Tuesday, April 27, 2021

Tamko la Azam kuhusu Prince Dube kutua Simba

 


Uongozi wa Klabu ya Azam Fc umesisitiza kwamba mshambuliaji wao Prince Dube hatoondoka klabuni hapo kama ambavyo imearifiwa na mitandao mbalimbali ya kijamii kuwa huenda atajiunga na wekundu wa msimbazi Simba mwishoni mwa msimu huu.

 


Kauli hiyo imetolewa na Mtendaji Mkuu wa wana lambalamba hao Abdulkarim Amim ''Popat'' ikiwa ni siku chache baada ya Prince Dube kuifungia bao pekee na la ushindi Azam Fc dhidi ya Yanga lililomfanya awe kinara wa ufungaji katika Ligi Kuu Tanzania bara akiwa amefikisha mabao 12 akimpiku Medie Kagere wa Simba mwenye mabao 11.


Popat amesema ''Kwa ufupi Prince Dube yupo sana Azam, na hauzwi kwa gharama yotyote hapa nchini Tanzania, iwapo ataondoka basi itakuwa ni nje ya nchi'' alisema Mtendaji Mkuu huyo wa Azam.


Kwa upande wa Dube alipoulizwa na East Africa Radio iwapo angependa kujiunga na Simba iwapo itatokea nyota huyo alikataa kuzungumza chochote.


''Mimi ni mchezaji wa Azam, na ninaheshimu Mkataba wangu na wao hivyo sipo tayari kusema lolote juu ya hilo''alisema Dube.


Nyota huyo raia wa Zimbabwe amekuwa na mwenendo mzuri ikiwa ndio msimu wake wa kwanza katika Ligi Kuu Tanzania bara, kiasi cha kuwa kivutia kwa vigogo wa soka nchini 

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...