Friday, May 28, 2021
Mwalimu akamatwa akijifanya Usalama wa Taifa ili atapeli
SALVATORY NTANDU
Jeshi la polisi mkoa wa shinyanga linawashikilia watuhumiwa watatu Dismond Zakaria mwalimu (33) Feisal Husein mtaalamu wa teknolojia ya mawasiliano (27) na Juma Almasi (35)mfanyabiashara kwa tuhuma ya kupatikana na nyaraka za serikali za kughushi kwa lengo la kufanya utapeli kwa wananchi.
Akizungumza na waandishi wa habari wilayani Kahama kamanda wa Jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga (ACP) Debora Magiligimba amesema kuwa watuhumiwa hao wamekamatwa mei 26 mwaka huu katika mtaa wa namanga wilayani humo katika msako maalumu wa kupambana na wahalifu.
Alisema kuwa baada ya kukamatwa walipatikana na nyaraka mbalimbali za serikali ikiwemo kitambulisho cha Idara ya usalama wa taifa,vitambulisho viwili vya jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ) mhuri mmoja na barua mbalimbali zenye nembo ya jeshi la hilo.
"Watuhumiwa hawa hutumia magari mawili kufanya utapeli katika maeneo mbalimbali ya Tanzania yenye namba za usajili T 677 BMA Toyota Carina na T 110 DSX Toyota Rumion kwa kujiwasilisha kwa wafanyabiashara hususani watoa huduma za kifedha kuwa wao ni maafisa wa umma na wakifanikisha azima yao hutoroka,"alisema Magilimba.
Kamanda Magiligimba amesema kuwa watuhumiwa hao wanatumia vitambulisho vya Jeshi la wananchi viwili vyenye cheo cha Kanali na kimoja cha idara ya usalama wa taifa,pamoja na sare kwa lengo la kuwahadaa wananchi ili kujipatia fedha kwa njia isiyo halali huku wakijua wazi kuwa suala hilo ni kinyume cha sheria.
"Tumewakamata wakiwa na karatasi bandia zinazotumika kutapelia watoa huduma za za fedha,walikuwa wanatumia mbinu ya kuacha mabegi yao yenye karatasi hizo bandia katika ofisi hizo na kisha hurudi jioni na kuwaaminisha kuwa ni fedha halali,jambo ambalo halina ukweli wowote,"alisema Magiligimba.
Amefafanua kuwa mbinu nyingine inayotumiwa na watuhumiwa hao ni pamoja na kuwatongoza na kuwanywesha pombe wanawake na kuwaibia vitu vya thamani kama vile simu na fedha pamoja na kuwaahidi kuwapatia kazi kwa idara ya usalama wa taifa na jeshi la wananchi wa Tanzania.
"Bado tunaendelea kuwahoji na upelelezi ukikamilika tutawafikisha mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili na kuwaomba wananchi kuendelea kutoa taarifa pindi wanapowatilia shaka watu wanamna hiyo ambao hutumia vibaya nyaraka za serikali kujipatia kipato kwa njia isiyo halali,"amesema Magiligimba.
Mwisho
-
Baadhi ya raia walioyatoroka makaazi yao baada ya mlipuko wa volkano uliotokea usiku wa kuamkia huko mjini Goma mashariki mwa Jamhuri ya Kid...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 9, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na ...
-
Bongo Deco wauzai wa vifaa mbalimbali vya umeme kama TV, Subwoofer, Hometheator, Majiko madogo na makubwa ya Gesi, Friji, Generator nk leo w...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Msanii maarufu Ntemi O Mabala ' Ng'wana Kang'wa kutoka Kahama Mkoani Shinyanga anakualika kusikiliza wimbo wake mpya unaitwa M...
-
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (kulia)akimsikiliza Waziri wa Maliasili na Utalii wa Jamhuri ya ...
-
Hii hapa ngoma mpya ya Msanii wa Nyimbo za asili Mama Ushauri ameshirikiana na Ng'wana Ng'washi inaitwa Merimela ,imetengenezwa Lw...
-
Kuongezeka kwa ghasia za hivi majuzi kumesababisha idadi kubwa ya raia wa Lebanon kukimbia kutoka Beirut huku milipuko ikitikisa jiji hilo...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 15, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan amekagua ujenzi wa Daraja la J.P Magufuli (Kigongo – Busisi) ...