Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linatarajiwa kufanya mkutano wa dharura na wa faragha kuhusu Mali hii leo, baada ya jeshi la nchi hiyo kuwakamata viongozi wawili wa serikali ya mpito.
Mkutano huo umependekezwa na Ufaransa, Niger, Tunisia, Kenya pamoja na Saint Vincent na Grenadines. Kanali Assimi Goita amesema jana kwamba amemuondoa madarakani rais wa mpito na waziri mkuu, waliopewa jukumu la kurejesha tena utawala wa kiraia baada ya mapinduzi ya Agosti iliyopita.
Hatua yake hiyo imelaaniwa vikali na jumuiya ya kimataifa iliyotoa vitisho vya kuiwekewa Mali vikwazo.