Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Kamishna Msaidizi wa Polisi,Wilbrod Mutafungwa ametoa taarifa ya hali ya Usalama Barabarani nchini.
Kamanda Mutafungwa amesema katika kipindi cha Januari hadi Aprili 2021, abiria 120 wamefariki na 332 kujeruhiwa.
Aidha ameongeza kuwa kwa upande wa pikipiki katika kipindi cha Januari hadi Aprili 2021, madereva bodaboa 61 wamefariki na 78 kujeruhiwa.