Saturday, May 1, 2021

Mapendekezo ya Tucta kwa Rais


Na Maridhia Ngemela

Shirikisho la vyama vya wafanyakazi Tanzania (TUCTA) limetoa pendekezo la kiwango Cha kumuwezesha mtu kuishi kiwe si chini ya laki 970,000 ili kuweza kupunguza ugumu wa Maisha kwa wafanyakazi.

Hayo yamebainishwa na Kaimu Katibu  Mkuu wa shirikisho hilo Said Wamba alipokuwa akisoma risala ya wafanyakazi Mbele ya Raisi Samia Suluhu Hassan kwenye maadhimisho ya sherehe  ya siku ya wafanyakazi duniani ambayo kitaifa yamefanyika Mkoani Mwanza.

Alisema Tucta ilifanya utafiti mwaka 2006 wa kima Cha chini Cha mshahara kinachomwezesha mfanyakazi kumudu mahitaji muhimu Kama vile chakula,Kodi ya pango,matibabu,kusomesha,mavazi usafiri na kubaini shilingi laki 315,000 kwa wakati huo ingetosha kumudu.

Aidha ili fanya utafiti mwingine mwaka 2014 na kubaini kuwa kima Cha laki 720,000 kw wakati huo ndicho kingemwezesha mfanyakazi kumudu maisha yake.

Alisema licha ya viwango hivyo kutofikiwa mpaka Sasa gharama za maisha zimeendelea kupanda na kuwaumiza wafanyakazi wa Sekta zote(Binafsi na Umma) Hali iliyopelekea wafanyakazi pamoja na familia zao kuishi maisha ya chini.

Alisema wakati umefika kuwa na kiwango halisi Kitaifa kitakachomwezesha mtu kuishi ili kuweka malengo ya kufikia kiwango hicho kitakacholinda  ustawi wa maendeleo ya wafanyakazi na Taifa kwa ujumla.

Hata hivyo aliongeza kuwa wafanyakazi hawajaongezwa mishahara kwa miaka nane kwa sekta isiyo rasmi na miaka sita kwa sekta ya umma kwani Hali hiyo imesababisha kupunguza kwa ari na mori wa kazi na kupelekea  ufanisi na uwajibikaji mahala pa kazi kwani gharama za maisha zimezifi kupanda  ilihali stahikina ujira zimeendelea kuwa duni.

Aliiomba Serikali  kupitia wataalamu na wazalendo kufanya marekebisho ya Sheria  kwani  tozo ya kuongeza thamani ya fedha( value retention fee) ambayo ni asilimia sita  kwa Kila mwaka  ili kufanya mkopo aliopokea mnufaika uendane na thamani ya fedha ya wakati  huo.

"Matokea ya thamani ya Deni inakuwa kubwa na inabadilika na kupanda kwa Kila mwaka tofauti na  kiasi  alichokopeshwa mnufaika,.


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...