Saturday, May 1, 2021

RAIS SAMIA : TUNATARAJIA KUAJIRI WATUMISHI 40,000...MISHAHARA TUTAPANDISHA MWAKANI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiwahutubia Wafanyakazi mbalimbali katika Kilele cha Sherehe za Siku ya Wafanyakazi Duniani Mei Mosi Kitaifa ambazo zimefanyika Jijini Mwanza leo tarehe 01 Mei, 2021 katika uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza. Picha Ikulu

**

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema jumla ya wafanyakazi zaidi ya 85,000 elfu hadi 91,000  watapanda vyeo mwaka ujao na  kuajiri watumishi  40,000 katika Idara ya Elimu na Afya.

Ameyasema hayo kwenye maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani Kitaifa leo Mei 1, 2021 katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

"Ndugu zangu mimi ni mama, mama ni mlezi..Dai hili ni la msingi na la kweli. Mishahara haijaongezwa muda mrefu. Kutokana na mlipuko wa ugonjwa Corona uwezo wetu kiuchumi umepungua, imekuwa vigumu kwangu kuongeza mishahara lakini tutaboresha maslahi ya wafanyakazi", amesema Rais Samia.

"Mishahara haijaongezwa kwa muda mrefu, Mimi binafsi natamani kuongeza mishahara mwaka huu ila kwasababu mbalimbali nimeshindwa, uchumi wa Tanzania umeshuka kutoka 6.9% hadi 4.7% kwasababu ya Corona, nawaahidi mwakani siku kama ya leo nitapandisha mishahara", amesema Rais Samia
 


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...