Saturday, May 1, 2021

Mei mosi usalama wa kutosha Mwanza


Na Maridhia Ngemela, Mwanza.

JESHI la polisi mkoani Mwanza   limejipanga  kuhakikisha  wanaimalisha ulinzi na usalama kabla wakati wa sherehe za maadhimisho ya meimosi itakayo fanyika   Mkoani hapa kesho.

Wito  huo umetolewa na Kamanda wa  Polisi Jumanne Murilo wakati akizungumza na waandishi wa habar Ofisini  kwake  alisema wananchi wa sekta binafsi na wanaofanya kazi Serikalini  mashirika yote  wanahakikishiwa mazingira ya usalama yameimalishwa kwani  hakutakuwa na kizuizi kitakachifanya  maadhimisho  hayo kuwa na dosari.

 Alisema mifumo ya kiusalama  imeimalishwa pande zote za  nchi kavu hadi ziwaVictoria ambayo nisehemu ya mkoani hapa.

"Jeshi la polisi linaendelea kupokea  taarifa mbalimbali kutoka kwa wananchi wema  kwani hatutakubali na  hatatoa nafasi kwa watu wenye fikra za kihalifu ambaye atatakutekeleza kipindi hili na baada ya sherehe hizi   tusilaumiane, nawaomba wananchi  wajitokeze kwa wingi kwenye sherehe hizi."alisema Murilo.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella amewaomba wananchi wa Mkoa wa Mwanza kama ilivyo ada wajitokeze kuunganana  na Rais Samia Suluhu Hassan kwenye shehere  za kilele cha maadhimisho ya siku ya Wafanyakazi Duniani  yanayoadhimishwa kila ifikapo Mei Mosi kila Mwaka pamoja na kuwaunga mkono wafanyakazi na kuonesha utaifa na uzalendo wao.

Mongella ameyasema hayo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya maandalizi ya  sherehe hizo ambayo yamefikia zaidi ya asilimia 99 huku akisema katika maadhimisho hayo Rais Samia ndiye mgeni rasmi huku kitaifa yanafanyika mkoani Mwanza ambapo kama Mkoa umepewa heshima kubwa hivyo wananchi kama ilivyo utamaduni wao wajitokeze kwa wingi katika uwanja wa CCM Kirumba ambapo milango itakuwa wazi kuanzia saa 12 alfajili.

Amesema sherehe hiyo ilianzishwa mwaka 1800 baada ya wafanyakazi kuungana kupigania maslahi yao kutokana na mapinduzi ya viwanda duniani.

"Ni siku muhimu kwa wafanyakazi wote ambao ni muhimu kiuchumi,kijamii na maendeleo ambapo mifumo imekuwa ikihangaika kutoa ajira zenye staha kwa watumishi kufanya kazi kulingana na mikataba.Pia ni heshima kubwa na pekee kwa Mkoa wa Mwanza, Rais Samia na Makamu wake,Philipo Mpango na viongozi mbalimbali watashiriki,"amesema Mongella na kuongeza

"Hii ni ziara ya kwanza ya Rais Samia mkoani hapa ambaye ni mwanzilishi wa MV Six Lake Victoria, hivyo niwaombe wadau wote kushiriki maadhimisho ya mwaka huu, Rais wa TUCTA Tumaini Nyamhokya, vyama vyote vya wafanyakazi katika kutekeleza hili tunashukuru na tunawapa heshima na kuwathamini wafanyakazi kwa utendaji wao," amesema Mongella

 

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...