Sunday, April 25, 2021

Chanjo ya Johnson & Johnson yaruhusiwa tena Marekani


Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa cha Marekani  (USA) kilitoa ishara njema kwa chanjo ya Johnson & Johnson, ambayo ilisitishwa mnamo Aprili 13, kutokana na kusababisha tatizo la kuganda kwa damu.

Kamati ya Ushauri ya Majaribio ya Chanjo ya CDC iliamua kuendeleza matumizi ya chanjo ya corona (Covid-19) iliyozalishwa na Johnson & Johnson kwa kuunga mkono kwa kura 10 dhidi ya 4.

Ilielezwa kuwa kamati hiyo ilifikia makubaliano kwamba faida za chanjo ya  Covid-19 ya Johnson & Johnson, ambayo hutolewa kwa kipimo cha dozi moja pekee, ni zaidi ya hatari yake.

Katika taarifa iliyotolewa na CDC na Mamlaka ya Chakula na Dawa ya Marekani (FDA) mnamo Aprili 13, ilipendekezwa kuwa matumizi ya chanjo ya Covid-19 ya Johnson & Johnson yasimamishwe kwa sababu ya mgawanyiko usio wa kawaida uliotokea siku 6 hadi 13 baada ya mchakato wa chanjo kufanyika kwa wagonjwa wengine.

Ilitangazwa kuwa chanjo ya Covid-19 inayotolewa kwa dozi moja iliyotengenezwa na Johnson & Johnson, ambayo FDA iliidhinisha kutumika mnamo Februari 26, ilitolewa kwa watu takriban milioni 8 huko Marekani ambapo watu 15 kati yao walikuwa na msongamano wa damu usiokuwa wa kawaida uliosababisha watu 3 kufariki.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...