Na Maridhia Ngemela Mwanza
JESHI la Polisi mkoani Mwanza linawashikiria watu 24 kwa tuhuma za makosa mbalimbali ikiwamo mauwaji , kuvunja ofisi za shule za msingi na kuiba vitabu pamoja na kujihusisha na mapenzi na wanafunzi.
Hayo yamesemwa na Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani hapa Jumanne Muliro wakati akizungumza na Waandishi wa Habari alisema mtuhumiwa Japherth Musiba amehukumiwa miaka 30 kwa kosa la kujihusisha na mapenzi na wanafunzi na kuwapatia mimba ambazo zinasababisha kuvunja ndoto zao.
Amesema kufanya mapenzi na mwanafunzi ni kosa kisheria kwani kubaka ,kulawiti ni vitendo ambavyo havikubariki katika jamii.
Kamanda ameongeza kuwa, Kosa la pili ni wizi wa vitabu uliofanyika katika
ofisi za shule tatu za msingi Wilayani Kwimba ziligundulika kuvunjwa na kuiba vitabu 529 vya mitaala mipya vya masomo mbalimbali.
Alisema Jeshi hilo linawashikiria walimu wa shule tatu za Msingi ikiwamo Igoma, Manguluma na Bujingwa kwa kosa la kula njama za kuiba vitabu na kutengeneza matukio ya kufikirika ya kuvunja ili kuficha uhalisia wa tukio hilo.
Alisema walibaini vitabu hivyo viliibwa na kuuzwa kwa wafanyabiashara wa maduka ya vitabu Jijini hapa kwani baada ya mahojiano ya kina walikili na kuhusika na ununuzi wa vitabu hivyo.
" Tunawashikiria Walimu watatu ,Walinzi wanne kwa kupokea Mali za wizi na mtaalamu mmoja Mengi Muheta (43)ambaye ni Mwalimu wa Shule ya Msingi Kishiri aliyekuwa anajihusisha na kufuta alama za serikali inayosema kitabu hiki hakiuzwi,"alisema Muliro.
Hata hivyo aliongeza kuwa Jeshi hilo linawashikiria watu wawili kwa tuhuma za makosa ya mauaji ya mtu mmoja 42 yaliyotokea eneo la Kanyerere kata ya Mkuyuni Wilayani Nyamagana kwa kinachodaiwa wivu wa kimapenzi.
"Pembeni mwa mwili wa marehemu waandika ujumbe kwenye sakafu uliosomeka kuwa mke wa mtu ni sumu kwani watuhumiwa wanafanyiwa mahojiano ya kina na upelelezi ukikamika watafikishwa mahakamani"alisema muliro.
Kamanda ametoa wito kwa wananchi kuelekea msimu wa sikukuu ya pasaka waendelee kutoa ushirikiano kwa JESHI la Polisi na kuhimalisha usalama Katika mkoa wa Mwanza na Jeshi Hilo linajivunia kuwakamata watuhumiwa kabla ya kufanya uhalifu.