufungwa kwa namba za siri maalum ambazo hutengenezwa na mitambo (end-to-end encryption) hivyo ili kutoa taarifa hizo kampuni hiyo itapaswa kufungua zamba hizo za siri kwa watumaji na wapokeaji na tayari watakuwa wameingilia taarifa binafsi za watumiaji.


Reuters imesema bado haijapata uhakika wa mashtaka hayo licha ya kuzungumza na watu wenye kulifahamu jambo hilo ambao hata hivyo wamekataa kutajwa hadharani kutokana na unyeti wa jambo hilo.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...