Thursday, May 27, 2021

Baraza la haki za binadamu la UN lailaumu Israel


Kamishna mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu Michelle Bachellet amesema kwamba mashambulizi makali ya Israel dhidi ya Gaza huenda yamesababisha uhalifu wa kivita na kwamba kundi la wanamgambo la Hamas pia limekiuka sheria ya kimataifa kwa kufyetua maroketi kuelekea Israel.

 Bachellet amesema ofisi yake imethibitisha vifo vya wapalestina 270 katika ukanda wa Gaza,Ukingo wa Magharibi na Jerusalem Mashariki,wakiwemo watoto 68 wakati wa vita hivyo vya siku 11 vilivyotokea mwezi huu. 

Wengi waliuwawa na mashambulizi ya Israel katika mji wa Gaza unaodhibitiwa na kundi la Hamas. Mashambulizi ya maroketi yaliyofanywa na Hamas yaliua Waisraeli 10. 

Mkuu huyo wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa ameyasema hayo katika kikao maalum cha baraza la haki za binadamu la Umoja huo kilichofanyika kufuatia ombi la nchi za kiislamu.

 Nchi hizo zimetaka tume maalum ya uchunguzi iundwe kuchunguza uwezekano kwamba vitendo vya uhalifu vimefanyika na wahusika kubebeshwe dhamana.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...